TUCTA kuitisha mgomo nchi nzima

TUCTA kuitisha mgomo nchi nzima

Tukta hamna huo ujanja.mkiona uchaguzi umekaribia wa vyama vyenu mnaanza uongo.
 
Hawa ni wa hovyo kabisa...kati ya trade union zinazopaswa kuwa imara ni kama hii...lakini hakuna kitu

By the way vongozi wake wote ni watu wa system
 
Hivi MGAYA ndo nilie muona juzi kavaa shati la CCM na yuko na wanaCCM au majicho yangu yaliona vibaya
 
Hatuna chama cha wafanyakazi hapa ni wahuni hawa. hawana uwezo wa kugoma
 
TUCTA hawana ubavu huo hata kidogo, kwanza wangeanza kupinga yale maagizo ya kijinga yanayotolewa na wakurugenzi wa halmashauri kama vile;kusaini daftari la mahuzurio kwa lazima kwenda kuwapokea viongozi wa ccm ambao si waserikali,kukatwa fedha kwa ajili ya mafuta ya mwenge nk! Hawana ishu hao kwani wao pia ni familia ya ccm!
 
TUCTA ipi??? hii ambayo waliambiwa akili za kuambiwa changanya na zako,wakaufyata.?? kama ni hao....HAKUNA JIPYA HAPO....MANENO MATUPU
 
Tataizo hivi vyama vya wafanyakazi ni kukosa uongozi imara na wanaongwa kirahisi sana na wanawaangusha wafanyakazi has a MTU kama mkoba huyu jamaa huwa anatafuta deal ili apewe chake tu
 

Mukoba1-300x201.jpg



SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), linatarajia kuitisha mgomo wa wafanyakazi nchi nzima, endapo Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) haitaondoa kanuni mpya ambayo inaruhusu watumishi watakaostaafu kwa hiari yao kukatwa asilimia 18 ya mafao yao.

Kanuni hiyo mpya itaanza kutumika Julai mwaka huu ambapo watumishi watakaostaafu kwa hiari watalazimika kukatwa kiasi hicho.

Ili kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa ndani ya muda mwafaka, TUCTA imeazimia kuitisha mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Aprili 23 na 24, mwaka huu ili kujadili suala hilo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Rais wa shirikisho hilo, Gratian Mukoba alisema kanuni hiyo ni kandamizi na inawanyima haki watumishi kwa sababu kulipwa mafao ni haki ya mtumishi aliyestaafu, ingawa pia wakati wanajadili kuipitisha hawakushirikishwa.

“Tutawahamasisha watumishi kugoma nchi nzima ili kuishinikiza SSRA kubadili kanuni hii kwa sababu ni kandamizi kwa mtumishi.

“Bila ya kufanya hivi, Serikali itaendelea kutunga kanuni nyingine ambazo zinaweza kutoa nafasi kwa watumishi kuendelea kufanya kazi hadi miaka 70 ili wakifariki kabla ya muda huo wawe wamepoteza mafao yao, kutokana na hali hii, hatutakubali na tunataka iondolewe mara moja,”alisema Mukoba.

Alisema kutokana na hali hiyo, shirikisho hilo linasubiri majibu ya barua hiyo na endapo hawasikilizwa watafanya mgomo huo.

“Baada ya kuona kanuni hii haifai, tumewaandikia barua SSRA ili waweze kutupa ufafanuzi,ikiwa hawajatupa majibu tutawahamasisha watumishi nchi nzima kugoma kama walivyofanya madereva,”alisema.

Alisema wakati SSRA inapitisha kanuni hiyo, tayari Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliiagiza mamlaka hiyo kurudi meza ya mazungumzo na wadau ili waweze kujadili kanuni tata inayoelekeza SSRA kutoa asilimia 25 badala ya asilimia 50 ya mafao yao.

“Bado tupo kwenye mgogoro na SSRA kuhusiana na kanuni tata ambayo inatumika sasa ya kutulipa asilimia 25 badala ya asilimia 50 ya mafao yetu,”alisema.

Alisema tangu agizo hilo litolewe hakuna utekelezaji wowote badala yake wameamua kutunga kanuni nyingine ambayo ni kandamizi zaidi.

Afisa Uhusiano wa SSRA, Sarah Kibonde alipoulizwa juu ya madai hayo, alisema kanuni mpya ya ukokotoaji haijaweka kiwango hicho cha makato na kanuni inahusu wafanyakazi walioajiriwa kuanzia Julai mwaka jana.

CHANZO: Mtanzania(15/04/2015)




Mbali na udhaifu wa TUCTA, hizi sheria wengine mnazionaje? Huu ni wizi!
Unakatwa 18% kwenye hela yako yote au ni kwenye ile tu iliyoongezwa na mfuko?

Kuna haja ya kuandaa takwimu itakayoonesha rekodi ya uchangiaji kodi serikalini ili kufanya ulinganifu wa uchangiaji kwa kila sekta.
Ionekane mfanyabiashara kachangia shilingi ngapi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Mwalimu, mbunge, polisi, majaji, n.k, n.k.
 
Mimi niko tayari. Kwanza wamenihudhi
sana , mimi nategemea kustaafu kwa hiyari hivi
karibuni nilivutiwa na mafao nitakayoliwa ,
sasa wakikata 18% ni sawa na kama milion
ishirini na ushee nani atakubali kupoteza
fedha zote hizo!!? na kazi nimechoka nataka muda wa kucheza na wajukuu.

Mimi nilivyoelewa ni kuwa kanuni hiyo itaanza kutumika kwa watumishi walioajiriwa kuanzia mwezi julai 2014 au pengine nilielewa vibaya ?? Eeeeh
 
Kiukweli hawa wasiseme lolote wapuuzi tu. Migomo wanajua madereva na wafanyabiashara
 
Hivi MGAYA ndo nilie muona juzi kavaa shati la CCM na yuko na wanaCCM au majicho yangu yaliona vibaya

Ndiyo yeye mkuu haukukosea , Mimi mwenyewe ilibidi nisogelee Luninga kwa karibu , na nikaangalia channel 3 tofauti nikathibitisha , yaani baada ya kuangalia ile taarifa eti anatetea katiba ya joka lenye makengeza niliuzunika sana yaani sikupata usingizi siku ile
 
Back
Top Bottom