Tuambie kitu ulichofanyiwa utotoni kikakuletea madhara hadi leo

Doooh Pole sana,Stori yako Inaumiza sana kwa kweli, Ishu yako kisaikolojia ni ngumu sana kufutika,Ila uombe Mungu kama Una Mume awe ni mume anayejali au kama ni mpenzi awe yule aliyelelewa kwa upendo na atakayeweza kukufundisha upendo na kukusahaulisha yote.
Ni kweli mkuu...!! Nina mume na watoto wawili. Ananipenda sana hata mungu anajua ila kuna kitu sina..sina kabisa yaaani ila sijui ni mini lakini kihisia sijakamilika.
 
baba yangu baada ya ripoti ya kushika mkia alinifuatilia shuleni kibabe na kunipiga ngumi na mitama na kunifunga kamba hadi home,nililala na kamba had I asubuhi ,basi nikikumbuka hii ishu huwa nacheka,lkn namshukuru kwani ilinifanya kuwa mgumu sana ktk life langu.
 
Nikiwa kidato cha kwanza 1974 muhula wa pili nilichelewa kutoka nyumbani mwanza kwenda tanga nilichelewa connection ya train ruvu nikasubiri wiki iliyofuata nilipofika shuleni mwalimu wa zamu enzi hizo bila kujali hali ya nchi miundo mbinu ilivyo kuwa mbaya NA usafiri wa tanga dar treni ilikuwa NA conetion ya Mara moja kwa wiki alitaka anichape nikamugomea likizo iliyofuata aligomea tiketi zangu hadi anichape nilikaa shuleni wiki nzima wenzangu wameondoka hadi nikawa naombeleza vyakula NA alitimiza lengo lake alinipiga vibaya sana hadi nikapata homa maumivu ya fimbo niliuza tiketi za train sikuenda likizo nikafadhiliwa NA wasukuma wa tanga hiyo mwalimu hadi nakufa sitamusahau NA alinifanya niwachukie wahaya kwa sababu naye ilikuwa muhaya mutashobya kama tuko hao namchukia mpaka Leo.
 
Nililelewa na Mama wa kambo alikuwa mkali sana kitu kidogo tu napigwa,nikiagizwa kitu nimpelekee kama yupo jikoni basi nikimpa tu kama sijarudi nakofi nashukuru Mungu,kutokana na Woga nikawa kila akinituma kitu nimpelekee mikono ikawa inatetemeka haijiamini,kwahiyo mpaka Leo Nina tatizo hilo mikono inatetemeka muda mwingi japokuwa najitahidi kujicontrol watu wasinotice ,pia aliwahi kuniunguza na moto kwenye vidole vya mikono na miguu kwa kosa la kutokufunga bomba la chooni,kwasasa ni MTU mzima Nina kazi yangu nzuri sabab nilijitahidi kusoma ili nifaulu niende shule za mbali niepuke mateso yake,matokeo yake yeye ndo amekuwa tegemezi kwangu,kwani hakubarikiwa kupata Mtoto yoyote na najitahidi kumsaidia kadri ninavyoweza sababu nilikwishaamua kumsamehe!!
Pole sana mkuu na hongera kwa kusamehe!
Nina amini kila unapomsaidia huumia ndani kwa ndani.
 
Kuanza kuvuta bange. Najitahidi kuacha lakini baada ya mda nashikwa kiu na kulazimika kuitafuta tena. Nimepata majanga mengi sana sababu ya bange ila naamini ipo siku nitafanikiwa kuacha.
Hahahaa ganja mbaya sana Mzee baba
 
Moyo ukifunguka. Tatizo moyo
Niliwahi jaribu kujiforce nikawa in relationship, it was worse, mapenzi sina, yaani he was there kama jina tu, yaan kujali hakuna, he was just like a normal person, uhusiano ulivunjika automatic coz hata kuwasiliana nae nilkua najilazimisha ikafikia muda nikaacha kabisa mpaka leo, uhusiano hakuna tena
ngoja ukutane na mtu atabadili maisha yako na vile unafikiria kuhusu mapenzi, time will tell. hujamjua bado, mapenzi na kama uchawi. ukinasa umenasa. am speaking from experience, enjoy life, your time will com. uta fall in love in un expected ways.
 
Poleni kwa yote mliopitia. Damu ya Yesu ikawaponye majeraha hayo mioyoni mwenu. Hakika huu uzi umenifundisha vitu vingi sanaaa haswaa malezi kwa watoto wangu.
 
Nililelewa na Mama wa kambo alikuwa mkali sana kitu kidogo tu napigwa,nikiagizwa kitu nimpelekee kama yupo jikoni basi nikimpa tu kama sijarudi nakofi nashukuru Mungu,kutokana na Woga nikawa kila akinituma kitu nimpelekee mikono ikawa inatetemeka haijiamini,kwahiyo mpaka Leo Nina tatizo hilo mikono inatetemeka muda mwingi japokuwa najitahidi kujicontrol watu wasinotice ,pia aliwahi kuniunguza na moto kwenye vidole vya mikono na miguu kwa kosa la kutokufunga bomba la chooni,kwasasa ni MTU mzima Nina kazi yangu nzuri sabab nilijitahidi kusoma ili nifaulu niende shule za mbali niepuke mateso yake,matokeo yake yeye ndo amekuwa tegemezi kwangu,kwani hakubarikiwa kupata Mtoto yoyote na najitahidi kumsaidia kadri ninavyoweza sababu nilikwishaamua kumsamehe!!
🤩🤩🤩🤩🤩
 
Cjui ila najitahidi kuonyesha upendo kwa watu mbali mbali lakini wapi. Sasa cjui namimi kwanini niko hivyo
Pole,tuko wengi!story yako kama mimi tu tena mimi mshua akawa adi ananisimanga pamoja na kunitelekeza!kinachonisaidia ni preachings za wahubiri kama joyce meyer,ukimsikiliza taratibu utaanza kuishinda hiyo hali vinginevyo unaweza kujeruhi mtu kirahisi sana na ukaona poa tu!
 
Very painful... My uncle aliwahi nishika matiti, nikiwa form 3... Na kunishika makalio huku akinipiga na mkanda wa suruali.. Nikawa namuona jinsi anavyosimamisha dudu lake anavyonipiga et nakataa shule ndio maana nimenenepa!!

Hopeless created people..... Maisha jamani.. Very painful

Niliwahi kufungiwa nje usiku had asubuhi!! Muda mwingi sijikubali.. Nikiona MTU ananipetipeti namshangaa sana!!!
Nafsi yangu INA kiu ya upendo!!
Amekutengenezea spirit of rejection,unaweza kuishinda dear kupitia positive thinking,mimi ni shuhuda wa hilo
 
Malezi ni ya msingi sana
Ndio mana kwenye jamii zetu leo unakuta kuna viongozi wako very aggresive,kuna wababa wakorofi mno kwenye ndoa zao ukisema uingie ndani utakuta wengi wao wana vidonda vya utotoni ambavyo vimewapa majeraha ya kudumu!
Siku zote majeraha huwa yanaongea unless mtu apone,majeraha huamua mtu aseme nini au afanye nini kwa nani
Wazazi watarajiwa na wazazi wa sasa muwe makini sana kwenye malezi ya watoto ili kuepusha uzao wa watoto wenye majeraha na mwishoe kuathiri hatma za maisha yao!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom