Tuache Wivu kwa Nehemia Mchechu

Status
Not open for further replies.
Asante ndugu kwa hili bandiko tatizo watanganyika tunakariri mambo
 
hicho sio kigezo,makosa yalianza pale serekali ilipomfuata na kumuangukia,kazi ingetangazwa then watu washindanishwe,ingekuwa ndo hivyo sasa kuna maana gani ya watu kusoma??
Ndugu TAI anatua kwenye MZOGA ukiona watu wanakutafuta wakupe kazi manake wanakubali uwezo wako....kwanini sikutafutwa mimi...ushauri wangu kwa vijana wote waliokwenye Nafasi yyt ya Ajira lazima afanyekazi at the maximum... mwisho wa siku kuna kufanikiwa zaidi lkn mtu unafanyakazi chini ya kiwango Nani anataka kuajiri LOOSER
 
Msambichika, nisaidie majibu katika haya;

1. Kuna ukweli kiasi gani unaposema mshahara haupangwi au kutolewa kutokana na kiwango cha elimu cha mtu?.Hivyo si sahihi kumlipa Prof. anayefundisha chuo kikuu mshahara sawa na Tutorial Assistance ambaye "anaakili" sana.!

2. Huyo mkurugenzi kabla ya Nehemia aliyekuwa anazalisha bilioni tatu tu, unadhani hakuwa na akili za kuzalisha zaidi au kwa kuwa serikali ilikiwa haijaamua kuwekeza intensively katika shirika hilo la umma?

3. Maswala ya uendeshaji wa biashara binafsi kama kuendesha timu yako ya mpira, hayaendani na biashara zinazofanywa na mashirika ya umma. tambua kuwa lengo kuu la serikali kupitia taasisi hizo ni kuhalalisha inatoa huduma kwa wananchi wake. Kama Nehemia anajenga na kuuza nyumba hasa kwa wageni, Sera hiyo anayoifanya haiendani na Sera ya serikali ya kuhakikisha watu wake wanapata makazi bora. Basing on your argument ni kweli Msechu "anaakili" kubwa kuliko ma DG wote hapa nchini?
 
Asante ndugu kwa hili bandiko tatizo watanganyika tunakariri mambo
Mkuu watanzania hawakariri mambo, siku hizi wanauelewa mpana wa mambo!

Ukiona wanahoji Pesa anayolipwa jamaa huyo jua hawakajua awali kama kodi zao zinatumika kulipa watu wa namna hiyo!

Si dhambi kuhoji, ni wajibu wa wanaohojiwa kutolea ufafanuzi na sio kuwabeza kuwa hakuna mtanzania .wenye akili kama msechu na kustahili malipo hayo!
 
hata akina maswi walifuatwa kuombwa hivyo hivyo yuko wapi leo hii,ukipewa kazi unapewa na job descriptions zako zikikushinda unaachia ngazi,ndio maana ya ajira,ukiona hivyo ujue kuna mahali mambo hayapo sawa??

 
Mreta mada. Umetumwa. Ujee kumtetea. Sisitunaitaji. Atujibu. Yeye. Mwenyewe.
 
Wakati watu wako busy kumsifia ana miakili huyo CEO mwenyewe interview yake aliyoiweka juu ya website yao anajivunia balance sheet ya shirika yenye billioni $2 and 20,000 houses it as if asilimia kubwa ya hizo nyumba kajenga yeye.

Kumaliza mzuzu wa fitina kwanini asitoe financial report we all know hiyo balance sheet large contribution ni value ya majengo sio cash assets; na income kubwa ni rent ambazo anan'gamua wananchi ndio zinazosaidia kuonekana shirika lina pesa lakini sio miradi yake binafsi aliyobuni walidai nyumba mchikichini zimeisha leo wanapangisha tena kwa wabantu tu wakawaida.

It was all predictable bila ya rent hike alizokuja nazo sasa hivi angeshakuwa chali yaani n'gombe wa maziwa serikari iliyomuachia awakamue atakavyo kwa madai ya kuwa wako chini na bei ya soko ndio wanaomfichia madeni yake na ubovu wa miradi yake the guy is useless.
 
NCHI hii ina watu MASIKINI wengi mno. Unapodai malipo/mshahara wafikirie na hao wanaoishi kwa chini ya shs elfu1 kwa siku.
 
Mimi nasikitika sana hawa jamaa wa NHC wameingia ubia na wahindi kujenga majengo mengi na makubwa yakiwemo yaloanguka na lile linalovunjwa bila kutangaza tenda.PPRA uko wapi ? hayo majengo ni ya serikali walichotakiwa NHC ni kutangaza mtu anaetaka kuingia ubia wa ujenzi ,basi watoe tender ! wao wanafuata wahindi kimya kimya ! na wahindi kwa kutumia hati miliki za NHC wanapata mikopo kiulaini ndo wanajenga na zingine zikibaki mambo mengine ! halafu eti mnamsifia Mchechu ? watu wanapiga hela ndefu hapo ! hawa jamaa wanatumia Landcruisers za kisasa kila director wakati kila mmoja wao amekopeshwa Landcruiser mpya ! sasa kwa nini wasitumie hizo walizokopeshwa NHC ikawapa mafuta ? wamekopeshwa magari na bado wanatumia magari ya kisasa ya NHC jamani huu si ndo ufisadi wa waziwazi ?mi nashangaa mheshimiwa raisi hajatujumbua jipu hili ! mehishiwa Raisi NHC ni jipu kubwa sana.
 
Napendekeza Msechu awe CEO wa AIR TANZANIA baada ya Magufuli kununua ndege alizoahidi na kuwaondoa watumishi wote. Halafu alipwe 40M! Huyu kijana in hazina ya Taifa! Tuache wivu!
 
Napendekeza Msechu awe CEO wa AIR TANZANIA baada ya Magufuli kununua ndege alizoahidi na kuwaondoa watumishi wote. Halafu alipwe 40M! Huyu kijana in hazina ya Taifa! Tuache wivu!
He He he yaani huna mtu mwingine mwenye vision na exposure ya nini kinaendelea duniani ila Mchechu. Pole for that 46 m people you only see one. sitaki kufikiri upeo wako wa kufikiria ila nihisi umetumia hisia zaidi kuliko kichwa chako. Na kama ni kichwa fanya mabadiliko haraka utaachwa na wakati. wewe huoni arguments zinazotolewa ukaelewa kwa mapana nini kinaendelea onaongelea wivu. Wacha uvivu wa kufikiri bwana.
 
Mimi ninavyo jua serikalini hakuna kunigotiate malipo, yapo kwa elimu ,miaka ya kazi na vyeo kulingana na muundo wa sehemu husika. sasa ile post ilikuwa na benefit zake kilichofanyika ni kuvuruga scheme kwa manufaa ya MCHECHU does it worth that transformation ? Je huo sio uvunjwaji wa sheria za ajira serikalini? kwanini ifanyike hivyo? analipwaje zaidi ya katibu mkuu wake au waziri toeni reason sio hakuna mtu kama yeye wakati wato tena hawata piga dili yaani waadilifu zaidi Subiri post inapatiwa mtu.
 

mchechu hakutaka kuafanya kazi serikalini kwa sababu mbalimbali na mojawapo mishahara midogo. serikali ikamfuata na kutaka huduma yake, ni wazi jamaa ameweka dau analolitaka. sio kila mtu anaenjoy mishahara midogo na ukiritimba, na sio kila mtu yuko tayari kuwahudumia watanzania kwa kufanya kazi serikalini. kama magufuli na watanzania wengine wanafikiri mchechu anachofanya ni kibaya then wakatishe mkataba wake. aliamua kwenda private sector kwa sababu zake, msifamfanye awe sehemu ya kutoa nyongo zenu za chuki bila sababu za msingi
 
Mkuu huyo jamaa ulie mjibu amemtaja Mchechu nadhani baada yakuona kazi anayofanya hapo NHC kwa kumthibitishia kwamba NCHI hii sio Mchechu tu sivibaya ukataja baadhi ya Vijana wengine kama yy wanaofanya kazi zinazoonekana
 
Mkuu unaweza kuthibitisha hii
 
Mkuu huyo jamaa ulie mjibu amemtaja Mchechu nadhani baada yakuona kazi anayofanya hapo NHC kwa kumthibitishia kwamba NCHI hii sio Mchechu tu sivibaya ukataja baadhi ya Vijana wengine kama yy wanaofanya kazi zinazoonekana
Kuna kazi huoni kwa macho kwa maana ya majengo lakini zipo documented sasa utasemaje. wapo walimu wazuri sana lakini utasifia wanafunzi kuwa wanaakili husifii mwalimu aliye mfundisha, kunaadministrators wazuri sana huwezi kuona utasikia wanasifiwa. Kuona majengo kunakufanya usifie mtu je umejua yanaleta faida gani katika uchumi wa nchi? Nini lengo la uanzishwaji NHC kujengea kina nani ? umefanya uchunguzi ni kina nani wanunuzi wa hizo nyumba? Baada ya miaka kadhaa nini itakua hali ya Mabenki ambayo yamefacilitate ujenzi wa majumba hayo? kuna mkakati gani wa kuzuia kilichotokea Dubai kiuchumi kisitokee huku? ukisha nijibu hayo maswali Mlipe Mchechu 35M will be very happy. naomba tuangalie kwa misingi hiyo sio kutaja majina ya watu
 
Angaliwe upya! Hana haja ya mshahara wote huo, maana anachokifanya sio faida kwa Watanzania walio wengi!

Mtu kama Mkurugenzi wa Muhimbili Hosp alistahili kulipwa zaidi ya Mchechu, maana anaokoa
Mkurugenzi wa MUHIMBILI analipwa shilingi ngapi
kazi kwako kufuatilia.....!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…