Mzee Ngonyani
JF-Expert Member
- Dec 16, 2022
- 826
- 1,881
Picha: Ester Bulaya
Ninashangaa pamoja na baadhi ya wabunge kuwapigania wafanyakazi kuhusu kubadilisha kikokotoo kinachowanyonya wafanyakazi, Wakiongozwa na mbunge Ester Bulaya lakini viongozi wa TUCTA wamekaa kimya. Hiyo ndo dalili ya usaliti sio bure mtakuwa na maslahi fulani mnapata. Katibu na Mwenyekiti mjitokeze kukanusha kuwa ninyi sio sehemu ya wale waliokubaliana kupitisha kikokotoo cha kinyonyaji.
Halafu mnapangia mstaafu umri wa kuishi duniani eti aishi miaka kumi na mbili na nusu baada ya kustaafu halafu mwisho wake ataishije. Wastaafu wengi sasa hivi wanaishi zaidi ya miaka sabini.
Bahati mbaya hao mawaziri mnaojadiliana nao wenyewe wakimaliza muda wao hupewa hela zao zote, hawasubili miaka 55 au 60. Hata kama mnataka uteuzi yawapasa kutimiza majukumu yenu ya kumsaidia mfanyakazi ambae amekufanya uwe hapo na huyo waziri au serikali ikuone.
Solidarity forever.