Tuambie interview mbaya uliyowahi kuifanya

Nimefanya interview nyingi lakini nitaeleza kwa ufupi zile ambazo sikufanikiwa.

Baada ya kumaliza FVI, kulikuwa na mwaka mmoja uliofutwa JKT. Nikaamua kutafuta kazi. Kwanza nikapata interview kwa pharmaceutical company moja. Tukaitwa maeneo ya Kisutu. Nilipofika kikakuta watu zaidi ya 500 hivi! Halafu hakuna utaratibu mzuri wa interviewee kuingia ndani. Nilikaa nje, nikafikiria, baadaye nikaondoka.

Mwaka huo huo nikapata nyingine (Salesperson wa madawa). Kampuni ya Wahindi maeneo ya Uhuru iliyopo upande huu wa Kariakoo. Kwenye panel walikuwepo Wahindi 3 vijana. Nikijibu maswali wanacheka. Katikati ya interview nikawapandishia na kuchukuwa vyeti vyangu na kuondoka.

Miaka mingi imepita sasa. Nikapata interview ya UN, nje ya Tanzania, kwa Skype. Wale jamaa walikuwa wawili. Wakasema swali la kwanza linaulizwa kwa Kiingereza na kujibiwa kwa Kiingireza. Swali la pili linaulizwa na Kifaransa na kujibiwa kwa Kifaransa (ambacho sijui). Swali la kwanza nikajibu kwa Kiingereza. La pili likaulizwa kwa Kifaransa, nikaelewa swali lakini kujibu kwa kifaransa siwezi. Nikajibu kwa Kiingereza. Sikupata hiyo kazi.

Ukisoma comments nyingi hapa utagundua kwa nini wazazi wengine wameamua kupeleka watoto wao English medium schools.
 
Jamaa ada yao imechangamka, lakini pia inategemea na level baada ya kukupa mtihani wao na kuona unafaa kuanzia level ipi, kipindi kile Mimi nilipiga jwa 560k lakini kwa Sasa itakuwa juu...
ulivyopiga hiyo kozi ilikusaidia mkuu,unaweza kusikia na kufunguka ngeli kama ya CNN?au unaongea kawaida tu kama ngeli ya wasukuma?
 
Mimi juzi kati nimeitwa kwenye interview lakini walijichanganya nikafanya written ya nafasi ya juu zaidi ila nikafaulu kwenda oral interview.

Huko ndipo nilijuta maana nilikuwa sijawahi fanya project yoyote ya machine learning zaidi ya kusoma soma tu juu juu,nilikutana na technical questions za statistics na python nilijuta.

Jasho lilikotoka hata sielewi,nikawa najiropokea tu ili niwahi kutoka kabla sijazimia.

Ni hapo kwenye jengo lina vioo kibao afu refuu,lipo kati ya Ubungo na Mwenge.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app
 
I think TBS oral interview,,,dah nilianza vzur sana na introduction njaa na uchovu wa kusubir kuingia chumba cha interview na ile pannel ya watu nikajikuta napanick aicee nilijibu ovyo mpaka mama mmoja hv kwny pannel akanambia pambana baba maisha yako haya huku wengine wakicheka balaa nilivyotoka pale nikarudi mpole kwa mhindi kudadadeki
 
2018 kidogo nile maisha aseeee,nilipigwa interview moja matata via video call,mmoja yupo S.A na wengine wapo London.Kiingereza cha ndani kabisa ila nilipambana sanaa wale jamaa wa London walinielewa sana tatizo lilikuwa kwa huyu wa South Africa...Haikuwa bahati yangu ila ilikuwa bonge ya kazi ile aseee,nilipambana sanaaa mwanaume..Hii interview sitaisahau kbs...Ilikuwa ya masaa 3,pale conference nilikuwa na mdada operator wa mitambo tu ila interview inafanywa na wenyewe majuu huko.
 
Jamaa ada yao imechangamka, lakini pia inategemea na level baada ya kukupa mtihani wao na kuona unafaa kuanzia level ipi, kipindi kile Mimi nilipiga jwa 560k lakini kwa Sasa itakuwa juu...
nmeambiwa 650k, ila sijajua kama ndo unakuwa full package au bora liende tu ila kupitia kwako nmejifunza kitu mkuu
 
I think TBS oral interview,,,dah nilianza vzur sana na introduction njaa na uchovu wa kusubir kuingia chumba cha interview na ile pannel ya watu nikajikuta napanick aicee nilijibu ovyo mpaka mama mmoja hv kwny pannel akanambia pambana baba maisha yako haya huku wengine wakicheka balaa nilivyotoka pale nikarudi mpole kwa mhindi kudadadeki
Kujieleza ni changamoto kwa waswahili tulio wengi mkuu
 
Kuna moja walitangaza msd kila wilaya kama sikosei na walikua wanahitaji watu 33 kwa sisi wa Tmk,mtafutaji nikapeleka maombi nikapigwa chini.

Ikabidi nilazimishe maana kuna dogo nilikutana naye siku ya kupeleka maombi nimemzidi kwa level zote za elimu ila yeye aliitwa na kwa bahati mbaya au nzuri kipindi hicho tayari alikua kapangiwa shule ya kufundisha huko Bukoba.

Basi bwana interview ya kwanza written ikafanyika pale DUCE,kufika pale watu kama 300 hivi nikaona isiwe kesi tukaingia (ikumbukwe nilienda kwa jina la dogo ila vyeti vyangu mwenyewe),kufika ndani maswali yote yakaja ya civics sijui national symbol,sijui multipartism ili mradi kero tu.

Nikafanikiwa kupita pale...interview iliyofuata tukafanyiwa pale MSD kwenyewe darajani kwa mbele pale ile bwana tukashangaa tunabebeshwa mabox ya dawa yani unayatoa kwenye gari unaenda kuyapanga store tena manne manne halafu ni mazito yale...( nakumbuka kuna watu kama wanne hivi walisalimu amri hata interview yenyewe hawakufanya).

Nikapita na hapa...ya mwisho sasa ikabidi ikafanyike maktaba pale posta na ni oral...kizaazaa kikaanzia hapa,ukaguzi wa vyeti ukatofautiana na majina yaliyoandikwa wale jamaa si ndio wakachimba biti la kuniweka chini ya ulinzi nikajieleza pale wakanirudishia simu zangu maana simu zetu zote zilikua chini yao wakanitimua tangu siku ile mimi na interview kama chui na paka tu....
 
Dah Mkuu we ni hatari, yaani umezamia jina la mtu afu vyeti ni vyako
 
Ningefanyaje mkuu? Halafu hilo interview la mwisho nimeliwahi kutoka Kahama kabisa sema jamaa hawakua fair tu imagine watu 300 mpaka tukabaki 50 na wanatakiwa 33 nilikua natoboa kabisa
Yah ulipambana sana wangeweza kukufanyia consideration lakini tatizo kwenye issue kama hizo watu wanakuja kwa shughuli tofauti, wapo wanaotafuta kazi na wapo wanaokuja kwa 'kazi maalum'.

Kwa namna ulivyo penya hatua za awali huku jina sio lako, hata ingekuwa ni mimi ningekuchinjia baharini kwa usalama wangu, honestly ni ngumu sana mtu kukuamini kwenye mazingira hayo.
 
Wanalafudhi ngumu sana inahitaji umakini sana kuelewa wanazungumzia nini na wao wenyewe wapunguze speed ya uongeaji.....

Ila kama wapo wazungu tu njia ambayo niliyotumia mara 3 kupata ajira ni licha ya kuwa na quality nzuri ila pia kutia huruma, yani nagusa quality zangu na najivisha umasikini ambao hauelezeki....
I conqur mkuu.
Wazungu ukitia huruma tu na kuzihusisha na umaskini wa kutupwa, as long una quality kadhaa kati ya wanazozohitaji trust me you are nailing that job.
 
Yah ulipambana sana wangeweza kukufanyia consideration lakini tatizo kwenye issue kama hizo watu wanakuja kwa shughuli tofauti, wapo wanaotafuta kazi na wapo wanaokuja kwa 'kazi maalum'.

Kwa namna ulivyo penya hatua za awali huku jina sio lako, hata ingekuwa ni mimi ningekuchinjia baharini kwa usalama wangu, honestly ni ngumu sana mtu kukuamini kwenye mazingira hayo.
Angalau wewe ndio umeweza kunishawishi nikakuelewa ila wale jamaa aisee daaah wakanichimba na biti eti halafu nilikua na safari ya ardhi na mzee ikabidi aende tu maana hata hewani sikuwa nikipatikana
 
Lazma wakukate biti la maana ili kama umetumwa upeleke taarifa kuwa jamaa sio wa kisport sport

Ila nadhani ungetafuta namna ya kufanya reconciliation mapema kuwa me sikuwa shortlisted lkn nimekuja tu kushow up kama mtakuwa impressed na mimi.

Na ungewaeleza mfano, nimekuja baada ya mwenzangu aliyekuwa shortlisted kupata kazi tayari na hivyo hana interest tena na kazi hii ndio maana in the first place niliingia kwa jina lake lkn me ni Mr. So and so na cv zangu hizi hapa, who knows.... may be ungeweza kuwa considered.
 
Sio kwa roho zetu wabongo mkuu
 
Back
Top Bottom