TUCTA kuitisha mgomo nchi nzima

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698

Mukoba1-300x201.jpg

SHIRIKISHO la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), linatarajia kuitisha mgomo wa wafanyakazi nchi nzima, endapo Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) haitaondoa kanuni mpya ambayo inaruhusu watumishi watakaostaafu kwa hiari yao kukatwa asilimia 18 ya mafao yao.

Kanuni hiyo mpya itaanza kutumika Julai mwaka huu ambapo watumishi watakaostaafu kwa hiari watalazimika kukatwa kiasi hicho.

Ili kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa ndani ya muda mwafaka, TUCTA imeazimia kuitisha mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika Aprili 23 na 24, mwaka huu ili kujadili suala hilo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na MTANZANIA mjini Dar es Salaam jana, Rais wa shirikisho hilo, Gratian Mukoba alisema kanuni hiyo ni kandamizi na inawanyima haki watumishi kwa sababu kulipwa mafao ni haki ya mtumishi aliyestaafu, ingawa pia wakati wanajadili kuipitisha hawakushirikishwa.

"Tutawahamasisha watumishi kugoma nchi nzima ili kuishinikiza SSRA kubadili kanuni hii kwa sababu ni kandamizi kwa mtumishi.

"Bila ya kufanya hivi, Serikali itaendelea kutunga kanuni nyingine ambazo zinaweza kutoa nafasi kwa watumishi kuendelea kufanya kazi hadi miaka 70 ili wakifariki kabla ya muda huo wawe wamepoteza mafao yao, kutokana na hali hii, hatutakubali na tunataka iondolewe mara moja,"alisema Mukoba.

Alisema kutokana na hali hiyo, shirikisho hilo linasubiri majibu ya barua hiyo na endapo hawasikilizwa watafanya mgomo huo.

"Baada ya kuona kanuni hii haifai, tumewaandikia barua SSRA ili waweze kutupa ufafanuzi,ikiwa hawajatupa majibu tutawahamasisha watumishi nchi nzima kugoma kama walivyofanya madereva,"alisema.

Alisema wakati SSRA inapitisha kanuni hiyo, tayari Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliiagiza mamlaka hiyo kurudi meza ya mazungumzo na wadau ili waweze kujadili kanuni tata inayoelekeza SSRA kutoa asilimia 25 badala ya asilimia 50 ya mafao yao.

"Bado tupo kwenye mgogoro na SSRA kuhusiana na kanuni tata ambayo inatumika sasa ya kutulipa asilimia 25 badala ya asilimia 50 ya mafao yetu,"alisema.

Alisema tangu agizo hilo litolewe hakuna utekelezaji wowote badala yake wameamua kutunga kanuni nyingine ambayo ni kandamizi zaidi.

Afisa Uhusiano wa SSRA, Sarah Kibonde alipoulizwa juu ya madai hayo, alisema kanuni mpya ya ukokotoaji haijaweka kiwango hicho cha makato na kanuni inahusu wafanyakazi walioajiriwa kuanzia Julai mwaka jana.

CHANZO: Mtanzania(15/04/2015)
 
jamani tunaibiwa na serikali,fedha zangu nazitaka halafu wewe unakata.TUCTA hata senti wasikate
 
hawa nao wametuchosha kwa kutishia kwao...mbona hakuna hata siku waliwahi kutekeleza matishio yao...wadhaifu tu hao!
 
mukoba1-300x201.jpg

shirikisho la vyama vya wafanyakazi tanzania (tucta), linatarajia kuitisha mgomo wa wafanyakazi nchi nzima, endapo mamlaka ya usimamizi wa mifuko ya hifadhi ya jamii (ssra) haitaondoa kanuni mpya ambayo inaruhusu watumishi watakaostaafu kwa hiari yao kukatwa asilimia 18 ya mafao yao.

kanuni hiyo mpya itaanza kutumika julai mwaka huu ambapo watumishi watakaostaafu kwa hiari watalazimika kukatwa kiasi hicho.

ili kuhakikisha suala hilo linashughulikiwa ndani ya muda mwafaka, tucta imeazimia kuitisha mkutano mkuu unaotarajiwa kufanyika aprili 23 na 24, mwaka huu ili kujadili suala hilo.

akizungumza katika mahojiano maalumu na mtanzania mjini dar es salaam jana, rais wa shirikisho hilo, gratian mukoba alisema kanuni hiyo ni kandamizi na inawanyima haki watumishi kwa sababu kulipwa mafao ni haki ya mtumishi aliyestaafu, ingawa pia wakati wanajadili kuipitisha hawakushirikishwa.

"tutawahamasisha watumishi kugoma nchi nzima ili kuishinikiza ssra kubadili kanuni hii kwa sababu ni kandamizi kwa mtumishi.

"bila ya kufanya hivi, serikali itaendelea kutunga kanuni nyingine ambazo zinaweza kutoa nafasi kwa watumishi kuendelea kufanya kazi hadi miaka 70 ili wakifariki kabla ya muda huo wawe wamepoteza mafao yao, kutokana na hali hii, hatutakubali na tunataka iondolewe mara moja,"alisema mukoba.

alisema kutokana na hali hiyo, shirikisho hilo linasubiri majibu ya barua hiyo na endapo hawasikilizwa watafanya mgomo huo.

"baada ya kuona kanuni hii haifai, tumewaandikia barua ssra ili waweze kutupa ufafanuzi,ikiwa hawajatupa majibu tutawahamasisha watumishi nchi nzima kugoma kama walivyofanya madereva,"alisema.

alisema wakati ssra inapitisha kanuni hiyo, tayari waziri mkuu, mizengo pinda aliiagiza mamlaka hiyo kurudi meza ya mazungumzo na wadau ili waweze kujadili kanuni tata inayoelekeza ssra kutoa asilimia 25 badala ya asilimia 50 ya mafao yao.

"bado tupo kwenye mgogoro na ssra kuhusiana na kanuni tata ambayo inatumika sasa ya kutulipa asilimia 25 badala ya asilimia 50 ya mafao yetu,"alisema.

alisema tangu agizo hilo litolewe hakuna utekelezaji wowote badala yake wameamua kutunga kanuni nyingine ambayo ni kandamizi zaidi.

afisa uhusiano wa ssra, sarah kibonde alipoulizwa juu ya madai hayo, alisema kanuni mpya ya ukokotoaji haijaweka kiwango hicho cha makato na kanuni inahusu wafanyakazi walioajiriwa kuanzia julai mwaka jana.

chanzo: mtanzania(15/04/2015)

hahahaha mmeshasahau maji ya washawasha?hii nchi ina track record mbaya sana ya haki za binadamu,ref david mwangosi etc
 
Mimi niko tayari. Kwanza wamenihudhi
sana , mimi nategemea kustaafu kwa hiyari hivi
karibuni nilivutiwa na mafao nitakayoliwa ,
sasa wakikata 18% ni sawa na kama milion
ishirini na ushee nani atakubali kupoteza
fedha zote hizo!!? na kazi nimechoka nataka muda wa kucheza na wajukuu.
 
Tucta + talgwu + chama cha walimu tanzania = mamluki wa chama chetu chajenga nchi
 
kwahiyo hiyo barua wakijibiwa hawatagoma? kwani madereva juzi waliandika barua wapi? upuuzi huu wa Gracia mkoba hadi lini... nawasikitikia wafanyakazi wa inji hii wanaomtegemea mkoba...
 
Ccm imeshindwa nchi wanatakiwa wapumzike mpaka leo mfuko wa wastafu pspf hawajawalipa wastafu hela zao za miezi mitatu, nakumbuka maneno ya Padri moja alivyosema Ccm ndio watakuwa wakwanza kuleta machafuko nchini
 
TUCTA na Walimu ni moja kati ya taasisi weak sana hapa nchini. Hawawezi kumobilize mgomo na wakafanikiwa.
 
Back
Top Bottom