Tuambie interview mbaya uliyowahi kuifanya

Tuambie interview mbaya uliyowahi kuifanya

Mimi sikuchemsha oral, nilichemsha practical. Miaka ile namaliza six Kama mwezi mshkaji wangu mmoja akaniambia Kuna kazi pahala huna hata haja yabkupeleka barua Wala CV. Akanielekeza nikaenda maeneo ya kijitonyama.

Kufika nikawakuta jamaa wapo smart wadada na wakaka wananyonga Tai. Nikasema yah hapa patanifaa. Nikajiyambulisha na kuwaeleza shida yangu. Wakaniambia nenda kwa HR chumba flani, nikamkuta mdada hr yupo na mkurugenzi wa kampuni. Wapo smart hatari.

Nikaulizwa maswali matatu tu Tena kiswahili. Unaitwa Nani, una elimu gani na unaelewa Nini kuhusu customer care in businesses. Nikafunguka kisawasawa. Nikaambiwa njoo kesho saa moja kamili asubuhi ukiwa smart tayari kuanza practical before giving you a contract. Nikatoka pale najiona Nina ngekewa ya kuzaliwa.

Asubuhi kumi nambili nipo pale. Mida Kama saa tatu nikaitwa ofisi ya marketing nikawakuta jamaa wawili, mmoja ndio inabidi awe job couch wangu. Nikaambiwa dogo Sasa kuanzia Sasa nakukabidhi kea huyu jamaa atakutrain wiki moja then utakuwa independent. Nikajimwambafy usjali mkubwa I'm a fast learner. Hee Mara yule couch akanipeleka store. Naona mwenzangu anachukua vistuli vya kukalia vya kukunja, chupa za chai, majagi ya juice. Then akaniambia Mimi nichukue pia. Me namuuliza vya Nini, ananiambia ndio anaenda kunifundisha kazi.

Nikamuuliza tunaenda kuzunguka kule mjini kwenye maofisi ya watu? Bila noma akanijibu ndio..... Kumbe hautanisumbua wewe maana una idea idea ya hii kazi.
Dah, nikakumbuka jinsi tulivyokuwa tunawacheka Hawa machinga smart mtaani, halafu enzi zile za kikwete mtaani masista duu kibao halafu wanahela nyingi za kuhongwa na kina liyumba sjui!!!! Nikasema usintanie wewe.

Nikamwambia tu bro hii interview Mimi nimeshafeli. Akataka sijui kunishawishi, nikamwambia bro Mimi Nina matusi Sana nitagombana tu na watu. Jamaa ananiambia dogo acha kuchezea bahati. Akh hata sikumsikiliza nikasepa.

DS Marx nawakumbuka Sana hope mnaendelea vizuri.
 
Kama uko Dar basi unaweza sikiliza 103.3 radio bbc world news. itakusaidia kukuza mauwezo ya lugha ya ENGLISH.

my pleasure to help
 
Mwezi wa 5 Mwaka huu nilifanya interview katika Microfinance Moja inaitwa Serena ipo Mkabala na Victoria .

Nilituma Maombi walikua wanataka Credit Manager nikafanikiwa kuwa shortlisted nikapigiwa simu na kutumiwa Msg nikaenda katika written wakasema wanatoa majibu kesho yake maana ilikua ni Jumatano interview oral ni Jmox

Baada ya kufika Makumbusho shule ya kijitonyama nikakutana na watu kama 25 ivi kumbuka wanataka mtu Mmoja tukapiga paper kiukweli ule mtihani ulikua mgumu but kama mtu amesoma maswala ya finance anateleza so mimi nilikua nateleza pale nikatoka na hope nimetusua.

Siku ya Alhamis ikapita sikupata msg wala kupigiwa simu nakaongea na wenzangu nliopiga nao paper wawili walipigiwa simu wakaambiwa jumamosi kila mtu akapewa muda wake wa interview.

Mimi mpk ijumaa saa 6 mchana bado nikakata tamaa inafika saa tisa mchana napata msg ya kuonesha nimeitwa interview kesho saa tisa nikasali nianza pitia pitia maswala ya Loans.

Jumamosi ya interview nliambiwa niende saa tisa mimi nkaenda saa sita nkawai ili nizoee mazingira wenzangu wanaingia mule ndani wanakaa nusu saa wengine wanakaa dk 10 apo na pressure kweli mara ikapigwa interview mpk saa kumi nikawa wa mwisho kuingia apo sijala kitu since asubui wale jamaa interviwer walikua wanapita na Mavyakula tu ata karibu hapana.

Sasa niko pale nje naongea na jamaa anafanya kazi pale ananipa dondoo za kampuni mara naskia Hr anasema kabaki mmoja wale watu wa pannel wanasema tumechoka tushafanyia watu 11 naisi tushapata best kwa wote ni nani uyu hawezi badili matokeo Hr anawakonvice sana nkaitwa.

Nimefika pale ndani naona kama hawana interest ivi Hr akatambulisha wote then akaniomba niji introduce jina, experience, education nkafanya ivyo.
Mara jamaa pembeni anasema ongeza sauti utakuaje wa kiume sauti iko chini nkaongeza then yakaanza maswali kwenye Cv nikajibu jamaa wakasema experience yako haiendani na hii kazi ,

Unataka mshahara wa sh ngapi nkawatajia, unaswali gani nkawauliza maswali mawili wanatumia vigezo gani kuwin market, na wanaset vp interest swali likarudishwa kwangu kwanini umeuliza nkawaambia coz MFis nyingi zinakufa kwenye vitu vikuu 2 nlivyotaja apo wakauliza mfano nikawapa then wakaanza wewe haujui kitu zikaingia siasa za mikopo ya serikali wakauliza unajua hii sijui TASAF nikawa nasema hapana mimi siasa sifatilii then nkaskia asante tukiwa na shida na wewe tutakujuza.

Nkatoka nje ata skukaa dk 10 nimetoka pale ninahasira sana nkajiuliza aya ndio maswali anaulizwa mtu wa top position kweli?

Afu why kama walikua hawako interested wangesema si kuniharibia muda wangu niko nje pale naskia wanasema uyu hakuna kitu kabisa yani ata elimu aliopata haijamsaidia anambwela mbwela tu na iyo ikawa mwisho wa story
 
Pole mkuu jamaa walikufanyia fitna tu inawezekana walikuwa na mtu wao.... Alafu siku nyingine ukiambiwa utaje mshahara unaweza sema nipo tayari kupokea mshahara ambao utaendana na input yangu pamoja na mafanikio nitakayoiletea kampuni
 
Yangu nilifanya na watu wanaitwa Wezesha wazawa microfinance, Hawa jamaa walipigia simu kazi ambayo nishaomba miezi nane ishapita,,, Wakasema Njoo kwa ajiri ya interview ,nafika pale ofisin pao nawaambia niliitwa kwa ajili ya interview wanabaki wananishangaa tuu, Kumbe aliyebipigia simu hata hakutoa taarifa kwa wenzake.

Nilikaa pale Kama saa moja hivi ,nikawafata nikawambia Kama hamna interview naombeni mnirudishie gharama zangu za usumbufu, niliwapelekesha hawatakuja sahau , baadaye Wakasema tutafanya mida ya saa nane nikawambia sawa,, nikatoka pale nikaenda kunywa k- vant na safari mbili, mda ulivyofika wa saa nane maana nilikuwa Niko peke yangu tunafika kwenye interview room nikawaambia mie nahitaji hela zangu na mda niliyopoteza.

Nilivyokuwa nimechange walitoa nauli wajinga wale.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka kama 7 iliyopita niliitwa kwenye usaili kwenye International Organization moja yenye ofisi hapa nchini, hawa wako chini ya UN..Tulikuwa watatu kwenye nafasi yetu na walihitajika watu wawili tu. mimi nilikuwa wa mwisho kabisa kuingia kwenye chumba cha usaili lakini kila mtu aliekuwa anatoka kwenye room ya usaili alikuwa na sura ya upole sana. Ikafika zamu yangu maana ndiye nilikuwa wa mwisho.

Waendesha usaili wote walikuwa wazungu then wanatumia lafudhi ile ya ndani kabisa. Nilipigwa maswali technical, nikawa sijui hata ninachojibu wala lugha ninayoongea . Wale mainterviewer wakawa hoi kwa kicheko. Walivyoona akili haiko pale ishahama kwa panick, wakanipa swali dogo angalau nirudi kwenye hali ya kawaida. Wakaniuliza kwa kiingereza " Bendera ya taifa ina rangi ngapi na maana ya tafsiri ya hizo rangi" huwezi amini Nilipuyanga 😀😀 naongea vitu hata mwenyewe sivielewi,Jamaa wakaangua kicheko tena. Kiukweli ile interview nilipanick sana

Mpaka leo sijui aina ya lugha niliyokuwa natumia kujibu maswali kwenye ile interview. Nikaambulia kumla mdada aliyekuwa anatuita kwenda kwenye room ya usaili angalau nikajipooza machungu ya kuchekwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanalafudhi ngumu sana inahitaji umakini sana kuelewa wanazungumzia nini na wao wenyewe wapunguze speed ya uongeaji.....

Ila kama wapo wazungu tu njia ambayo niliyotumia mara 3 kupata ajira ni licha ya kuwa na quality nzuri ila pia kutia huruma, yani nagusa quality zangu na najivisha umasikini ambao hauelezeki....
Aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi juzi kati nimeitwa kwenye interview lakini walijichanganya nikafanya written ya nafasi ya juu zaidi ila nikafaulu kwenda oral interview.

Huko ndipo nilijuta maana nilikuwa sijawahi fanya project yoyote ya machine learning zaidi ya kusoma soma tu juu juu,nilikutana na technical questions za statistics na python nilijuta.

Jasho lilikotoka hata sielewi,nikawa najiropokea tu ili niwahi kutoka kabla sijazimia.

Ni hapo kwenye jengo lina vioo kibao afu refuu,lipo kati ya Ubungo na Mwenge.

Sent from my Redmi Note 5 using JamiiForums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi juzi kati nimeitwa kwenye interview lakini walijichanganya nikafanya written ya nafasi ya juu zaidi ila nikafaulu kwenda oral interview.

Huko ndipo nilijuta maana nilikuwa sijawahi fanya project yoyote ya machine learning zaidi ya kusoma soma tu juu juu,nilikutana na technical questions za statistics na python nilijuta...
Pole sana unaweza ukapata lakini hainaga formula
 
Back
Top Bottom