Tuanze upya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuanze upya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 17, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 17, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Kwenye riadha na baadhi ya michezo mingine kuna kitu kinachoitwa 'False start". Hii inatokea pale ambapo kwa mfano mkimbiaji anaanza kukimbia kabla bastola haijapigwa (kutokana na papara au kitu kingine) au ameanza kinyume na taratibu nyingine. Hilo linapotokea wakimbiaji wote hurudishwa mstarini na kuanza moja.

  Najiuliza kuwa yawezekana kama TAifa we had a false start and now we need to restart the building of our nation.

  Kama tukiamua kuanza upya:

  a. Tufute kesi zote za mafisadi
  b. wenye kusahamewa ndiyo wasamehewe (kilichoenda kwa "mganga"! na iwe kama sandakalawe!
  c. Panga upya vikosi vyote,
  d. Pangua upya safi nzima ya uongozi na kupanga upya
  e. andaa ajenda mpya ya taifa

  n.k !

  And then let see if we can start right!
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Feb 17, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Mkuu wangu tatizo sio false start hata kidogo isipokuwa wakimbiaji wetu wote kiuchumi ni vilema wa akili katika mbio hizo..
  Kila siku tunatafuta magongo (donors) tuanze mbio zetu, hivi kweli unafikiria tutaweza kuanza vizuri vipi ikiwa hao wenzetu wanalipwa na sponsors ktk mavazi yao iwe hata kuvaa kofia tu...
  Mshindani mzuri siku zote ni lazima awe mtu aliyejiandaa na mbio hizo kimwili na kiakili wakati sisi matayarisho yetu tunatafuta mkate wa kula kwa siku moja..
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sisi hawa au wengine? Mimi bado nina matumaini na hawa ASKARI wetu wawili mmoja MWANAJESHI (JK); na mwingine mtu wa UwT (Pinda), ambao naamini wanajua vizuri nchi ilikofikishwa sasa.
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu, tunaweza kufanya lolote hapa ila sikuachia mafisadi na mali zetu. Tunaweza kuunda tume ya ukweli na maridhiano lakini kwanza kila kilicho chetu watupatie kama wanataka tuanze moja! Sasa utaanza vipi moja wakati watu wengine wamechukua vifaa vyako na kukimbia kiasi kwamba mbio zinapoanza wao tayari wako mbele kama mita 5500 kati ya 10000. Hatuwezi kufika namna hiyo. Hata hivyo kama wazo lako likifanyiwa marekebisho lina kitu cha maana ndani yake!
   
 5. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Macho yangu yaona kitu tofauti kabisa. Hata hivyo aisifuye mvua imemnyea au unasemaje??:rolleyes:
   
 6. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mzee mwanakijiji..
  I first give u congrats for u a opinions. For real, and if i have to be honest, I appreciate u a work. Sioni haja ya kuanza upya mkuu maana kama ni hivyo tutaajikuta kila baada ya muda tunaanza upya! serikali yetu, katika mantiki ya mfano wako, ni kama wakimbiaji waliokwenda china mwaka jana pasipo kujua wamekwenda kufanya nini. Lengo lilikuwa ni Tanzania tupeleke wawakilishi. Basi. Serikali ya sasa hata tukiipa nafasi tena itakosea tuu. Haiwezi kufanya kazi. Haifanyi kazi na haijui kwanini ipo madarakani!.............

  Wanasema mti ukiupinda sana unavunjika, kadhalika mpira ukiuvuta sana unakatika. The same applies to a huge system which will always plant the seeds of its own destruction, just like colonialism and so does the CCM. Kwa sasa wanakufa maji, hawaachi kutapatapa. hata kuku katika dakika za mwisho za kukata roho hurusha miguu na hatuwezi kumrudishia uhai kwa matumaini kwamba atapona, labda tummalizie au tumwache afe taratibu. lakini kwa vyovyote, ni lazima afe, ili tuanze upya!
   
 7. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Upo sawa kabisa na ukumbuke si kila mwenye macho anaona
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sio kwamba nawasifu hawa. Ni wao na CCM yao ndio waliotufikisha hapa tulipo. Naamini wanajua namna watakavyotutoa humu. Na kwa kuwa wameanza kutafunana na kuadhiriana hadharani; matumaini yapo. Tuwape muda. Nakumbuka hata Wamarekani walipoona George Bush amelikoroga kule IRAQ, walimpa miaka mingine minne ili arekebishe mambo wakamwacha John Kerry ambaye alikuwa amejenga hoja na sababu nzuri sana za kumng'oa
   
 9. Makindi N

  Makindi N JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2009
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 1,068
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kwanza kabisa, japo ni swali, binafsi naona it's failing question that will lead to failing statements and arguments.

  Mkubwa kuanza upya kuna maana kubwa sana kwa Kikwete and his entourage. Kwa muda alivyopata uraisi, na kuanza serikali yake, pale ALIANZA UPYA. Lakini yote tuyaonayo mengi aliyakuta na mengi yametokea ktk uongozi wake. Amefanya mengi lakini yale ambayo ndo topical "roho ya watanzania" bado anasuasua (namaanisha yalio-cost Tanzania haswa).

  Kuanza upya kwa maana ya kisiasa na nyanja zingine ya kutuletea maendeleo, kwa watu hao hao akina Kikwete haiwezekani. Ni pale tu watakapoamua kubadilika wao au atakaeingia atakapobadilika na kuanza afresh.

  I always say, development it's a choice that none of our leaders have, ndo maana tunajionea yote haya...... Its gonna be a damn new wine in the damn old bottle. Watu wale wale, fikra zile zile, utendaji ule ule, siasa zile zile... Sana sana tutazidi tiana hasara tu kwa kuwaachia hivyo hivyo!

  Tukiwa tunanyambua tuanze upya, tujiulize kwa nini tuanze upya? Naamini kuna kitu kinachoweza kutufanya tuanze upya,je tunafikiri baada ya kuanza upya tutaweza kukidhibiti na kwanini tushindwe sasa wakati huo uwezo unao kama utakavyoweza kuanza upya?
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  The damage had happen already, and the cause still exsist. What we do then?

  a. We dig to remove the roots and throw into fire (Law cleansing procedures)
  b. We restore the stolen wheat ghalani (Filisi wote)
  c. We baptize again all who sin against society after make them to repent.
  d. We starts over.
  e. Everybody is happy.

  No way to forget because waliokufa kwa uzembe wa mafisadi are watching. Let them sleep in peace after we done something pleasing.
   
 11. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu Mwanakijiji, natanguliza heshima nyingi. Mkuu matatizo yote ya kiutendaji tuliyonayo nchini yanatokana na mfumo usiokidhi mahitaji. Mfumo uliopo ambao kimsingi umejengwa na Katiba yetu, hauwezi kutuletea tija kubwa tunayoitarajia na ambayo wanasiasa wetu wamekuwa wakiizungumzia kwenye majukwaa ya siasa. Mfumo huu ni mgumu kuwa na mafanikio hata tukianza upya kila harakati kama ulivyoainisha.

  Mimi naamini kuwa hatukuanza vibaya, ila tunaendelea vibaya. Ni sawa kabisa na mkimbiaji uliemtolea mfano, ambae ameanza mbio zake vizuri, halafu akasahau kuwa yuko mashindanoni na kuanza kuokoja maembe njiani au akaanza kuongea na simu huku akipoteza mwelekeo na muda bila kujali. Maana yake ni kuwa, sio tu kwamba mbio tunazokwenda nazo si za kimashindano, bali pia zinaelekea nje kabisa ya route inayotakiwa.

  Nikirudi kwenye sababu za kimfumo zinazotufanya tushindwe kuendelea. Ukweli unabaki kuwa uzalendo kwa wananchi wote na hata viongozi wetu haupo tena, Ufisadi umeota mizizi, utendaji umeshuka sana (hasa kutokana na uoga wa kuthubutu walionao watendaji wa umma), na zaidi ushirikishwaji wa wananchi katika kujiletea maendeleo uko chini sana. Yote haya, ni matunda ya kuchezea au kuharibu misingi yetu ya uchumi ama kuweka misingi isiyoendana na hali halisi ya ukuaji wa Taifa huru.

  Nahofia kuwa, kusamehe Mafisadi na hata watu wote waliopo magerezani hakutaweza kutatua tatizo lililopo. Kinachotakiwa sasa, ni kuunda Katiba mpya, yenye ushiriki wa wananchi wote na itakayojadiliwa na kupitishwa na Bunge (kama taratibu zilivyo). Katiba hii inatakiwa itoe nguvu zaidi kwa wananchi na sio kwa viongozi wachache kama ilivyo sasa. Iweke misingi imara ya kidemokrasia na utawala wa pamoja.

  Katiba iweke bayana masuala ya uongozi ambapo kiongozi wa Taifa (Rais) asiwe ni mwenyekiti wa chama chochote cha siasa. Sababu ya hili ni kuwa, chama kilichomteua kuwa mgombea wake wa uRais kinatakiwa kiwe na uwezo wa kumhoji anapokwenda kinyume na ahadi za chama chake, na pia kiweze kumbadili kikiona hafai kugombea tena katika kipindi kinachofuata. Hali ilivyo sasa (inawezekana ni ya kimazoea zaidi, lakini haiko kisheria), inamfanya Rais awe na nguvu sana ndani ya chama chake, Taifa na taasisi zote nchini. Hii inayoweza kumfanya asiwe makini kiutendaji. Inawezekana hatujapata Rais alietumia vibaya madaraka yake kiasi hicho, lakini atakapotokea, itakuwa shida kumdhibiti.

  Pili, ni vyema Mawaziri wote wanapoteuliwa na Rais, wajadiliwe na Bunge kuona kama wanakidhi mahitaji ya utekelezaji/utendaji unaokusudiwa katika agenda za nchi na walio na uwezo na maadili ya kuweza kulipeleka Taifa mbele. Imeshadhihirika sasa kuwa Mawaziri (ambao ni viongozi muhimu sana kitaifa) wamekuwa wakifanya mambo yasiyotegemewa na wenye maadili tata.

  Azimio la Zanzibar (ambalo haliko kimaandishi hadi leo) linatakiwa lirekebishwe na kuweka misingi ya utawala bora. Mabadiliko yake yahusishe maazimio yaliyotangulia (hasa Azimio la Arusha) kwa kuyafanyia mabadiliko yaliyo ya lazima tu, badala ya kuyafuta maazimio hayo, ambayo yaliweka misingi mizuri ya kiutawala.
   
 12. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  1. Nafikiri itakuwa sio jambo jema kuwaacha mafisadi waendelee kupeta kama hakuna
  kitu kibaya walichofanya. Ni vema sheria ikaamua hatima yao.Hili litakomesha tabia ya
  wasomi wa nchi hii, wenye madaraka kuendelea kufanya madudu kwa visingizio
  kuwa hawajui wanachofanya
  2. Nahisi kuna dalili za mabadiliko au baadhi ya watu wameonyesha nia ya kutaka
  kubadilika. Kwa mfano majibu mengi ya waziri mkuu bungeni hakuyafanya kwa
  mazoea kama ilivyokuwa awali. Ilivyokuwa zamani, watawala walipenda tuamini
  pengine hata kwa dharau na jazba kuwa chochote serikali ilichofanya kilikuwa halali
  hata kama kilikuwa kinanufaisha watu wachache tu walio serikani na kuwaacha
  wananchi wengi pembeni.Huu ulikuwa uongo mkubwa kwenye nafsi za watawala mana
  ilikuwa ni suala la muda tu kabla ya wananchi kuanza kuhoji
  3. Dalili nyingine ya mambo kuanza kubadilika ni hili la vigogo wengi wa zamani ambao
  kuanza kuloloma hadharani kuwa mambo hayaendi sawa. Wameshaanza kuona hakuna
  tena kulindana walikokuzoe...wanatoka nje kutafuta sympath ya wananchi wakati wao
  wamechangia tena kwa makusudi kulidumaza Taifa letu.
  4. Naafiki wazo lako la kusuka system zetu upya. Tuache kucheza na vitengo nyeti kwa
  kuajiri watu wasiokidhi mahitaji ya kazi hizo just because ni watoto zetu au watoto wa
  wandugu. Wanageuza vitengo hivyo nyeti kuwa vijiwe vya madeal na kufanya mambo
  yasiyo ya kizalendo. kama tunataka kufika, kazi nyeti lazima wapewe watu baada ya
  kufanyika proper due diligence kuona kuwa wataweza kuzimudu kazi hizo.
   
 13. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hata ukiniweka kitanzi bado nitakwambia hawajui! Kama wangejua jinsi ya kututoa wasingetuacha tukaendelea kuzama kwenye tope tena linalonuka kila aina ya uozo.

  Hapo naona kama unachanganya mambo. Huwezi kulinganisha system ya kikatiba ya Marekani na sisi huku uswahilini. Kwetu hata kichaa akipitishwa na CCM na akawa na pesa za kununua kura anaweza kutinga Ikulu pale Magongoni. Sina hakika kama hili linaweza kutokea USA.
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Drastic measures are needed.Lakini nani achukue? Mtu mmoja mmoja akichukua hatua kunusuru umma kuna hatari zake ( rejea DC aliyeona njia pekee ku deal na walimu walevi/wavivu ni viboko aliishia kuonekana ana ugonjwa wa akili na akaishia kufukuzwa kazi).Tukisema tusubiri system ichukue hatua kunusuru nchi..tutasubiri sana and it will never happen maana there is too much at stake na kuna interests tofautitofauti katika kila eneo lenye ubovu.
  lets wait and see........
   
 15. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mkjj, tumejichanganya sisi wenyewe kwenye hizi mbio. Mbio ni marathon za mita 10000, lakini baadhi yetu tulio anza nao ghafla wamebadilika na kuanza kukimbia mbio za mita 1000, na wengine mita 100. Na wamefanya hivi bila kutaarifu wenzao tulioanza nao. Na kibaya ni kwamba wamekuwa ma-Dwayne Chambers na ma-Marion Jones katika hizi mbio. Na kibaya zaidi ni kwamba hawa ma-dwayne na marion wetu hawakukubali makosa wala kukosolewa kuwa mbio wakimbiazo na mbinu watumiazo si njema kwa wengi wetu. Haziko kwenye makubaliano.

  Zaidi cha kusikitisha ni kwamba, katika mbio hizi ambazo wote tulikubaliana kukimbia kwa mwendo sawa; wengine wameamua kukata tamaa na kubakia kuwa washangiliaji. Na wale ambao tungewaamini kuwa wasimamizi wa mbio hizi, wamebadilika na kuwa watumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu na wasambazaji wa madawa hayo kwa baadhi ya wakimbiaji.

  Kwa kuwa mbio za mita 10000 zinaonekana ndefu mno, na zile za 1000 hazina tija pia, halafu zile za 100 ni fupi mno; basi, tukubaliane tu kuwa tunakimbia za mita 200 au 400 na kila mmoja wetu awe Michael Jonnson au Cathy Freeman. Maana kuanza moja/upya haiwezekani, na kusema liwe na liwe na kuacha mbio ziendelee kama zilivyo sasa, wengi watakuwa wameachwa nyuma, na wengine watakata utepe wa mwisho kabla hata wenzao hawajafikisha robo ya safari.

  Suluhisho ni kuratibu mbio hizi mapema iwezekanavyo. Mapendekezo mengi yapo na tumeshayaandika. Mojawapo likiwa hili HAPA.

  SteveD.
   
 16. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Sure Steve, we need to make a U-turn and do something.

  But  • This is brilliant

   I will need some time to make my mind before I can re-introduce it as a full package. But can't hesitate to pick some critical and implementable parts of it, such as ethics codes!

   May be the CCM's Ujamaa which remains on papers. Otherwise the type of Ujamaa we sang doesn't seem to work and I would not even dream of it. May be talking of a system which cares for the majority and let's the few enjoy their talents. But the type Ujamaa in which the Government could send you to jail for drinking 4 beers (after working hard the whole week) has no place in this 21st century.
   
 17. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Tukiamua kuanza upya, lazima tujue wapi tumekosea! kama tunajua wapi tumekosea , lazima tujue jinsi ya kurekebisha hayo makosa. Sasa kama tunajua jinsi ya kurekebisha hayo makosa, Je hatuwezi kufanya hivyo bila kuanza upya? Kwani naamini kuwa sio yote yaliyofanywa ni mabaya; basi hayo mazuri machache tunaweza kuendelea nayo wakati tunarekebisha kasoro tulizozigundua!! Naomba kuwasilisha.
   
 18. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  ili ujue kama ulianza vibaya, ni lazima ujue kama umeanza vibaya, na ukubali kwamba ulianza vibaya. Sasa waliotufikisha hapa tulipo kama wapo tayari, kukubali kwamba tulianza vibaya, na kwamba ni makosa yao kwamba tupo hapatulipo, na je wapo tayari kujirekebisha ? - i.e vijisenti vyote virudi, majumba yetu yote waliyopeana yarudi, mirahaba ya dhahabu irekebishwe retro-actively. - Only then will i think about it.Otherwise we will all be enablers in this.
   
 19. F

  Felister JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2009
  Joined: Aug 5, 2008
  Messages: 377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Before treating the disease you should first know the causative agents and see if there are curative and preventive measures so that when you treat the patient you can if possible wipe the agents if not possible advice on preventive measures otherwise you might be treating the signs and the patient will always be in the risk of attacks and ultimately death can occur.

  The way I percieve our major problem is not who is in power and who is not as all of us every one depending on degrees are responsible for the out come of the situation we are now in; if there is any genius in this situation then would have come up with a viable solution be it in leadership or implementation longtime a go and we would have been just enjoying. The moment we ralize this we would take time to develop our own development models (not kutegemea wazungu wao wako busy na ya kwao) into changing the situation and nobody would think or do for us; its our own responsibility yes each one of us. Now this is my nut shel contribution am still in the homework of trying to come up with Tanzania's tailored models. i never believe in failing if I have not tried for whoever want to help here is the skeleton.

  perceived problems

  Life uncertainty- The former models contributed into this, The first leaders devoted their time and energy into serving the Tanzanians unfortunately they forgot what is called life after office and the community in return rewarded to them bad life after the office; the followed leaders having learnt from the mistakes made; tried to remove the uncertainty which was always arround to do away with it they decided to tranfer to those who are not well informed not knowing that society live longer than individuals and thats where the problem started kwahiyo ikaanza ni huyu mimi nikiingia nitafanya hiki na kile ikawa sasa strugle for power so as to remove individual's life uncertainty every place every where na tatizo linaanza kuonekana maana information flow imekuwa kubwa kwahiyo transfer of uncertainty is no longer easy as the the marginal increse of informed is growing.

  Another problem decrease in social capital i.e trust etc but this is easly restored if there is good economy and efficient legal system.

  Yes tuanze upya swali unaweza kubadili your past, if one is able i would want to change mine as I think if I would have thought rightly Tanzania would never have been like it is now. Realising this I dont blame anybody neither myself but to try to find solutions. My dream is to revive Nyerere's Ideology Siasa ni Kilimo this time with better developed models. Nikiwa tayari will come up with some theories to work on and implementation strategies and I would very much appreciate the contribution from this forum let me first do my home work.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,619
  Likes Received: 2,004
  Trophy Points: 280
  Mzee mwanakijiji kwanza umesema mkiamua...Mkiamuwa wewe na nani? Kwani nani huko serikalini kasema tuko pabaya?
  Kama unazungumzia wananchi tukiamua then uwe specific,lakini hata hivyo kama uli refer wananchi,then rejea second highlits...Kama ukiwaachia uwezo wa kukushughulikia kwa kuwaachia rasilimali za taifa basi ni lazima uhakikishe kuwa wamekubali kuna blunder na kwamba kuna need of change in direction.
  Kama ulimaanisha serikali ya JK...Then usisahahu uongozi bora unapimwa kwa uwezo wa kuomba omba misaada na kuna imani kuwa misaada inafanya kazi zaidi kuliko pesa zetu sisi wenyewe, sasa si ni sawa na kuwapa ushindi mafisadi? Na si ni the same na wewe unavyotaka hapo.
  Kwanza wao mafisadi ndio wakubali,halafu wasikilize,then we will see....Otherwise itakuwa ni ku jeopordize vita ya kuung'olea mbali ufisadi.
  NB;
  Naomba ufafanue zaidi kwenye kuanza upya,je mafisadi wameshirikishwa ama ni maoni yako tu?
   
Loading...