RC Fatma Mwassa: Tupambane Kurejesha Ubora wa Elimu Kagera

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942

RC FATMA MWASSA: TUPAMBANE KUREJESHA UBORA WA ELIMU KAGERA

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa amewataka wananchi wa mkoa huo kuungana kwa pamoja kurejesha kiwango cha ufaulu katika mkoa huo ambacho amesema kimeendelea kushuka kwa miaka mitatu mfululizo.

Hajjat Mwassa ametoa rai hiyo kwenye maadhimisho ya Ruzinga Day ambayo yamefanyika kata ya Ruzinga wilaya ya Missenyi yenye lengo la kutathimini yaliyofanyika kwa kipindi cha mwaka mzima kwenye kata hiyo hususan yanayohusu maendeleo ya kijamii.

Pamoja na kupongeza juhudi na ubunifu wa uongozi wa Ruzinga Development RD kwa kuiandaa siku hiyo maalumu ambayo wamekuwa wakiadhimisha kwa miaka 17 sasa, amesema umoja huo umekuwa chachu kubwa ya maendeleo katika kata hiyo na kupelekea uanzishwaji wa miradi mbalimbali katika sekta ya elimu, Afya na Maji kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa Ruzinga.

Ameongeza kuwa ipo haja sasa ya kuongeza nguvu Zaidi katika kuboresha na kuongeza ufahulu ambao umeonekana kushuka kila mwaka kulinganisha na miaka ya nyuma ambayo kagera ilisifika kwa kuthamini elimu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Nkenge Florent Kyombo amewapongeza wanaumoja wa RD kwa namna wanavyopigania maendeleo ya kata yao kwa kushirikiana na serikali huku mwenyekiti wa umoja huo Dkt. Devid Rwechungula akiomba serikali na jamii kuweka mkazo kwenye ujenzi wa bweni la wavulana shule ya sekondari Ruzinga ili kuwanusuru vijana hao kutembea mwendo mrefu.
 

Attachments

  • thumb_611_800x420_0_0_auto.jpg
    thumb_611_800x420_0_0_auto.jpg
    50.7 KB · Views: 4
Wilaya ya Missenyi ina changamoto nyingi sana mbali ya kwamba kata ya Ruzinga imepiga hatua.. Mbunge wa Nkenge nguvu nyingi ameweka kiziba sehemu nyingine amesahau. Hebu fikiria kata Kassambya ambayo imebeba wilaya ya Missenyi umeme uko senta tu lakini ukitoka kwenye makao makuu ya Wilaya nje ya km 2/3 hamna umeme hii ni aibu kubwa sana. Ili elimu iweze kuimarika ni pamoja na kukuza miundombinu ikiwemo barabara, maji , umeme nk... Viongozi wa Wilaya Missenyi wanapaswa kujitathimini.
 
Back
Top Bottom