Tuambie interview mbaya uliyowahi kuifanya

Tuambie interview mbaya uliyowahi kuifanya

Ulivokuwa unawajibu walikuwa hawacheki
Nilikuwa nina idea ila nilikutana na kitu sikukitegenea nikapanic,nilipoona hapa nitaumbuka nikawa nawaambia "have no idea".

Sema walikuwa serious sana, hawacheki wala hawanuni wapo katikati.
 
Usicheke mdada, subiri siku ukipigwa interview na hawa weupe ndio utajua tunachozungumza hapa
comedian tena wakati tunazungumza uhalisia wa yaliyotukuta.

Wewe maliza shule kwanza halafu uje ukutane na hizi saili ndio utajua huu ni ukweli
Nimecheka kama mazuri hivi[emoji1787].
Ila mkuu nje na mada, una kipaji cha kuchekesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka kama mazuri hivi[emoji1787].
Ila mkuu nje na mada, una kipaji cha kuchekesha.

Sent using Jamii Forums mobile app
sio kipaji ni uhalisia tu ambao uanchekesha...wale mainterviewer wenyewe walibaki kunicheka tu.

Na ilikuwa ni bonge la kazi, mtu ambaye aliajiriwa kwa leo anakula 13m ukiachana na malupulupu mengine
 
sio kipaji ni uhalisia tu ambao uanchekesha...wale mainterviewer wenyewe walibaki kunicheka tu.

Na ilikuwa ni bonge la kazi, mtu ambaye aliajiriwa kwa leo anakula 13m ukiachana na malupulupu mengine
Aisee[emoji23][emoji134]
Sema haikuwa rizki yako boss

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimecheka sana[emoji23][emoji23][emoji23]

Mimi bwana maishani nimefanya interview moja tu ikanipa pa kujishikiza
Kiufupi nilikwenda tu kujaribu kwa kulazimishwa na bi mkubwa baada ya kukaa sana mtaani sina mbele wala nyuma, na nilishakata tamaa maana kwa hali yangu ya kimaisha sikuwa sikuwa na refa wala hela ya kuhonga mtu(kwa dhana iliyokuwepo pengine bado ipo)

Picha linaanza nikakutana na idadi kubwa sana ya wasailiwa, na wengi walivyokua na confidence niliamini aidha wana sifa kunizidi au wana marefa

Siku ya kwanza tulikaguliwa vyeti tu na sifa mbalimbali wakachuja na kuita majina

Wakati jina langu linaitwa sikuwepo nilikua kuvuta sigara, nikashangaa narudi wenzangu hawapo nje kumbe wameitwa ndani kusomewa majina, naingia tu nasikia jina sielewi kinachoendelea jamaa alimaindi sana akanifokea kisha akaniambia nimepita mchujo nikashukuru

Siku iliyofuata ilikuwa oral, wakaanza kuitwa mmoja mmoja, kama kawaida watu wakitoka wanakuwa na confidence nikazidi kuwa mnyonge

Nilipoitwa nikaingia, nilikutana na watu wazito sana kwenye vyombo vya serikali sikutegemea, kilichonisaidia sikuwa na hofu sababu nilikua tayari kwa lolote nikiamini najaribu tu kuna watu wameshatengewa nafasi

Confidence hiyo ndio ikanisaidia, ikawa ni maswali bandika bandua sitetereki, mengi yalihusu current issues na huo ndio uwanja wangu haswa dah wakachoka, mwisho nikaambiwa hufai wakaangua kicheko wote na mimi nikacheka nao(confidence)0

Wakasema nenda, nafika mlangoni naambiwa rudi nikapigwa swali(kunivuruga tu) nikapangua kama nimekaa ukimya ukatawala
Nikaondoka zangu

Kiufupi ziliendelea interview kama tatu au nne baadae ila zote ni kama kule kwenye interview ya kwanza waliniandikia kimemo kwenda juu kwamba hiyo ni mashine msijisumbue na maswali maana ilikua nikiingia wananitazama, wanacheki vyeti wananiruhusu kutoka

Ndivyo nilivyopata kazi
 
Mimi sikuchemsha oral, nilichemsha practical. Miaka ile namaliza six Kama mwezi mshkaji wangu mmoja akaniambia Kuna kazi pahala huna hata haja yabkupeleka barua Wala CV. Akanielekeza nikaenda maeneo ya kijitonyama.

Kufika nikawakuta jamaa wapo smart wadada na wakaka wananyonga Tai. Nikasema yah hapa patanifaa. Nikajiyambulisha na kuwaeleza shida yangu. Wakaniambia nenda kwa HR chumba flani, nikamkuta mdada hr yupo na mkurugenzi wa kampuni. Wapo smart hatari...
Nimemaliza diploma 2015 nachek chek mishe nikakutana na tangazo la kaz kwa gazeti bhana kumbe na machalii zng wengne wameona post "sales & marketing officer"[emoji23] nikasema mimi IT hii kaz haiwez nishinda nikaenda bhana.

Nimefika naangalia maeneo yenyew ya florida pale nasema hii ofisi iko wap kumbe kuna kagorofa kuna kachumba kapo akatoka jamaa kavaa tai na moka hyo upande imelika akili ikanicheza, nikasema hii kaz ya ma-stage show nin..?[emoji34][emoji23] Muhun nkazama ndan.

Nikaambiwakaandae Cv na barua nikasema kaz ya aina gan hii maana kuna wengine wamevaa mashati ya Satini yanang'aa kisenge, muhun nikabonyea stationery chap Cv si iko kwa simu nikaprint chap...nikarud walivoona mpaka diploma nnayo wakafurahia sana kwamba bhana ww utapanda cheo baada ya muda.

Mi nkarud magetoni kula sana Valeur na Ganja nkasema muhun nimepata kazi kiujanja mi ndo chalii mjanja usiku nikazima kuja kushtuka huyo nikakoga chap kidala kwa fasi Florida pale pemben ya pin point.

"Karibu bwana Papaa007 uko tayar kwa kazi kumekucha..asubuh njema kabsa hii siku ya leo j5 embu njoo tuanze kuset mambo ya kazi aisee nimeingia room flan nkakutana na sabun, birika, thermos, vyombo ya home...Jicho likanitoka kwanza yes Muhun mla Ganja leo unauza vyombo njian[emoji23].

Nkajisemea mi kidume napambana nikakabizziwa jomba mmoja wa kirangi aisee anarusha ndula hatar tembea mpaka mitaa ya njiro,uswahilin, sombetini nkaona kwel nimepatikana tukafika mitaa ya ngalimited relin tukaingia nyumban lwa mtu flan yule mRangi akadondosha saani chini "oohh mamq sahan haivunjiki nunua bei ni 5000 tu sahan utatumia mpaka wajukuu"

yule mama alisimama akasema mnaingia nyumba za watu kuna wagonjwa mnarusha saana chin zinalia kama bomu akaingia ndan tukajua pesa alitoka na maji ya moto fasta nikawah kusepa Mrangi akaipata ya mgongo kuanzia pale kazi za kijinga jinga hapana aisee hata kama ni kuhustle.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipiga interview moja vizuri na nikaona jinsi jamaa wanavyokubali presentation yangu, issue ilikuwa baada ya kumaliza interview. Kwa kihoro nilichokibana wakati wote wa interview badala ya kupita kwenye mlango nikaenda kupita kwenye vioo vilivyokuwa vimezunguka hiyo ofisi (meeting room imezungukwa vioo) nikagonga kwa nguvu mpaka nikadondoka.

Kwa vicheko cha watu sita nilivyosikia nyuma,pole niliyopewa na wadada wawili miongoni mwa wale wasaili na aibu niliyopata,nikajua hakuna kazi.
 
Nilipiga interview moja vizuri na nikaona jinsi jamaa wanavyokubali presentation yangu, issue ilikuwa baada ya kumaliza interview. Kwa kihoro nilichokibana wakati wote wa interview badala ya kupita kwenye mlango nikaenda kupita kwenye vioo vilivyokuwa vimezunguka hiyo ofisi (meeting room imezungukwa vioo) nikagonga kwa nguvu mpaka nikadondoka.

Kwa vicheko cha watu sita nilivyosikia nyuma,pole niliyopewa na wadada wawili miongoni mwa wale wasaili na aibu niliyopata,nikajua hakuna kazi.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1430]
 
Niliifanya TAA miaka hiyo walikuwa wanatafuta mashallah mwongoza ndege
 
Back
Top Bottom