Tuambie interview mbaya uliyowahi kuifanya

Tuambie interview mbaya uliyowahi kuifanya

Wanalafudhi ngumu sana inahitaji umakini sana kuelewa wanazungumzia nini na wao wenyewe wapunguze speed ya uongeaji.....

Ila kama wapo wazungu tu njia ambayo niliyotumia mara 3 kupata ajira ni licha ya kuwa na quality nzuri ila pia kutia huruma, yani nagusa quality zangu na najivisha umasikini ambao hauelezeki....
Hivi wanaangaliaga hii?

Wale jamaa wanaongea utafikiri wote tumezaliwa ulaya bhana, mimi sikuwaelewa na wao nadhani hawakunielewa
 
Yangu nilifanya na watu wanaitwa Wezesha wazawa microfinance, Hawa jamaa walipigia simu kazi ambayo nishaomba miezi nane ishapita,,, Wakasema Njoo kwa ajiri ya interview ,nafika pale ofisin pao nawaambia niliitwa kwa ajili ya interview wanabaki wananishangaa tuu, Kumbe aliyebipigia simu hata hakutoa taarifa kwa wenzake...
Dahh😂😂😂😂
 
Miaka kama 7 iliyopita niliitwa kwenye usaili kwenye International Organization moja yenye ofisi hapa nchini, hawa wako chini ya UN..Tulikuwa watatu kwenye nafasi yetu na walihitajika watu wawili tu. mimi nilikuwa wa mwisho kabisa kuingia kwenye chumba cha usaili lakini kila mtu aliekuwa anatoka kwenye room ya usaili alikuwa na sura ya upole sana. Ikafika zamu yangu maana ndiye nilikuwa wa mwisho...
 
Hivi wanaangaliaga hii?

Wale jamaa wanaongea utafikiri wote tumezaliwa ulaya bhana, mimi sikuwaelewa na wao nadhani hawakunielewa
Yes wanaangaliaga mkuu kama unasifa kadhaa na hiyo sifa ya ufukara ukaiongezea unakuwa considered....kwakweli mimi sehemu zote 3 ukiacha quality ambazo ji za kawaida hiyo ya ufukara imenibeba sana, just trigger hisia zao za huruma waone uhitaji wako.....
 
Yes wanaangaliaga mkuu kama unasifa kadhaa na hiyo sifa ya ufukara ukaiongezea unakuwa considered....kwakweli mimi sehemu zote 3 ukiacha quality ambazo ji za kawaida hiyo ya ufukara imenibeba sana, just trigger hisia zao za huruma waone uhitaji wako.....
Nilipotoka pale fasta nikaenda British council kuulizia ada ya English course na nikaanza darasa rasmi ule ujinga sikuutaka tena.
 
Bana we mi kama mbili tatu hivi nilimbwela yani na uhakika hadi nilivyogeuza shingo, walibaki kusema huyu dogo hayuko makini na maisha.

Nayo kumbuka vizuri ni International Organization for Migration (IOM) ni kama watu wa UN vile. Walikuwa wanataka mtu yani kamaliza tu school hana hata miezi 12 toka amalize shule. Wakanipata.

Picha linaanza sikuona mail yao iliyotaka kuconfirm kama ntakuepo kwenye interview au nko mbali wafanye utaratibu mwingine. Siku ya interview kama siku 7 baada ya email yao, wananipigia DanbyHR hujaconfirm kama utakuepo kwenye interview, vipi utakuja au tukufanyie phone/Skype interview? Nkafikiria nkaona sielewi nkasema nakuja. Hapo muda saa 4 interview saa 8.

Nkajivuta vuta saa 8 na unusu mchana nko pale getini nkaruhusiwa nkachoma ndani, in short nlikuwa mwenyewe tu, so nkaingizwa interview room nkakuta panel ya mtu tano pale kati nkapatwa na kizunguzungu cuz ilikuwa mara ya pili kupiga interview sikujua watu wanaweza kuwa wengi wananishambulia kwa maswali.

Ukapigwa utambulisho pale swali zikaanza "Tell us about yourself?" Sielewi nasemaje nkajikanyaga pale, nkaulizwa unatujuaje IOM, hapo nkasema kabisa sijui kitu kuhusu IOM, wakauliza job responsibilities and duties za HR walizozisema, nkajibu kiukweli mmeniita fasta sana na katika harakati zangu za kutafuta ajira si mambo yote au matangazo yote ntakumbuka. Wakaanza maswali mengine yani nilikuwa najikanyaga sana.

Moja ya interview ambazo nilikaa saa naongea tu licha ya kwamba nilikuwa naenda chaka ni hiyo. Mwishoni nilipomaliza maswali yao nkaambiwa "Asante kwa kuja".

Cha msingi ni kutojutia bali ni kurekebisha makosa yanayotokea, na kufurahia ikibidi hiyo ndo histori yenyewe.
Nshakufahamu kaka,tulikaa siku moja mmeetoka interview pale kituoni taifa kwenye tairi tukabadilishana mawili matatu.Mimi nlikuwa nimefata mzigo wangu pale kambi ya jeshi.Vipi ushanikumbuka??
 
Wanalafudhi ngumu sana inahitaji umakini sana kuelewa wanazungumzia nini na wao wenyewe wapunguze speed ya uongeaji.....

Ila kama wapo wazungu tu njia ambayo niliyotumia mara 3 kupata ajira ni licha ya kuwa na quality nzuri ila pia kutia huruma, yani nagusa quality zangu na najivisha umasikini ambao hauelezeki....
Hahaha umasikini usioelezeka ndio upoje mzee 😂😂😂😂
 
Miaka kama 7 iliyopita niliitwa kwenye usaili kwenye International Organization moja yenye ofisi hapa nchini, hawa wako chini ya UN..Tulikuwa watatu kwenye nafasi yetu na walihitajika watu wawili tu. mimi nilikuwa wa mwisho kabisa kuingia kwenye chumba cha usaili lakini kila mtu aliekuwa anatoka kwenye room ya usaili alikuwa na sura ya upole sana. Ikafika zamu yangu maana ndiye nilikuwa wa mwisho.

Waendesha usaili wote walikuwa wazungu then wanatumia lafudhi ile ya ndani kabisa. Nilipigwa maswali technical, nikawa sijui hata ninachojibu wala lugha ninayoongea . Wale mainterviewer wakawa hoi kwa kicheko. Walivyoona akili haiko pale ishahama kwa panick, wakanipa swali dogo angalau nirudi kwenye hali ya kawaida. Wakaniuliza kwa kiingereza " Bendera ya taifa ina rangi ngapi na maana ya tafsiri ya hizo rangi" huwezi amini Nilipuyanga 😀😀 naongea vitu hata mwenyewe sivielewi,Jamaa wakaangua kicheko tena. Kiukweli ile interview nilipanick sana

Mpaka leo sijui aina ya lugha niliyokuwa natumia kujibu maswali kwenye ile interview. Nikaambulia kumla mdada aliyekuwa anatuita kwenda kwenye room ya usaili angalau nikajipooza machungu ya kuchekwa.

🤣🤣🤣
 
Nshakufahamu kaka,tulikaa siku moja mmeetoka interview pale kituoni taifa kwenye tairi tukabadilishana mawili matatu.Mimi nlikuwa nimefata mzigo wangu pale kambi ya jeshi.Vipi ushanikumbuka??
Kabisa!! Nshakumbuka. Ni kweli kabisa.
 
Hahaha umasikini usioelezeka ndio upoje mzee
hahahahaha mfano nakaa kwenye nyumba ya babu yetu na ndugi zangu 12, nategemewa na familia mama dada zangu 3 na wadogo zangu 2 baba alitukimbia, kula yetu ya shida yani unaelezea vitu ambavyo itaonekana mshahara wako mzima utautumia kwa nidhamu na kuweka vizuri home
 
Mimi niliwahi kufanya interview DTB, interview nilifanyiwa na makanjibai Mimi kiukwl maneno mengi niliyotumia Ile siku ni "come again" "again please" hahah mpka walichoka
Mkuu umenikumbusha hahaha, mimi nilikuwa sijali napuyanga mpaka maneno kama "Mfecane war" niliyaweka wakati hayahusiki hata.
kidogo
 
Back
Top Bottom