Tubadilike sasa. Si king'amuzi ni kisimbuzi

Tubadilike sasa. Si king'amuzi ni kisimbuzi

Raia Fulani

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2009
Posts
11,866
Reaction score
4,264
Tunapohama toka analojia kwenda digiti neno 'king'amuzi' limeshamiri sana. Ndipo majuzi kupitia Radio One kwenye kipindi cha lugha ya kiswahili Jumamosi waendesha kipindi wakawa wanajadili haya.

King'amuzi ni detector. Mfano vile vibao vinavyotumika kupapasia sehemu za vizuizi na kwenye maofisi ni ving'amuzi. Vinang'amua uwepo wa kitu kisicho cha kawaida na ndio maana vinatoa mlio.

Decoder (codec)-code-decode ni kutafsiri toka mfumo mmoja kwenda mwingine mfano mawimbi ya analojia kwenda digiti. Na kiswahili chake kutokana na wataalam ni kisimbuzi. Linatokana na neno 'simba'-ficha. Halafu 'simbua'. Hivyo kifaa cha kusimbua kuitwa kisimbuzi
 
Hakuna haja ya kuendekeza sana hii kitu kwa sababu LUGHA ni mfumo
wa sauti za nasibu, hilo jina halipendezi zaidi ya king'amuzi na ni ngumu
kuwalazimisha watu kutumia majina hayo yanayotoka vikaoni ndio maana
kwenye kiswahili kuna maneno yana utata kwani yanatafsirika zaidi ya
mara moja.
1.NDEGE - Ipo inayopaa angani pia kuna kiumbe anaitwa ndege
2.Mbuzi - Ya kukunia nazi na Mnyama
3.Barabara- Ya kupita magari au jambo lililofanyika vizuri
4.Mpaka.....................
5. Mama huruma...........
6.Mwanga.................
7.Mzee wa Busara................
N.k
 
Kwa majina yote duniani king'amuzi kinabaki kuwa ni program amboyo ilifeli katika maisha ya Mtanzania,kwa taarifa yako hapa Dar asilimia 70% ya wakazi wa Dar hawaangalii tena taarifa ya habari maana hawana uwezo wa hicho king'amuzi
 
Kwanini Bakita wasitumie maneno ambayo yameshakuwa maarufu mtaani badala ya kulazimisha maneno yao?

Wajua Laptop ni komputa mpakato? neno refuuuuuuuu!!!!!!
 
Hakuna haja ya kuendekeza sana hii kitu kwa sababu LUGHA ni mfumo
wa sauti za nasibu, hilo jina halipendezi zaidi ya king'amuzi na ni ngumu
kuwalazimisha watu kutumia majina hayo yanayotoka vikaoni ndio maana
kwenye kiswahili kuna maneno yana utata kwani yanatafsirika zaidi ya
mara moja.
1.NDEGE - Ipo inayopaa angani pia kuna kiumbe anaitwa ndege
2.Mbuzi - Ya kukunia nazi na Mnyama
3.Barabara- Ya kupita magari au jambo lililofanyika vizuri
4.Mpaka.....................
5. Mama huruma...........
6.Mwanga.................
7.Mzee wa Busara................
N.k

Mkuu GAZETI hapana. Nomino ulizotaja: NDEGE, MBUZI, BARABARA, MWANGA na naongeza KANGA, KAMBA n.k. hazina uhusiano wowote na muundo, sayansi, teknolojia ama ufanano wowote na kitu husika. Vifungu vya maneno "Mama huruma" na "Mzee wa busara" ni lugha za mtaani na si Kiswahili sanifu, hivyo havina uhalali wa kuwa hoja. Labda unachanganya na nahau kama "Ana kichwa kikubwa (ana kiburi)" n.k. ambazo ni rasmi katika sarufi ya Kiswahili.

KISIMBUZI
Kama neno "kisimbuzi" ndilo sahihi basi tutumie hilo. Hii habari ya "wameshazoea kusema king'amuzi hivyo tutumie hilohilo" haina mashiko. Neno king'amuzi ni istilahi (technical term) na limeundwa kuakisi sayansi inayoongoza teknolojia husika kama ambavyo kisimbusi linaakisi sayansi/teknolojia husika. Hata lugha zingine huheshimu hili, kwa mfano neno LASER ni kifupi cha Light Amplification by Stimulated Emission of Radiation, au maneno Computer na Calculator yametokana na maneno (vitenzi) Compute na Calculate, sasa kama kuna watu wanashindwa kuzoea kutamka LEZA (LASER, ama Computer ama Calculator basi wamepitwa na wakati.

Ikiwa ni kweli sisi Watanzania "hatuwezi" kulizoea neno kisimbuzi kwa kuwa ni "gumu" na "tumeshazoea king'amuzi (makosa)" basi kuna jambo kubwa (baya) linaloonesha uwezo wa bongo zetu. Nitasikitika ikiwa nitajua kuwa "ukweli" huu ni ukweli.

Tusisitize weledi.
 
Last edited by a moderator:
Kwani hawa watu wa BAKITA walikuwa wapi muda wote huo mpaka ili neno king'amuzi likapata mashiko. Acha wananchi wa kawaida viongozi wa serikali nao wanakiita king'amuzi ua awakuwa na jina lake ndiyo sasa wamelipata?
 
Mkuu GAZETI hapana. Nomino ulizotaja: NDEGE, MBUZI, BARABARA, MWANGA na naongeza KANGA, KAMBA n.k. hazina uhusiano wowote na muundo, sayansi, teknolojia ama ufanano wowote na kitu husika. Vifungu vya maneno "Mama huruma" na "Mzee wa busara" ni lugha za mtaani na si Kiswahili sanifu, hivyo havina uhalali wa kuwa hoja. Labda unachanganya na nahau kama "Ana kichwa kikubwa (ana kiburi)" n.k. ambazo ni rasmi katika sarufi ya Kiswahili.

KISIMBUZI
Kama neno "kisimbuzi" ndilo sahihi basi tutumie hilo. Hii habari ya "wameshazoea kusema king'amuzi hivyo tutumie hilohilo" haina mashiko. Neno king'amuzi ni istilahi (technical term) na limeundwa kuakisi sayansi inayoongoza teknolojia husika kama ambavyo kisimbusi linaakisi sayansi/teknolojia husika. Hata lugha zingine huheshimu hili, kwa mfano neno LASER ni kifupi cha Light Amplification by Stimulated Emission of Radiation, au maneno Computer na Calculator yametokana na maneno (vitenzi) Compute na Calculate, sasa kama kuna watu wanashindwa kuzoea kutamka LEZA (LASER, ama Computer ama Calculator basi wamepitwa na wakati.

Ikiwa ni kweli sisi Watanzania "hatuwezi" kulizoea neno kisimbuzi kwa kuwa ni "gumu" na "tumeshazoea king'amuzi (makosa)" basi kuna jambo kubwa (baya) linaloonesha uwezo wa bongo zetu. Nitasikitika ikiwa nitajua kuwa "ukweli" huu ni ukweli.

Tusisitize weledi.

mkuu nashukuru sana kwa ufafanuzi wako wa kitaalam. Mazoea mabaya. Fursa ya kufahamishwa usahihi inapojitokeza ni jambo jema sana ila sie huwa wakaidi kukubali ukweli huo. Neno la decoder lingekuwa halina ugumu kama kisimbuzi, ingekuwa rahisi kwa wadau kulitumia. Kosa siku zote haliwezi kuwa vema kwa kisa tu hutaki kukubali kuwa ni kosa.
 
Last edited by a moderator:
Siku zote ni ngumu kukubali mabadiliko, kukosea kitu au jambo kwa mazoea hakufanyi kitu au jambo hilo kuwa sahihi. Decoder siyo king'amuzi!
 
Bakita wanazingua.
Eti kichongeo cha penseli kinaitwa KIFIRIO
 
Back
Top Bottom