Tuhuma za mauaji: Nimehojiwa na Polisi, nimetimiza wajibu wangu

Maxence Melo

Maxence Melo

JF Founder
Staff member
Joined
Feb 10, 2006
Messages
2,882
Points
2,000
Maxence Melo

Maxence Melo

JF Founder
Staff member
Joined Feb 10, 2006
2,882 2,000
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.

Maxence


 
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2008
Messages
12,950
Points
2,000
Victoire

Victoire

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2008
12,950 2,000
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi.

Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.

Musiba ni nani nchi hii ?
 
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Messages
11,918
Points
2,000
britanicca

britanicca

JF-Expert Member
Joined May 20, 2015
11,918 2,000
Musiba kwanini anaruhusiwa kufanya haya?
Je kwa namna hii tunajenga Taifa gani?
Sidhani Kama Magufuli atastaafu nao wanaojipendekeza kwake,
Sina Hakika saana kama Polisi walipaswa kukuhoji wewe, maana nao ni watuhumiwa kama wewe kwa mjibu wa taarifa za Musiba,

Ningekuwa mimi ndo Mello Maelezo yangu yangekaa hivi,,
Ninaotuhumiwa kushirikiana nao kufanya njama kumuua Musiba wamenihoji,
Yaan nimemaliza maojiano na watuhumiwa wenzagu kwenye njama za kumuua Musiba"


Britannica
 
Mr Nyau

Mr Nyau

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2018
Messages
312
Points
1,000
Mr Nyau

Mr Nyau

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2018
312 1,000
Pole sana hata kwa maelezo mafupi haya yanatosha sana najua wapo masikio wazi na macho kodo kujua utaandika nini ili wajipange tena.

Hakuna kitu cha ajabu kama kutafuta attention kwa watu wakujue mimi sikuwahi kumjua mtu huyo kabla.

Nadhani hata watoto wake wakikukua watajua baba yao uzee wake kaumaliza kwa njaa mbaya sana..
 
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Messages
7,638
Points
2,000
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2018
7,638 2,000
Huyu Musiba naye ni jipu,mbona yeye hawa police hawamuiti kumuhoji tuhuma anazoandika kuwakashfu wengine?

Pole mkuu,ndiyo ukubwa huo,kuna kitu unacho unique wanataka wakukatishe tamaa,ila move on na endelea kukazia hapo hapo usirudi nyuma.

Na hili litapita......
 
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
6,360
Points
2,000
Crimea

Crimea

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
6,360 2,000
Mm na amini Musiba ni genge tu flani la kijinga linalotumiwa kututia kwenye mambo ya msingi katika Taifa hili.

Miaka ya nyuma yalikuwepo magazeti aina ya hayo ya msiba ila yenyewe yalikuwa yanajipambanua kama ni kutoka vyama pinzani, na kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwashambulia baadhi ya watu flani flani kwa mgongo wa kufichua ufisadi lkn kiuhalisia yalikuwa na kazi kama hii hii ya Musiba.

Naamini Musiba atapita na kuna wakati atakuja tutakuwa tunakula nae ugali huku mitaani, baada ya kibarua chake kuisha.
 
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
8,585
Points
2,000
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
8,585 2,000
Jibu: yupo upande wa mpini wa kisu anaowatukana wapo upande wa makali wa kisu.
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi. Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.Musiba ni nani nchi hii ?
 
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Messages
8,585
Points
2,000
Billie

Billie

JF-Expert Member
Joined Aug 13, 2011
8,585 2,000
Jibu: yupo upande wa mpini wa kisu anaowatukana wapo upande wa makali wa kisu.
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi. Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.Musiba ni nani nchi hii ?
 
Masanva Aya

Masanva Aya

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2016
Messages
241
Points
1,000
Masanva Aya

Masanva Aya

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2016
241 1,000
Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!
 
P

Pythagoras

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Messages
5,583
Points
2,000
P

Pythagoras

JF-Expert Member
Joined Feb 24, 2015
5,583 2,000
Hawajui tu kuishambulia JF nikuishambulia nchi nzima na wao wanajishambulia.

Hao polisi bila shaka walisema ni kwanini hawamuhoji Musiba ambaye ndiye mleta tuhuma na kwa.mujibu wa sheria mleta tuhuma ndiye mwenye wajibu wa kuthibitisa tuhuma zake.

Sote tunaelewa lengo la awamu hii ya tano.

Tuko.pamoja endelea kupambana utashinda, Mungu yuko pamoja nasi. Huyo.Musiba ipo siki atabaki peke yake.
 

Forum statistics

Threads 1,316,463
Members 505,652
Posts 31,891,271
Top