Tuhuma za mauaji: Nimehojiwa na Polisi, nimetimiza wajibu wangu

Maxence una akili saana..
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.

Maxence

Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi.

Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.

Musiba ni nani nchi hii ?
Ulishawahi kumuomba ushahidi akakunyima?
 
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi.

Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.

Musiba ni nani nchi hii ?
ukiwa upande wa chama cha kijani kama micba jua upo juu ya shelia pia wewe ni mteule wa mkuu pale magogoni unaweza ongea unavyo taka tukana viongozi wa upinzani pinga sela za upinzani fulaia akina mbowe wanavyo taabika huwezi guswa kabisa elewa ivyo ndugu yangu
 
Ndugu wana JF na watanzania kwa ujumla,

Nachukua fursa hii kuwashukuru wote mlioguswa kusikia nimeitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano baada ya magazeti mawili leo kunihusisha na linalodaiwa kuwa ‘Genge la Watu wanaopanga mikakati ya kumuua Cyprian Musiba”.

Genge hili lilihusisha wanasiasa, taasisi za serikali, watu binafsi (nikiwemo mimi) na hadi viongozi wa Taasisi za Serikali.

Si mara ya kwanza magazeti haya kufanya hivi kwangu na kwa watu wengi (ingawa kwangu imekuwa ikirudiwa kwa angle tofauti tofauti).

Naam, niliitwa saa 3 asubuhi (ingawa habari yenyewe ilitoka siku hiyo hiyo) na nikaambiwa nijitahidi niwe nimefika kabla ya saa 5; nikajitahidi kuitikia wito na kufika mnamo saa 4 na dk 30 asubuhi pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Nikiri, jopo la wachunguzi wa Jeshi la Polisi walioshiriki kwenye mahojiano nami walionyesha weledi katika kazi yao na hivyo kupelekea mimi na mwanasheria wangu kutoa maelezo yaliyohitajika katika sakata hili.

Nilihoji maswali ya msingi juu ya tuhuma ambazo zimekuwa zikitolewa na bwana huyu na nikahoji kinachopelekea mara zote vyombo vya dola kumwacha aendelee kuumiza watu. Aidha, nikiri pia kuwa maswali yote niliyouliza yalijibiwa kwa staha na undani wa mahojiano yetu nachelea kuuweka bayana kwani naweza kuvuruga uchunguzi.

Niseme: Nawashukuruni nyote mlioguswa na kunitafuta kwa njia mbalimbali kunitia moyo au kutaka kujua mnaweza kusaidiaje. Wengine mlijitoa kuwa tayari kwa dhamana kama ingehitajika, kitendo kilichonifariji kuwa watu wanaelewa tunasimamia nini na kwanini tunaendelea kukisimamia.

Kwa watanzania: Watu kama ndugu huyu wapo, tuzikatae kazi zao na wanaowatuma kwa nguvu zote; tusikubali kuletewa migawanyo inayokwepeka. Tuwakemee pale tunapoweza lakini tukibaini kuwa wana nguvu ya ziada, tumwombe Mungu akatende muujiza wake!

Once again, asanteni sana na Mungu asimame nasi katika kuijenga nchi yetu, Tanzania.

Maxence

Pole Sana mkuu, shetani hajawahi kumshinda Mungu...
 
Mkuu, kama unajihusisha na magenge ya wanasiasa uchwara wanaofanya mipango ya kudhuru watu wengine, au hata kumaliza maisha yao kabisa, achana nayo. Haiwezi kukujengea jina jema katika jamii, wala kukujenga kibiashara.
 
Pole ndugu Marcelo, unajua kuna vichaa wanaovalishwa na baba zao suti na tai, ukiwaona utasema huyu mtu ni mtu wa maana ama msomi mwenye kazi nzuri, lakini akifungua kinywa ama ukiona vitendo vyake , unabaki bumbuwazi.

Huyo ni musiba, nguvu yake ni ya soda, gesi itatoka na nanitakuwa flat siku za hivi punde.

Umevumilia mengi endelea kuvumilia na endelea kupiga hatua asikusitishe kwenye shughuli zako njema.
 
FB_IMG_1562767785453.jpg
all d best
 
Pole sana Max. Kinachonishangaza ni huyu Musiba kuachwa anaropoka ropoka hovyo kwa kuwatuhumu watu huku yeye wala hahojiwi.

Polisi walitakiwa wamuhoji huyo Musiba na ikiwezekana gazeti lake lifungiwe kabisa. Huwa anatuhumu watu bila ushahidi kabisa na anaachwa tu.

Musiba ni nani nchi hii ?
Ni mwananchi anayedai kuwa amejitoa muhanga kumtetea Mheshimiwa Rais na kutangaza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano.
 
Hong Kong raia wameandamana kupinga amendment ya "Extradition Bill" kwa kudai mtuhumiwa atakosa fair trial. Tanzania imepitishwa Cyber Act 2015, Sheria ya vyombo vya habari, Written Law (Miscellaneous amendment No. 3), Sheria ya Takwimu na Mafao nk Wananchi kimya, ELIMU ×3.
 
Back
Top Bottom