mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,580
- 9,821
Ni muda upatao miaka minne sasa umepita toka pale serikali ya awamu ya tano ilipoanza kugharamia elimu ya msingi, hivyo kuifanya ipatikane bure kwa watoto wa Kitanzania, hasa wale wenye vipato vya chini. Nimegusia kuhusu vipato vya wananchi, kwa kuwa ni jambo lililokuwa wazi kwamba wale wenye vipato vinono hawathubutu kabisa kufaidi huo ubure uliowekwa.
Nafikiri tunapaswa kupata tathimini halisi hivi sasa, ili tuweze kupata kufanya uamuzi, ama tuzidi kuendelea kushabikia ubure huu, ama serikali ijikite zaidi katika maeneo mengine ya kielimu yenye kuhusu stadi za kazi, elimu ya juu, sayansi na teknolojia.
Mimi kwa maoni yangu naona, serikali za CCM toka Ile ya awamu ya pili mpaka hii ya sasa, hupenda sana kujinadi kwa kupitia vitu rahisi kuweza kuonekana kwa sura za "quantitatives" badala ya "qualitatives" ili kuweza kuwahadaa watu wengi wasio na ufahamu mpana kwenye masuala nyeti yaihusuyo nchi yetu. CCM na serikali hufaidika na umbumbumbu wa wananchi wengi, jambo ambalo hata tafiti za TWAWEZA ziliweza kuthibitisha.
Ukifuatilia background yake, suala la utoaji bure wa elimu lilibuniwa na viongozi wa CDM, lkn CCM walidandia treni kwa mbele, walikuja kuliiga nahata kuliingiza ktk ilani yao ya 2015 kama njia mojawapo ya kuwavutia wananchi maskini na fukara, lkn lengo lao kubwa lilikuwa ni kura zao wakati wa uchaguzi. Hawakuwa na maandalizi wala udhati juu ya hilo, ndiyo maana hata watoto wa viongozi wa CCM hatumii fursa ya ubure uliopo kwa kuwa wanautambua uduni uliopo ktk ubora wake.
Labda, tathimini yetu ijikite kwenye ubora uliopo hivi sasa ktk elimu inayotolewa. Ili kuiweka hoja hii vyema, pengine tujiulize maswali yafuatayo ili tupate tafakari zaidi:
a) Je! Serikali imeweza kuweka kiwango cha chini cha ubora kwa elimu itolewayo hivi sasa?
b) Je! Bajeti inayotengwa inaweza kufikia ubora wa elimu unaotolewa na shule binafsi ya chini kabisa?
c) Je! Wabunge wengi wa CCM wanaridhika na ubora uliopo na hata kuridhia bajeti inayopitishwa kila mwaka?
d) Je! Kwa kuwa CCM huendeshwa na matamko, na pia kwa kuwa wanaridhika na ubora wake, itakuwa vyema tamko litolewe ili watoto wote wa viongozi wakasome huko ili wakapate kufaidi ubure na ubora wake?
e) Je! Serikali ipo tayari kukubali kufanya makongamano na wadau wa elimu nchi nzima ili kutetea ubora wa elimu hii ambayo inatolewa bure ili wananchi nao wapate kuchangia maoni yao?
Natambua changamoto nyingi ziwapatazo familia fukara na maskini za Kitanzania, lkn pia serikali haiwezi kujificha ndani yake na izidi kuwahadaa kupitia ubure huu. Ndiyo! Huwezi ukatenga kiwango kiduchu cha bajeti ktk masuala muhimu ya kisha kuanza kutoa majisifu kuwa unawajali watoto maskini wa Kitanzania.
Mimi nafikiri tusijielekeze ktk ubure bali ubora, serikali ije na mikakati ya wazi na iwe inatenga bajeti zaidi huku pia ikiwahimiza wazazi nao wawajibike kugharamia pia. Hasa kwa yale mambo ya msingi ambayo uongozi wa shule unaweza kuyaainisha kwa wazazi, ili nao wazidi kufanikisha ubora wa elimu kwa watoto wao..