Tucta yatakiwa kutomwalika Rais Jakaya Kikwete Mei Mosi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Tucta yatakiwa kutomwalika Rais Jakaya Kikwete Mei Mosi

 Send to a friend Friday, 25 February 2011 20:47

jk%20kampeni2.jpg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Hamida Shariff, Morogoro
BARAZA Kuu la Chama cha Wafanyakazi Wanataaluma na Watafiti (Raawu), limetaka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), kutomwalika tena Rais Jakaya Kikwete, sherehe za Mei Mosi, mwaka huu, iwapo madai yao yaliyowasilishwa serikalini mwaka jana yatakuwa hayajapatiwa ufumbuzi.

Akisoma maazimio ya baraza hilo, Mwenyekiti wa Raawu, Profesa Kiko Hamza, alitaka Tucta kuanza mchakato wa kufuatilia madai hayo, ikiwamo kiwango cha chini cha mshahara kinachoweza kukidhi gharama za maisha.

Profesa Hamza alisema mchakato huo uanze haraka iwezekanavyo Machi mwaka huu, iwapo hautaanza Raawu itashindwa kuvumilia dhuluma ya serikali kwa wafanyakazi wanaoteseka na kwamba, itakuwa ya kwanza kuanzisha mgomo.

Alisema tayari vyama vya wafanyakazi viliweka bayana kuwa, uwezo wa serikali kulipa mishahara mizuri upo kama ingejipanga kwenye kukusanya mapato na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima.

Kuhusu kodi ya mapato inayokatwa kwenye mishahara, Profesa Hamza alisema imekuwa mzigo mkubwa kwa wafanyakazi, kupitia vyama vyao walitaka kodi ipunguzwe kutoka asilimia 15 ya sasa hadi asilimia 9, lakini serikali ilipunguza asilimia moja, hali ambayo aliita kejeli na dharau.

Pia, Profesa Hamza alisema baraza linasikitishwa na hali mbaya ya huduma ya umeme nchini na kwamba, ni aibu kwa Taifa lenye miaka 50 tangu lipate uhuru kukosa umeme wa uhakika.

Alisema wanashangazwa na malumbano yanayoendelea nchini kuhusu mitambo ya kufua umeme ya Dowans na kutamka bayana kuwa, yanatia kichefuchefu na ishara ya kukosekana kwa uongozi na usimamizi thabiti wa shughuli za umma.

Kuhusu milipuko ya makombora ya Gongo la Mboto, Profesa Hamza alisema baraza kuu limesikitishwa na tukio hilo na limetoa pole kwa waathirika na kutaka serikali kuweka bayana sababu za milipuko hiyo mara mbili kipindi cha miaka miwili.

Pia, alisema baraza hilo lilipongeza vyombo vya habari kwa kazi nzuri vinayofanya kuelimisha na kuhabarisha wananchi masuala mbalimbali.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Friday, 25 February 2011 21:09 Comments




0 #5 GILLIARD 2011-02-26 08:21 Mei Mosi ndiyo siku ya maandamano nchi nzima na ndio siku ya kukitoa chama cha Mapinduzi CCM na Serekali yake madarakani.
Quote









+1 #4 fredy chokela 2011-02-26 07:25 Hakuna pingamizi hapo maana JK anawaona wafanyakazi kama [NENO BAYA] fulani au haoni mfano wa Gadafi licha ya wananchi wake kuandamana ila kaamua kuwaongezea wafanyakazi mishahara kwa 150% kwa ajili ya kupanda kwa ghalama za maisha, hivi JK yeye haoni ghalama ya maisha imepanda au ndoo kusema viongozi wa TZ wana dhalau kwa wananchi???????????
Quote









+1 #3 Emily Kashingo 2011-02-26 07:02 Na serikali ina uwezo wa kuwalipa walimu laki 7 kwa kiwango cha chini ni kwa sababu tu serikali yetu inatudhulumu lakini sasa wakati umefika ni mwisho sasa tunataka haki zetu,serikali ya kikwete imeshindwa bora waondoke mapema kabla mambo hayajaiva.
Quote









+1 #2 Emily Kashingo 2011-02-26 06:56 Nyie ndo wakombozi wetu jaman kwa sisi walala hoi,haiwezekani wabunge na wakurugenzi na mawaziri wapewe mamilioni halafu walimu wapewe laki 3 mwalimu wa degree.Haiwezekani hilo gape ni kubwa mno lazima tukae chini tuelewane ama sivyo amani ivurugike Tanzania lakini hatukubali kuteseka hivi.
Quote









+1 #1 Bakari 2011-02-26 05:44 Wasomi wameanza kusoma ishara za nyakati; mabadiliko ya maana duniani kote yanaanzhishwa na wasomi, nashangaa mmekaa kimya siku zote. Anyway, hamjachelewa, songeni mbele!
Quote

 
The legitimacy of Jk to reign terror upon us is on nadir days.....................................................................
 
Naungana kwa asilimia 1,000 kwamba jk asialikwe kwenye sikukuu ya mei mosi na siku hiyo litolewe tamko zito kuhusu mpango kamili wa wafanyakazi nchini endapo serikali haitapandisha kima cha chini cha mshahara.
 
Siku za Mei Mosi kila mwaka inatakiwa iwe ni siku ya wafanyakazi kudai haki zao toka kwa WAAJIRI, si siku ya KUWASIKILIZA WAAJIRI, na watoa hotuba inapaswa wawe ni VIONGOZI WA WAFANYAKAZI (VYAMA VYA WAFANYAKAZI), na kamwe isiwe Rais.

My take: Asialikwe kabisa, hata miaka ijayo. Akitaka aje kusikiliza tu kama raia wengine, na kamwe si kuhutubia.
 
Sijui kwa nini tucta wana utaratibu wa kualika rais wakati hii siku yeye haimuhusu!
 
Sijui kwa nini tucta wana utaratibu wa kualika rais wakati hii siku yeye haimuhusu!
Imerithiwa toka mfumo wa (Chama kimoja) cha kikomunisti. Sijawahi kusikia nchi yenye demokrasia ya kweli kuwaalika maraisi hata kama ni wa kutoka itikadi moja. TUCTA inapaswa kuusitisha utaratibu huu.
 
Asialikwe mpaka anaondoka Ikulu,hv jamani wafanyakazi mmesahau ile hotuba yake eti "Na sizihitaji kura zenu" na maneno mengine kibao ya kutowajali,kutowathamini na kuwadhalilisha wafayakazi halafu aalikwe nitwashangaa sana TUCTA.Kwa ile hotuba yake wala haina haja ya kujiuliza ni asialikwe forever
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom