Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Status
Not open for further replies.
He does not deserve to be paid such big amount of money period! 35M for what?? Let's be serious ah ah!
 

Ukikutana mahali na Magufuli, akakuomba ushauri, ucjarbu kumpa mana umejaa moyo wa husda sana....badlika, hyo ni destiny ya failures
 

Wewe utakua unafaidika kwa namna moja au ingine na hiyo Mil30 anayoipata Nehemia Mchechu.
Haiwezekani shirika la uma mkurugenzi wake alambe Mil30 kwa nchi kama Tanzania, bado hatujafikia huko. Kwa kazi ipi hasa?
 
Mleta uzi aseme mambo anayoyafahamu fika na kwa kina na asiseme mambo anayodhani anayajua, aje aseme hapa sheria ya NHC inasemaje, aje atuambie kama iliwahi kubadilishwa na pia aseme je zile nyumba za mabibo hazikuwa za NHC? NHC ya Nyerere na alokabidhiwa huyo anayesema anaonewa wivu zina lengomoja au malengo tofauti?
 
 
Mchechu anastahili huo mshahara.. Kama serikali inaona huo mshahara ni ghali kuliko perfomance yake watafute DG wakumlipa laki 8 anayepga dili za M100 kwa mwezi..
 
DG wa TANAPA alipwe mabilion mangapi!? Unajua sekta ya utalii inaingiza kiasi gani kwa nchi? Au Kamishna wa TRA tumlipe trillion ngapi? Tukitaka kila mtendaji anayekusanya raslimali kwa niaba ya serikali alipwe kulingana na anachokusanya....sijui kama tutafika.

Kwa kukusaidia tu....NHC chini ya Mchechi inatoa gawiwo la mil 200 kwa serikali kuu kila mwaka. Je, faida ya huyo Mchechu ipo wapi!?

Pia kama hujui, pesa zote anazopata kutokana na mauzo ya nyumba uwa zinatumika kulipa mikopo aliyoichota kwenye mabenki.
 

Ni wapi Mchechu alitajwa kuhusiana na mshahara wa Tshs. 35 ml?
 

Ni wapi Mchechu ametajwa kuhusiana na kupokea mshahara wa Tshs. 35 ml?
 
Kwani yeye tu ndio CEO ambaye shirika lake lina mchango mkubwa? Kwanza sijui NHC inachangia kiasi gani kwenye pato la taifa. Kwa hoja yako basi DG wa TANAPA ndo anatakiwa ale hela ndefu maana tourism ina mchango mkubwa kwenye GDP ya nchi.
Na bado takribani 60% ya watanzania wanaishi chini ya dollar moja,kama hizo nyumba sio kwa ajili ya manufaa ya umma wasio kuwa na uwezo haina maana
 
mimi nimesema EPL,
halafu Madrid haijawahi kwa siku za hivi karibuni kuwa na mkusanyiko niliokutajia. Man city wamesajili majembe angalau ndiyo yameiwezesha angalau kupita 16 bora
 
Mtamkumbuka kikwete, ten years mlibembea sana na matusi na kejeli juu kwa wananchi,unatetea mafanikio ya watu waliokwiba pesa za umma,arudi sasa kwenye hiyo asasi hakuna mtu atahoji,nhc ni mali ya umma,

halafu natoa maoni kwa magufuli hawa mameneja na wakurugenzi walipwe mil 2 tu na mawaziri mil 3, kwanza serikali haina pesa, pili kubana matumizi, tatu hizo ni kazi za kuhudumia jamii kama ilivyo kwa walimu na madaktari anae taka afanye huwezi kwendaa!mmetusumbua sana huku kitaa na pesa za ufisadi,

nakumbuka kisa kimoja nilikutana nacho kwa mziba pancha,wakati mimi na bargain jamaa aniuzie tairi used kwa elf 30,akaibuka yule meneja wa bank bot yeye anataka jamaa amchekie upepo matairi,basi jamaa akacheki tairi zote zikawa sawa,akamwambia tayari bosi ni elf 1 alahaulaa! Meneja anamwambia mziba pancha hii ni range wewe kupima upepo sio elf 1,akatoa elf 40 akampa jamaa huyo akasepa zake,sasa si kaniachia msala mimi kabla meneja hajafika mziba pancha alikua anaelekea kunipa tairi kwa elf 30,baada ya kupewa ile 40 kabadilika bwana ananiambi bro hili tairi mwisho elf 50 na yeye nae aka anza kunitia vijembe ananiambia braza magari haya gharama usilazimishe kama vp uza gari yaani ! Nilitoa hiyo 50
 
Kati ya watu m46, hivi yeye tu ndio ana skili nyingi?
skill ya kuwanyang'anya fursa raia waliopewa na nyerere rukhsa ya kuishi mitaa ya upanga kama mindu, na maeneo mengine na kuwapa nafasi wahindi, waarabu na wachina hukuakilipwa na jamii anayowafukuza.
 
Mbona Makocha wa Taifa Stars wanalipwa mishahara mikubwa na tunaishia kuwa kichwa cha mwendawazimu hawasemi?
Hahahahahaha,mkuu kuna uzi humu yapata wiki moja sasa unajadili mada ya mshahara anaolipwa Mkwasa.
 
Tena hiyo ndogo sana... Mchechu anastahili kulipa Million 70 kama wanavyolipwa DG wengine...
 
Nashukuru kwa ufafanuzi wako wa kina....haya ndio niliyokuwa nayataka na sio bra bra.....

Kwa mujibu wa maelezo yako( kama ni kweli) basi nami naungana na wadau wanaopinga mshahara wa huyo bwana.....kama hicho ndicho anachoizalishia serikali....
 
Hii ni boomerang effect. Ukiirusha ujue itakurudia. Alikejeli sana watu, mpaka wakajiuliza kijana huyu hii jeuri anaipata wapi? Sema wivu, sema roho mbaya, sisi tunasubiri ushahidi. Mtu aliyekosa unyenyekevu na kudharau watu wenye umri wa wazazi wake lazima amefanya madhambi mengi. Na kama alijipa nyumba naomba itaifishwe mara moja. Akae sehemu ya hadhi yake, lupango.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…