Tufanye tathimini sasa juu ya ubora wa elimu ya msingi itolewayo bure

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,574
9,814
Ni muda upatao miaka minne sasa umepita toka pale serikali ya awamu ya tano ilipoanza kugharamia elimu ya msingi, hivyo kuifanya ipatikane bure kwa watoto wa Kitanzania, hasa wale wenye vipato vya chini. Nimegusia kuhusu vipato vya wananchi, kwa kuwa ni jambo lililokuwa wazi kwamba wale wenye vipato vinono hawathubutu kabisa kufaidi huo ubure uliowekwa.​

Nafikiri tunapaswa kupata tathimini halisi hivi sasa, ili tuweze kupata kufanya uamuzi, ama tuzidi kuendelea kushabikia ubure huu, ama serikali ijikite zaidi katika maeneo mengine ya kielimu yenye kuhusu stadi za kazi, elimu ya juu, sayansi na teknolojia.

Mimi kwa maoni yangu naona, serikali za CCM toka Ile ya awamu ya pili mpaka hii ya sasa, hupenda sana kujinadi kwa kupitia vitu rahisi kuweza kuonekana kwa sura za "quantitatives" badala ya "qualitatives" ili kuweza kuwahadaa watu wengi wasio na ufahamu mpana kwenye masuala nyeti yaihusuyo nchi yetu. CCM na serikali hufaidika na umbumbumbu wa wananchi wengi, jambo ambalo hata tafiti za TWAWEZA ziliweza kuthibitisha.

Ukifuatilia background yake, suala la utoaji bure wa elimu lilibuniwa na viongozi wa CDM, lkn CCM walidandia treni kwa mbele, walikuja kuliiga nahata kuliingiza ktk ilani yao ya 2015 kama njia mojawapo ya kuwavutia wananchi maskini na fukara, lkn lengo lao kubwa lilikuwa ni kura zao wakati wa uchaguzi. Hawakuwa na maandalizi wala udhati juu ya hilo, ndiyo maana hata watoto wa viongozi wa CCM hatumii fursa ya ubure uliopo kwa kuwa wanautambua uduni uliopo ktk ubora wake.

Labda, tathimini yetu ijikite kwenye ubora uliopo hivi sasa ktk elimu inayotolewa. Ili kuiweka hoja hii vyema, pengine tujiulize maswali yafuatayo ili tupate tafakari zaidi:
a) Je! Serikali imeweza kuweka kiwango cha chini cha ubora kwa elimu itolewayo hivi sasa?
b) Je! Bajeti inayotengwa inaweza kufikia ubora wa elimu unaotolewa na shule binafsi ya chini kabisa?
c) Je! Wabunge wengi wa CCM wanaridhika na ubora uliopo na hata kuridhia bajeti inayopitishwa kila mwaka?
d) Je! Kwa kuwa CCM huendeshwa na matamko, na pia kwa kuwa wanaridhika na ubora wake, itakuwa vyema tamko litolewe ili watoto wote wa viongozi wakasome huko ili wakapate kufaidi ubure na ubora wake?
e) Je! Serikali ipo tayari kukubali kufanya makongamano na wadau wa elimu nchi nzima ili kutetea ubora wa elimu hii ambayo inatolewa bure ili wananchi nao wapate kuchangia maoni yao?

Natambua changamoto nyingi ziwapatazo familia fukara na maskini za Kitanzania, lkn pia serikali haiwezi kujificha ndani yake na izidi kuwahadaa kupitia ubure huu. Ndiyo! Huwezi ukatenga kiwango kiduchu cha bajeti ktk masuala muhimu ya kisha kuanza kutoa majisifu kuwa unawajali watoto maskini wa Kitanzania.

Mimi nafikiri tusijielekeze ktk ubure bali ubora, serikali ije na mikakati ya wazi na iwe inatenga bajeti zaidi huku pia ikiwahimiza wazazi nao wawajibike kugharamia pia. Hasa kwa yale mambo ya msingi ambayo uongozi wa shule unaweza kuyaainisha kwa wazazi, ili nao wazidi kufanikisha ubora wa elimu kwa watoto wao..
 
Elimu,usafiri wa wanafunzi vitakuwa bora endapo tu Sheria ikatungwa watetezi wa wanyonge wote ni lzm wasomeshe watoto wao hizi shule za kata,na wasitumie mav 8 kupelekea watoto wao shule Hapo elimu itakuwa bora zaidi ni ngonjera tu
 
Mimi tathmini yangu nitalifanya 2030 wakati Elimu bure wa Magufuli watapiga kura kwa mara ya kwanza.

P
 
Dah.....!
 
Ni lazima tutofautishe kati ya haya mambo mawili, tunajali ubora kwa maana ya thamani, ama wingi wa wanufaika wa ubure ambao unahubiriwa, ambao makada huja na takwimu zake.
 
Kwani ilivyokuwa inalipiwa ilikuwa ni bora? Tatizo ni elimu sio nzuri au tatizo ni bure? Je leo hii serikali ikitangaza elimu ilipuwe, je ndio itakuwa bora? Ubora wa elimu ni kilipiwa?
 
Mimi tathmini yangu nitalifanya 2030 wakati Elimu bure wa Magufuli watapiga kura kwa mara ya kwanza.

P

Keep in your mind that you will be 60+ by then! Will you be able to do any meaningful analysis?
 
Unaota kama 2030 kutakuwa na uchaguzi?
 
Keep in your mind that you will be 60+ by then! Will you be able to do any meaningful analysis?
Yes kuna two types of brain patterns, the vegetable pattern and the wine pattern. The vegetable rot as it gets old, the wine gets better as it stays longer.
Nitakuwepo!.
P
 
Kwani ilivyokuwa inalipiwa ilikuwa ni bora? Tatizo ni elimu sio nzuri au tatizo ni bure? Je leo hii serikali ikitangaza elimu ilipuwe, je ndio itakuwa bora? Ubora wa elimu ni kilipiwa?

Mkuu zamani elimu ilikuwa hailipiwi na bora kuliko hivi sasa na ilikuwa hivyo kwani utashi ulikuwa ni wa ukweli na sio siasa kama hivi sasa, hebu fikiria mfano wa darasa moja form one kuwa na watoto 800 huku wakiwa na madarasa mawili na walimu 100 tu kwa form 1-4? kweli tupo serious na elimu bora? watoto wanasoma kwa zamu ya masaa manne tu kwa siku ili kupisha kila mmoja angalau aingie darasani kweli hapo nani atashukuru hiyo elimu bure?
 
Wanafunzi Wa shule za uma ni majanga... Vilaza sijawai ona. Lakin wanafaulu..
 
Ni muda upatao miaka minne sasa umepita toka pale serikali ya awamu ya tano ilipoanza kugharamia elimu ya msingi, hivyo kuifanya ipatikane bure kwa watoto wa Kitanzania, hasa wale wenye vipato vya chini. Nimegusia kuhusu vipato vya wananchi, kwa kuwa ni jambo lililokuwa wazi kwamba wale wenye vipato vinono hawathubutu kabisa kufaidi huo ubure uliowekwa.

Nafikiri tunapaswa kupata tathimini halisi hivi sasa, ili tuweze kupata kufanya uamuzi, ama tuzidi kuendelea kushabikia ubure huu, ama serikali ijikite zaidi katika maeneo mengine ya kielimu yenye kuhusu stadi za kazi, elimu ya juu, sayansi na teknolojia.

Mimi kwa maoni yangu naona, serikali za CCM toka Ile ya awamu ya pili mpaka hii ya sasa, hupenda sana kujinadi kwa kupitia vitu rahisi kuweza kuonekana kwa sura za "quantitatives" badala ya "qualitatives" ili kuweza kuwahadaa watu wengi wasio na ufahamu mpana kwenye masuala nyeti yaihusuyo nchi yetu. CCM na serikali hufaidika na umbumbumbu wa wananchi wengi, jambo ambalo hata tafiti za TWAWEZA ziliweza kuthibitisha.

Ukifuatilia background yake, suala la utoaji bure wa elimu lilibuniwa na viongozi wa CDM, lkn CCM walidandia treni kwa mbele, walikuja kuliiga nahata kuliingiza ktk ilani yao ya 2015 kama njia mojawapo ya kuwavutia wananchi maskini na fukara, lkn lengo lao kubwa lilikuwa ni kura zao wakati wa uchaguzi. Hawakuwa na maandalizi wala udhati juu ya hilo, ndiyo maana hata watoto wa viongozi wa CCM hatumii fursa ya ubure uliopo kwa kuwa wanautambua uduni uliopo ktk ubora wake.

Labda, tathimini yetu ijikite kwenye ubora uliopo hivi sasa ktk elimu inayotolewa. Ili kuiweka hoja hii vyema, pengine tujiulize maswali yafuatayo ili tupate tafakari zaidi:
a) Je! Serikali imeweza kuweka kiwango cha chini cha ubora kwa elimu itolewayo hivi sasa?
b) Je! Bajeti inayotengwa inaweza kufikia ubora wa elimu unaotolewa na shule binafsi ya chini kabisa?
c) Je! Wabunge wengi wa CCM wanaridhika na ubora uliopo na hata kuridhia bajeti inayopitishwa kila mwaka?
d) Je! Kwa kuwa CCM huendeshwa na matamko, na pia kwa kuwa wanaridhika na ubora wake, itakuwa vyema tamko litolewe ili watoto wote wa viongozi wakasome huko ili wakapate kufaidi ubure na ubora wake?
e) Je! Serikali ipo tayari kukubali kufanya makongamano na wadau wa elimu nchi nzima ili kutetea ubora wa elimu hii ambayo inatolewa bure ili wananchi nao wapate kuchangia maoni yao?

Natambua changamoto nyingi ziwapatazo familia fukara na maskini za Kitanzania, lkn pia serikali haiwezi kujificha ndani yake na izidi kuwahadaa kupitia ubure huu. Ndiyo! Huwezi ukatenga kiwango kiduchu cha bajeti ktk masuala muhimu ya kisha kuanza kutoa majisifu kuwa unawajali watoto maskini wa Kitanzania.

Mimi nafikiri tusijielekeze ktk ubure bali ubora, serikali ije na mikakati ya wazi na iwe inatenga bajeti zaidi huku pia ikiwahimiza wazazi nao wawajibike kugharamia pia. Hasa kwa yale mambo ya msingi ambayo uongozi wa shule unaweza kuyaainisha kwa wazazi, ili nao wazidi kufanikisha ubora wa elimu kwa watoto wao..View attachment 1195155
Words
 
Kwani ilivyokuwa inalipiwa ilikuwa ni bora? Tatizo ni elimu sio nzuri au tatizo ni bure? Je leo hii serikali ikitangaza elimu ilipuwe, je ndio itakuwa bora? Ubora wa elimu ni kilipiwa?
Elimu bora ni mchezo wa bao
 
Nafikiri, suala sio elimu bure, bali ni ubora wa elimu inayotolewa. Elimu ya Tanzania, imekuwa duni tangu enzi za kulipia hadi sasa enzi za elimu bure. Kwa kiufupi, THERE IS A MISMATCH, BETWEEN OUR EDUCATION QUALIFICATIONS AND LABOUR MARKET DEMAND. Ndio maana changamoto za ajira ni nyingi, uwezo wa watu kujiajiri ni mdogo (japo kuna sababu nyingi katika hili la kujiajiri, ila sababu ya mfumo wa elimu unaomfanya mtu asifikirie nje ya box ipo pia),rate of problem solving is disproportional to the number of graduates we have, Ni ngumu sana kwa graduate wa Tanzania kufanya competition in business or labour outside the country. Pia, huwezi mkuta mtoto wa kiongozi yeyote wa kiserikali katila shule izi, wanajua zina mapungufu makubwa, hivyp, haziwafai watoto wao, ila sisi. Mfumo wa elimu unatufanya tuwe inferior, kuwa watu wasioweza kueleza kile wanachokijua with confidence na kuwa watu wa altenative solutions. Leo hii,mtu hadi anamaliza chuo, hajui hali halisi ya Taaluma yake ndani ya nchi, anaweza kufanya nini tofauti na kilichopo. Mbaya zaidi, mapungufu haya ya elimu, ambayo huzalisha wasomi wasiojua wamesoma nini, kwa sababu gani, hutumiwa kama mitaji ya kisiasa.
Mfumo wa elimu unahitaji mabadiliko makubwa sana, kuanzia mitaala, qualifications za waalimu, miundombinu ya shule. Haya yote yatakuwa clearly, kama tutakuwa na DIRA YA TAIFA, INAYOELEZEA TANZANIA INATAKA NINI, KWA SABABU GANI, KWA MUDA GANI NA KWA FAIDA YA NANI. Hiyo dira, itatuongoza kujua aina ya graduates tunaowahitaji, ili kukidhi haja za Taifa na hata ikiwezekana haja za kimataifa, aina ya waalimu wa kutupikia hawa wanafunzi (qualifications), aina ya mitaala, mazingira ya ufundishaji na mahitaji mengine.
 
Back
Top Bottom