Tucheke sote

Tucheke sote

Bukwabi

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
3,352
Reaction score
1,154
Wakati Bank moja inavamiwa nikapiga 112 nikajibiwa "Karibu jeshi la Police TZ kitengo cha dharura for Kiswahili press 1 for English press 2", nikabonyeza 1 Sauti ikasema "Kwa ajali za barabarani au moto bonyeza 1 kwa ujambazi bonyeza 2".

Nikabonyeza 2, sauti ikasema "kama majambazi wana panga, rungu au visu bonyeza 1, pisto bonyeza 2, SMG bonyeza 3. AK 47 bonyeza 4, bomu bonyeza 5, Kama wanavyo vyote bonyeza 6".

Nikabonyeza 6, sauti ikasema "Ungekuwa wewe ni polisi ungeenda? Au unataka sifa ili uonekane unajua kutoa taarifa za matukio?
Acha hizo kwani sisi hatuogopi kufa?

Kwanza umekosea namba hapa ni Tanesco.
 
Back
Top Bottom