Tuambie kitu ulichofanyiwa utotoni kikakuletea madhara hadi leo

Watu mmeumizwa jamani poleni sana, Yeye aliye mponyaji awaponye majeraha yenu, Amen.

Espy na HS nawaelewa sana maana nilikuwa mwalimu kwa miaka kama 4 hivi kwenye shule zetu hizi za kata , ukiishi na wanafunzi utaelewa ni kwa jinsi gani watoto wanapitia changamoto kwenye makuzi yao.

Ni wajibu wetu wazazi wa sasa kulibadilisha hili, tuwe responsible ingali tuna uhai bado.
 
Ngoja kwanza nilie kabla sijaanza kuandika

Nakumbuka wakati nipo mdogo nilikuwa mtu wa kujichanganya sana na wenzangu mtaani kwetu yaani naweza kuondoka asubuhi nikarudi usiku muda wote huo napiga stori na wezangu

Baadae wazazi wangu wakaanza kunikataza kushinda na wenzangu kwa nia njema lakini kwa sababu wengi walikuwa hawasomi na walionekana hawana tabia nzuri

Baada ya hapo maisha yangu yakabadilika kabisa nikawa mtu wa kushinda tuu nyumbani nimesoma kuanzia la kwanza mpaka form six sijui rafiki ni mtu gani advance nimesoma bweni niliishi maisha ya majonzi mno,upweke,huzuni,nililia kila siku nilitamani mno kuwa kama wezangu ambao walikuwa wanahave fun na marafiki zao kwangu nilishwindwa

Chuo niliaacha kutokana nilishindwa kujichanganya na wezangu kwenye group discussion,kushindwa kupata hata rafiki mmoja wa kumpigia simu kujua habari za chuo huwa naumia sana napoona miss chaga@heaven sent na wengineo wanapokumbukia maisha yao ya chuo

Nawashukuru sana marafiki zangu wa JAMII FORUM kwa kunipenda
 
Waswahili wanasema chagua maneno ya kusema unapokuwa na hasira,pia usitoe ahadi pindi ukiwa na furaha sana.

Kipindi nipo mdogo,kulikuwa na mama yetu mdogo aliyekuwa anatutembelea mara kwa mara, na pia alikuwa na kawaida ya akija Dar basi alikuwa anafikia kwetu. Akiwepo au ikitokea amefika home alikuwa na kawaida ya kuleta zawadi ndogo ndogo kwa watoto pale home. Nina kaka yangu mmoja huyo ndio alikuwa her favorite,yani hawezi kuleta kitu alafu akamsahau. Ila mimi kusahaulika au kutoa zawadi kwa wengine alafu zikaisha kabla mimi sijapata hiyo ilikuwa kawaida sana. Nakumbuka pia kuna siku tukiwa home alinituma nikamletee pochi yake,nilivyoileta akatoa zawadi na kumpa broh.

Pamoja na umri wangu mdogo enzi zile,lakini sikuwahi kuumiana hivyo vitu au kumuonea wivu broh na mdogo wangu. Nilimchukulia ni mama yangu mdogo na sikuwahi kumkasirikia hata kwa jambo lolote.

Sasa kuna siku tulikuwa tumekaa sebleni tunapiga story za hapa na pale walay muda uende. Ilikuwa usiku,na home hakukuwa na umeme bado (kipindi hicho kuwekewa umeme ni process as if unaenda kukopa). Kikawaida mimi ni talkative and very charming,smilling all the time ( ingawa maisha ya ukubwani yamenipunguzia hivi vitu).

Katikati ya maongezi,sikumbuki mada ilikuwa nini (sababu ya umri niliokuwa nao that time) ila mama mdogo ndio alikuwa anaongea,sasa mimi bila kujua plus akili za utoto nikamkatisha yale maongezi,nikataka niongee kitu. Dah dah dah. Nayakumbuka hadi leo maneno yake. "KELELE WEWE,NDIO MAANA SIKUPENDI"

Baada ya ile kauli,ulipita ukimya wa ghafla. Maana sebleni alikuwepo Baba,Mama,Sister,ma brother wawili,mdogo wangu na yeye mama mdogo.

Ile kauli ikanikumbusha kuna siku nilienda kumpokea Ubungo,alikodi tax tukapakia mizigo. Alafu yeye akaniacha mimi na mdogo wangu tukiwa nje ya tax pale ubungo tubaki na dreva hadi arudi (sikumbuki alienda wapi but alitumia kama dakika 10). Huku nyuma kwa vile tulikuwa karibu na sheli,yule dreva tax akaniambia anaingiza gari sheli kujaza mafuta.

Mamdogo kurudi tax haipo,na mwambia jamaa kaenda kuongeza mafuta. Wakuu kabla hata sijamaliza kumwambia nilipokea matusi makubwa makubwa ya nguoni,nayakumbuka hadi leo. Nilimwambia tu kwa upole,tax ile pale ( maana sheli ilikuwa pale pale),dreva nae akawa amerudi.

Huwezi pendwa na kila mtu,ila kuchukiwa ni kitu kingine wakuu. Huwa najaribu kufanya vitu vitakavyo niondolea hasira juu yake na kunifanya nimpende. Nahisi nafanikiwa katika ili,maana moyo sio mgumu katika kumsaidia katika jambo lolote.

Funny enough kuna siku (enzi hizi za ukubwani) aliwahi kuniambia "Nawashangaa eti wanaosema sikupendi wakati mimi na wewe tunaiva vizuri tu"

Ashasahau tayari.

God is good All the time. Lets overcome hatred by love.
 
Jamani we love you so much
 
Watu mmeumizwa jamani poleni sana, Yeye aliye mponyaji awaponye majeraha yenu, Amen.

Espy na HS nawaelewa sana maana nilikuwa mwalimu kwa miaka kama 4 hivi kwenye shule zetu hizi za kata , ukiishi na wanafunzi utaelewa ni kwa jinsi gani watoto wanapitia changamoto kwenye makuzi yao.

Ni wajibu wetu wazazi wa sasa kulibadilisha hili, tuwe responsible ingali tuna uhai bado.
Kwa kweli tumuombe sana Mungu juu ya malezi ya hawa watoto wetu
 
Khaaa kumbe kuna muda tunalaumu tu fulani kwa kupenda majimama, bila kujua kuwa mtu ameathiriwa kisaikolojia. Jamani mimama mingine, mbona kutulaanishia watoto wetu? Mungu tulindie hawa watoto
Mkuu comment yako imenifanya nicheke . Ila point yako nimeielewa,wengine zinakuwa psychological effects.
 
Kweli bana, Unamkuta kijana mdogo yeye na majimama tu. Tunafikiri kuwa ni umario tu kumbe hamna maskini
 
Mi siku moja nilikua karibu na chumba chawazazi wangu nikasikia wana semezan tukiachana utamchukua nani,..mzee akasema mkubwa wangu,mama akasema wadogo zangu wawili ila hakuna alienitaja,nikasubiri labda watanitaja,hakuna nilienda katikati ya ukuta za chumbani nililia sana nilidhan wazazi wangu hawanitaki,..kwa nzia apo nilikua nasoma tu niende nisome shule za boarding na wakati wa likizo sirudi,..mpaka leo hii UA sikai nyumban,..nikirudi home nakaa sio zaidi ya miezi miwil natokomea,..
Pole sana mkuu. Vipi walitengana kweli au ndio walikuwa wanapiga tu story?
 
Motorola usiku bila uoga nilisoma semeniary ipo mbali saana na mjini hivyo ilikua lazima kutoroka usiku unapita katikati ya pori nene

Hali imenipa ujasiri safari zangu zote Nafanya usiku mfano nikitaka kutoka dar kwenda dodoma nawasha gari saa nne usiku ndio safari inaanza
 
Walipotengana wazazi when I was 10 hapo ndo THINGS HAS FALLEN APART.
Many impacts has happened,nyingi ni negative.
 
Waswahili wanasema chagua maneno ya kusema unapokuwa na hasira,pia usitoe ahadi pindi ukiwa na furaha sana.

Kipindi nipo mdogo,kulikuwa na mama yetu mdogo aliyekuwa anatutembelea mara kwa mara, na pia alikuwa na kawaida ya akija Dar basi alikuwa anafikia kwetu. Akiwepo au ikitokea amefika home alikuwa na kawaida ya kuleta zawadi ndogo ndogo kwa watoto pale home. Nina kaka yangu mmoja huyo ndio alikuwa her favorite,yani hawezi kuleta kitu alafu akamsahau. Ila mimi kusahaulika au kutoa zawadi kwa wengine alafu zikaisha kabla mimi sijapata hiyo ilikuwa kawaida sana. Nakumbuka pia kuna siku tukiwa home alinituma nikamletee pochi yake,nilivyoileta akatoa zawadi na kumpa broh.

Pamoja na umri wangu mdogo enzi zile,lakini sikuwahi kuumiana hivyo vitu au kumuonea wivu broh na mdogo wangu. Nilimchukulia ni mama yangu mdogo na sikuwahi kumkasirikia hata kwa jambo lolote.

Sasa kuna siku tulikuwa tumekaa sebleni tunapiga story za hapa na pale walay muda uende. Ilikuwa usiku,na home hakukuwa na umeme bado (kipindi hicho kuwekewa umeme ni process as if unaenda kukopa). Kikawaida mimi ni talkative and very charming,smilling all the time ( ingawa maisha ya ukubwani yamenipunguzia hivi vitu).

Katikati ya maongezi,sikumbuki mada ilikuwa nini (sababu ya umri niliokuwa nao that time) ila mama mdogo ndio alikuwa anaongea,sasa mimi bila kujua plus akili za utoto nikamkatisha yale maongezi,nikataka niongee kitu. Dah dah dah. Nayakumbuka hadi leo maneno yake. "KELELE WEWE,NDIO MAANA SIKUPENDI"

Baada ya ile kauli,ulipita ukimya wa ghafla. Maana sebleni alikuwepo Baba,Mama,Sister,ma brother wawili,mdogo wangu na yeye mama mdogo.

Ile kauli ikanikumbusha kuna siku nilienda kumpokea Ubungo,alikodi tax tukapakia mizigo. Alafu yeye akaniacha mimi na mdogo wangu tukiwa nje ya tax pale ubungo tubaki na dreva hadi arudi (sikumbuki alienda wapi but alitumia kama dakika 10). Huku nyuma kwa vile tulikuwa karibu na sheli,yule dreva tax akaniambia anaingiza gari sheli kujaza mafuta.

Mamdogo kurudi tax haipo,na mwambia jamaa kaenda kuongeza mafuta. Wakuu kabla hata sijamaliza kumwambia nilipokea matusi makubwa makubwa ya nguoni,nayakumbuka hadi leo. Nilimwambia tu kwa upole,tax ile pale ( maana sheli ilikuwa pale pale),dreva nae akawa amerudi.

Huwezi pendwa na kila mtu,ila kuchukiwa ni kitu kingine wakuu. Huwa najaribu kufanya vitu vitakavyo niondolea hasira juu yake na kunifanya nimpende. Nahisi nafanikiwa katika ili,maana moyo sio mgumu katika kumsaidia katika jambo lolote.

Funny enough kuna siku (enzi hizi za ukubwani) aliwahi kuniambia "Nawashangaa eti wanaosema sikupendi wakati mimi na wewe tunaiva vizuri tu"

Ashasahau tayari.

God is good All the time. Lets overcome hatred by love.
Let's overcome hatred by love, always love wins!
 
Huu uzi umenifanya niotokwe machozi sana nikikumbuka niliyopitia nikiwa mdogo. Kwa kweli poleni sana kwa mliyopitia lakini tujue kwmba Mungu yu pamoja nasi. Huwa kila nikukumbuka huu wimbo unanipa faraja sana na kumtumaini Mungu kila kukicha.

anakuwa sehemu Fulani..... Pale alipokuwa siku ile mwanae alipodhalilishwa, akaa kimya.... Huwa hajifichi bali huwa pamoja na wale wateswao.....

I love the song, indeed He is still at the same place.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom