dolevaby
JF-Expert Member
- Aug 25, 2013
- 12,956
- 9,482
Sema mimi nataka katiba mpya. Ukisema watu wanaweza wakawa laki moja wakati watanzania ni milioni kadhaaTunataka Katiba Mpya ya Wananchi
Mkuu hakuna watu mambumbumbu kama watz..hawaelewek wanataka nn wanapenda nini yaani yapo yapo tuu!Nashindwa hata kuelewa kama ni kudeka au ni kutaka kudeka... kabla ya Rais Magufuli watu walilalamika sana na kutaka Rais mkali asiyecheka cheka, na mtu ambaye aliwaambia mapema kabisa kuwa yeye akiwa Rais watu "watalimia meno". Watu walishangalia na kutabasamu wakidhani aliwatania wakati hakuwahi kuwa na rekodi ya utani utani hivi. Watu waliomjua Magufuli waliombea aje awe Rais na wengine walidhania labda akiwa Rais atakuwa tofauti; well hakuwa na zaidi akawa mkali kuliko watu walivyomdhania. Wakaanza kulia...
Labda sala zao zilijibiwa Rais Magufuli akafariki akaja "Mama". Mama ambaye wengine walikuwa wanaombea kila kukicha aje kuwa Rais. Akawa Rais na mara vigelegele vya shangwe vikaibuka "mama mama". WEngine wakajikuta wanaimba kama Christian Bella "Nani kama mama". Wengine wakasema "mama tugombeze tu lakini tupe na soda kidogo"! Wengine wakasema baada ya mama kutengua watu fulani "mama umekunywa chai?" Yaani, mama hakuwa na kosa na asingeweza kuwaudhi. Kila kitu ikawa "ametufuta machozi" mara "sura zinatabasamu" mara "fedha imeanza kuingia mitaani" mara "mwendazake kaenda na yake". Wengine tunawaangalia tu...
Nilisema wakati ule "taifa liko salama" na sikuwa na shaka kuwa ajenda inayoendelea kutekelezwa ni ile ile ya Magufuli; watu wakanijia juu; nikawaangalia nikasema watu wanakumbukumbu ndogo. Watu wengine wakawa wanazungumza (na wengine wanaendelea kuzungumza) kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi akiwa amebeba ajenda ya Upinzani. Mara mambo ya Katiba Mpya yakafutika; mara wakamwona kawageuka. Wengine walidhania sasa kila kitu kiko kama zamani; watu wakalijaribu zari; wakambeep mama na kuwa wamesahau kabisa aliwaambia "ukinizingua na mimi nitakuzingua"!
Sasa hata miezi haijaisha watu wamegeuka kabisa; sasa mama "anahujumiwa" mara "mama siyo Rais" kuna watu nyuma yake. Wanamkumbusha kuwa yeye ni Rais kamili; wakati yeye mwenyewe aliwaambia ni Rais kamili. Kwa maneno mengine hakuna kinachotokea nje yake. Kama Rais Magufuli alibebeshwa kila kinachofanyika nchi nzima ndugu zetu wanataka kumnyima Rais Samia haki hiyo hiyo! Ndani yake kuna dharau fulani hivi na kebeji; kwamba kwa vile ni mwanamke basi hawezi kuwa mkali na kufanya vitu vinavyoonekana vya ukali; wanaona mama mpole mbona kawa mkali!
Unaweza kuona ni kudeka fulani hivi tulikokuwa tunataka.. watu wanataka wadeke; wasifokewefokewe... na mama wala hafoki.. lakini watu hawadeki sana... watu wanataka wasinuniwenuniwe, hawataki wasemwesemwe (wengine wakisemwa wanaweza kuanguka kama yule jamaa yake Jaffo).
Sijui wanataka nini; tuache ufyatu... ulichopewa ndicho ulichonacho...
Hata tukiwa wawili "Tunataka" ni sahihi, "nataka" sio sahihi.Sema mimi nataka katiba mpya. Ukisema watu wanaweza wakawa laki moja wakati watanzania ni milioni kadhaa
Watu wanaongea hoja ila wewe unaleta vihoja!Kwanini wanaccm mnatelekezwa halafu mamluki wanapewa vyeo ? mjitathmin sana vinginevyo mtabaki kupiga deki tu
Hayo yanatokea kwenye utawala upi?Tozo na miamala unaijua wewe?
Uonevu wa jeshi la polisi dhidi ya wapinzani huuoni?
Bidhaa muhimu kupanda bei unakujua wewe?
Hatutaki tabasamu au hasira ya mtu tunataka atawale kwa mujibu wa sheria nothing more
Ndio maana mimi huwa nasema ukipata nafasi piga hela ondoka!Mkuu hakuna watu mambumbumbu kama watz..hawaelewek wanataka nn wanapenda nini yaani yapo yapo tuu!