Tuache unafiki, sasa ndio nchi inagawanyika!

Sasa tunao walamba asali, walamba shubiri, walala hoi na pia mafisadi papa na machawa wao! Mnajitoa akili sababu ya shibe haramu, mnasifia mlipostahili kukemea! Wabunge mmegeuka "wabonge". Mbunge mwenye akili timamu, anasimama na kuomba bei ya mafuta iongezwe (ulaaniwe Jerry Slaa). Bila hata aibu, wakati anaomba hivyo... Bei huko mitaani ziko hivi:
  • Sukari @kg 3,200/=
  • Mchele @kg 3,200/=
  • Sembe @kg 1,700/=
  • Nyama @kg 7,500/= mpaka 8,500/=
  • Mkaa gunia @ 70,000/=
  • Maharage @kg 4,000/=
Sasa bado hatujaongelea tozo kwenye miamala! Bei za vifaa tiba bei juu! Madawa bei juu, huku hata upatikanaji wake ukiwa ni 30% huko kwenye hospitali za umma. Kiwango cha elimu shule za umma iko hoi!

Malipo ya wafanyakazi wanaostaafu au kuachishwa kazi kwenye mifuko ya pensheni yamegeuka sababu kuu ya vifo kwa wastaafu hao, kisa hayatolewi kwa wakati stahiki.

Lakini wafanyakazi na maafisa wa mashirika hayo, wanazitumia pesa za wastaafu kwa kujikopesha kiasi kwamba, mikopo yao inaelekea kulingana na pato zima la mifuko hiyo!

Rushwa mitaani na kwenye ofisi za umma imerejea kwa kasi ya kutisha!

Ubadhirifu kuanzia miradi ya kimkakati hadi Tamisemi ni wa kutisha, na pengine ni haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii.

Ripoti ya CAG inatisha kuisoma, halafu Spika wa bunge, anawazuia wabunge kuhoji bungeni... eti mpaka baada ya miezi saba kuanzia sasa.

Huku wajinga fulani, waandishi habari wasakatonge, wanajiundia cartel pamoja na mafisadi wa Tanesco, mafisadi wa mashirika ya mawasiliano, mafisadi wa hazina ya taifa, mafisadi wa miundombinu ya nchi hii.

Eti wanaandika kitabu kuhusu miradi ya wilayani Chato, kwamba ni kielelezo cha udikteta wa Magufuli.

Ila wanashindwa kutuandikia kama kuna tofauti gani kati ya miradi ya Chato na hii mingine ambayo yote aliiasisi Magufuli kama vile:
  • Mahospitali na vituo vya afya zaidi ya 360 nchi nzima.
  • Mitambo mipya ya vipimo kwenye hospitali zote za rufaa nchi nzima.
  • Miradi ya ujenzi wa masoko mapya ya kisasa mikoani.
  • Bwawa la umeme la JNHP.
  • Reli mpya ya kisasa ya SGR, ambayo sasa wanaifisadi kwa kwenda mbele.
  • Ujenzi wa meli mpya ziwa Victoria na Ziwa Nyasa, pamoja na ukarabati mkubwa wa MV Victoria.
  • Ujenzi wa daraja la Sallender, ambalo wao wamekuja kulipa jina jipya la Tanzanite.
  • Ujenzi wa daraja jipya la Mto Wami.
  • Ujenzi wa daraja jipya la Kigongo - Busisi la kipekee na la kwanza kwa urefu Afrika Mashariki.
  • Ununuzi wa Rada mpya nne, uliopelekea nchi kuingiza mapesa ya kigeni, kutokana na huduma tunayoitoa kwa nchi jirani za Kenya, Rwanda, Burundi na DRC.
  • Ufufuaji wa viwanda vya viatu na samani, pamoja na kilimo vinavyomilikiwa na majeshi yetu ya Magereza, JKT na hata JWTZ.
  • Ununuzi wa madawati kwa shule zote za umma nchi nzima.
  • Kukomesha tatizo la ukatikaji wa umeme, iko chini ya shirika la Tanesco nchini.
  • Kuwakamata bila uoga mafisadi, pamoja na vibaraka wao na kuwasweka lupango bila uoga.
  • Kuondoa vyeti feki kwenye ajira rasmi za umma.
  • Kukomesha mishahara hewa na kutumbua wazembe na wabadhirifu bila haya.
  • Ujenzi na ukamilishwaji wa Nyumba za Maghorofa ya Magomeni Quarters!
  • Ujenzi wa hosteli za Chuo Kikuu UDSM na kuondoa kero iliyokuwepo.
  • Ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami kote jijini Dar es Salaam.
  • Kuihamishia serikali makao makuu Dodoma na ujenzi wa Ikulu mpya ya Chamwino!
Mambo ni mengi huwezi kuyataja humu yote.....
Magufuli hachafuki, kadri mnavyotaka kumchafua ndivyo mnavyochafuka nyinyi vibaraka wa mafisadi mpaka siku zenu zitakapotimia.
Walaaniwe wote wanaomsema vibaya Hayati JPM na watu wote waseme Amina..
 
Lori zinazopaki pale njia ya kwenda Mchicha siku hizi

Superdoll walivyosambaza tanker service load yote mpaka Toyota

Hii ni ishawara wazi, inayoonekana na isiyoonekana ya kuwa WALE waua miundombinu wamerudi!

Mjamzito aliyepitia kisu akaruhusiwa kisa hakuna wodi za kutosha, karudi hospital hoi baada ya siku moja.
 
Sijui maana picha haifunguki, chagua yoyote tu. Sukuma gang mmekuwa na mwisho wa aibu sana. Poleni na kubalini matokeo na siyo kuomboleza na kilia kila siku eti watu wanalamba asali
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Acha kulia tafuta mrija japo kwa nyie sidhani maana mletenda uovu mwingi sana
 
Mwisho wa aibu unaoutaja ni upi mkuu?

Kwamba ubadhirifu uliotajwa na CAG ni wa Sukuma Gang au Msoga Gang?

Kama vile unateseka sana na kutumbuliwa vile?
Mawazo yako ni sawa na Cheti feki mmoja hivi.
Ndio sababu hujitambuwi tunaongelea mambo tofauti na tena nyeti na muhimu!wewe umekalia Sukuma Gang!
 
Hizo takataka zenu mnazohubiri hapa kila siku kwa kutokubaliana na ukweli kwamba mungu wenu hayupo ndo zinagawa watu sasa!
Hata Hitler alijenga barabara na viwanda lakini alikufa na taifa likaendelea sembuse nyie wanyea kwenye mashimo?
Kwamba kwasababu fulani amefariki basi matatizo yameongezeka huo ni unafiki mkubwa ambao mm naukataa
Mtu ambae hakuajiri watu miaka 6 na kupandisha mishahara anaonekanaje kwamba Ali solve matatizo?
Mtu ambaye alidanganua taifa kwamba anajenga viwanda kumbe uongo hili mbona hamsemi?
Wew naye huna akili unajaza Mambo ya aibu Tu hapa
 
Sasa tunao walamba asali, walamba shubiri, walala hoi na pia mafisadi papa na machawa wao! Mnajitoa akili sababu ya shibe haramu, mnasifia mlipostahili kukemea! Wabunge mmegeuka "wabonge". Mbunge mwenye akili timamu, anasimama na kuomba bei ya mafuta iongezwe (ulaaniwe Jerry Slaa). Bila hata aibu, wakati anaomba hivyo... Bei huko mitaani ziko hivi:
  • Sukari @kg 3,200/=
  • Mchele @kg 3,200/=
  • Sembe @kg 1,700/=
  • Nyama @kg 7,500/= mpaka 8,500/=
  • Mkaa gunia @ 70,000/=
  • Maharage @kg 4,000/=
Sasa bado hatujaongelea tozo kwenye miamala! Bei za vifaa tiba bei juu! Madawa bei juu, huku hata upatikanaji wake ukiwa ni 30% huko kwenye hospitali za umma. Kiwango cha elimu shule za umma iko hoi!

Malipo ya wafanyakazi wanaostaafu au kuachishwa kazi kwenye mifuko ya pensheni yamegeuka sababu kuu ya vifo kwa wastaafu hao, kisa hayatolewi kwa wakati stahiki.

Lakini wafanyakazi na maafisa wa mashirika hayo, wanazitumia pesa za wastaafu kwa kujikopesha kiasi kwamba, mikopo yao inaelekea kulingana na pato zima la mifuko hiyo!

Rushwa mitaani na kwenye ofisi za umma imerejea kwa kasi ya kutisha!

Ubadhirifu kuanzia miradi ya kimkakati hadi Tamisemi ni wa kutisha, na pengine ni haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii.

Ripoti ya CAG inatisha kuisoma, halafu Spika wa bunge, anawazuia wabunge kuhoji bungeni... eti mpaka baada ya miezi saba kuanzia sasa.

Huku wajinga fulani, waandishi habari wasakatonge, wanajiundia cartel pamoja na mafisadi wa Tanesco, mafisadi wa mashirika ya mawasiliano, mafisadi wa hazina ya taifa, mafisadi wa miundombinu ya nchi hii.

Eti wanaandika kitabu kuhusu miradi ya wilayani Chato, kwamba ni kielelezo cha udikteta wa Magufuli.

Ila wanashindwa kutuandikia kama kuna tofauti gani kati ya miradi ya Chato na hii mingine ambayo yote aliiasisi Magufuli kama vile:
  • Mahospitali na vituo vya afya zaidi ya 360 nchi nzima.
  • Mitambo mipya ya vipimo kwenye hospitali zote za rufaa nchi nzima.
  • Miradi ya ujenzi wa masoko mapya ya kisasa mikoani.
  • Bwawa la umeme la JNHP.
  • Reli mpya ya kisasa ya SGR, ambayo sasa wanaifisadi kwa kwenda mbele.
  • Ujenzi wa meli mpya ziwa Victoria na Ziwa Nyasa, pamoja na ukarabati mkubwa wa MV Victoria.
  • Ujenzi wa daraja la Sallender, ambalo wao wamekuja kulipa jina jipya la Tanzanite.
  • Ujenzi wa daraja jipya la Mto Wami.
  • Ujenzi wa daraja jipya la Kigongo - Busisi la kipekee na la kwanza kwa urefu Afrika Mashariki.
  • Ununuzi wa Rada mpya nne, uliopelekea nchi kuingiza mapesa ya kigeni, kutokana na huduma tunayoitoa kwa nchi jirani za Kenya, Rwanda, Burundi na DRC.
  • Ufufuaji wa viwanda vya viatu na samani, pamoja na kilimo vinavyomilikiwa na majeshi yetu ya Magereza, JKT na hata JWTZ.
  • Ununuzi wa madawati kwa shule zote za umma nchi nzima.
  • Kukomesha tatizo la ukatikaji wa umeme, iko chini ya shirika la Tanesco nchini.
  • Kuwakamata bila uoga mafisadi, pamoja na vibaraka wao na kuwasweka lupango bila uoga.
  • Kuondoa vyeti feki kwenye ajira rasmi za umma.
  • Kukomesha mishahara hewa na kutumbua wazembe na wabadhirifu bila haya.
  • Ujenzi na ukamilishwaji wa Nyumba za Maghorofa ya Magomeni Quarters!
  • Ujenzi wa hosteli za Chuo Kikuu UDSM na kuondoa kero iliyokuwepo.
  • Ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami kote jijini Dar es Salaam.
  • Kuihamishia serikali makao makuu Dodoma na ujenzi wa Ikulu mpya ya Chamwino!
Mambo ni mengi huwezi kuyataja humu yote.....
Magufuli hachafuki, kadri mnavyotaka kumchafua ndivyo mnavyochafuka nyinyi vibaraka wa mafisadi mpaka siku zenu zitakapotimia.
Ulianza vizuri ukaharibu ulipoanza kumtetea mwizi, fisadi, muuaji katili, dikteta na mwehu Magufuli
 
ccm ndiyo chanzo cha hayo yote. Hivyo usilalamike. Tuungane pamoja ili kutafuta namna bora ya kuiondoa madarakani.
Suppose ni kweli kwa uwezo wa Mungu, Watanzania wanai vote out CCM, halafu nafasi ya iliyokuwa CCM ndio mmampa nani?. Au kwa lugha rahisi, ili CCM iondoke, lazima kuwe na mbadala wa CCM!. Mbadala wa CCM ni chama gani?
p
 
Mkuu inawezekana upo sahihi lakini ccm haiwezi kutoka madarakani ukweli ndio huo. Pesa wanayo na uchawi wanao ni ngumu kwa kweli uongo dhambi.
 
Hizo takataka zenu mnazohubiri hapa kila siku kwa kutokubaliana na ukweli kwamba mungu wenu hayupo ndo zinagawa watu sasa!
Hata Hitler alijenga barabara na viwanda lakini alikufa na taifa likaendelea sembuse nyie wanyea kwenye mashimo?
Kwamba kwasababu fulani amefariki basi matatizo yameongezeka huo ni unafiki mkubwa ambao mm naukataa
Mtu ambae hakuajiri watu miaka 6 na kupandisha mishahara anaonekanaje kwamba Ali solve matatizo?
Mtu ambaye alidanganua taifa kwamba anajenga viwanda kumbe uongo hili mbona hamsemi?
Takataka unazifuata? Wewe si ndo takataka?
 
Hakuna mafanikio kama wasimamia katiba ni hawa hawa!
Hata katiba iliyopo hakuna mahali imeruhusu wizi wa mali za umma,hakuna mahali imeruhusu ubadhirifu na ufisadi.
Tatizo liko kwa wasimamia sheria,hasa pale mtu kama raisi anapotoa kauli tata za "kila mtu ale urefu wa kamba yake"

Katiba mpya ni takwa kuu la wanasiasa na sio hitaji kuu la wananchi.

Katiba mpya inayotafutqa ni ile itakayompunguzia rais madaraka!

Na wapinzani wengi wanaitaka hiyo kwa kuhisi huenda ikawapa upenyo na wao kuingia kuikomba hazina ya nchi.

Wanasisasa wa kiafrika ni wabaya kuliko hata majambazi wa silaha,maana hawana huruma nawananch maskini bali wamejaa ubinafsi na kuwaona wananchi kama misukule yao.

Kenya wamebadili katiba mara kadhaa na bado haijawaridhisha wanasiasa mpaka sasa wanalilia mabadiliko mengine kupitia BBI.

Mimi ni mwananchi ninayejitambua na kufuatilia mambo kwa kina!
Sifuati upepo wala kusulumwa na tamaa!
Unakaza fuvu alafu unalia lia.Inaonekana kinachokuuma wewe ni magufuli sio nchi kuharibika.ungekua unaumizwa na nchi ungeona umuhimu wa katiba mpya.utalalamika sana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Mimi nadhani tutetee wananchi bila kulinganisha Awamu za utawala wa CCM .

CCCCCM ni Ile Ile, japo nakubaliana na mwandishi kuwa upinzani wa Kweli utatoka CCM.

Itoshe kusema kuwa Hali ya wananchi ni ngumu, Bei za Bidhaa zipo juu,nk nk.

Tukifika hapo tutaweza kukwepa propaganda za kuacha kushughulika na hoja za wananchi wakijificha kwenye kichaka Cha mapungufu ya Magu.
Mkuu, hapo ulipo andika kuwa "upinzani wa kweli na wenye nguvu utatoka CCM" umekosea sana., yaani hii CCM ya sasa hivi imejivua gamba kwa mantiki hiyo inajijua yenyewe.
.
 
Takataka unazifuata? Wewe si ndo takataka?
Shida yenu nyie mmezoea kudanganywa raisi anajenga madarasa mikoani, maji yanatoka, umeme upo kila ukiamka oh miradi imesimama oh sijui nn? Mkijibiwa mmnakimbilia ushoga na ujinga ujinga na ushamba wa kisukuma hapa!
Kosa la wale wahariri ni nini mpaka mkaanza kuwatukana na kuwazushia wazee wa watu?.?.
 
Ulianza vizuri ukaharibu ulipoanza kumtetea mwizi, fisadi, muuaji katili, dikteta na mwehu Magufuli
mliokuwa na vyeti feki,wapigaji,mafisadi na wavivu kazini ndo mtazamo wenu huo.
 
Suppose ni kweli kwa uwezo wa Mungu, Watanzania wanai vote out CCM, halafu nafasi ya iliyokuwa CCM ndio mmampa nani?. Au kwa lugha rahisi, ili CCM iondoke, lazima kuwe na mbadala wa CCM!. Mbadala wa CCM ni chama gani?
p
Ikitoka ccm, kuundwe serikali ya mseto kwa kuchagua watu makini kutoka vyama tofauti. Na baada ya muda fulani, itengenezwe Katiba yenye maslahi na Taifa.

NB: Hofu yangu ni moja tu; wanasiasa ni vigeugeu, wanafiki, wabinafsi, na hawaaminiki. Wakionja tu utamu wa madaraka, na wenyewe wanageuka kuwa kama wale waliopita.

Na tatizo hili ni sugu kwenye nchi zetu nyingi za Kiafrika. Mifano ni mingi sana. Kuanzia Afrika ya Kusini na ANC yao, Uganda na Museven, Senegal na Mark Sally, Ivory Coast na Ouwattara, nk.
 
Shida yenu nyie mmezoea kudanganywa raisi anajenga madarasa mikoani, maji yanatoka, umeme upo kila ukiamka oh miradi imesimama oh sijui nn? Mkijibiwa mmnakimbilia ushoga na ujinga ujinga na ushamba wa kisukuma hapa!
Kosa la wale wahariri ni nini mpaka mkaanza kuwatukana na kuwazushia wazee wa watu?.?.
Ushamba awe nao msukuma, halafu mwenye kumsumbua ni Wewe! Huo si ni upumbavu!
 
Back
Top Bottom