Tuache Ufyatu: Ni Kama Bado Tunadeka...

Katiba Mpya itafanya nini na kwanini unafikiri CCM ina maslahi ya kuwa na Katiba Mpya? Wameweza kutawala kwa miaka sitini hivi kwanini leo waamue kuja na Katiba Mpya kabisa?
Hiyo katiba mpya itakayoweka tume huru ya uchaguzi ndio itamaliza hilo swali lako la Watanzania kwa wingi wao wanataka nini.
Kwa sasa unawalaumu bure tu na swali lako halina mashiko kwa sababu hakuna uhakika kama sanduku la kura au deep state ndio waamuzi wa nani awe nani.
 
Mbona kuna checks and balances...
Mwenyekiti wa CCM anaweza kumuondoa spika wa bunge au mbunge yoyote wa chama chake bungeni.

Rais anateua jaji mkuu, jaji Kiongozi, DPP na majaji wa mahakama zote bila uthibitisho wa bunge.

Rais anateua katibu wa bunge.

Rais anateua wakuu wote wa mikoa na wilaya.

Rais anaweza kulivunja bunge

Endelea...
 
Kwanini wanaccm mnatelekezwa halafu mamluki wanapewa vyeo ? mjitathmin sana vinginevyo mtabaki kupiga deki tu
Mimi sihitaji cheo chochote mkuu, tatizo linakuja hao wapinzani fake wanaopiganiwa na watu mwisho wa siku wanahamia CCM ili kutetea ubunge wao! Thats stupid, sitokuja kupoteza muda wangu kumsapoti mpinzani yeyote TZ! Huyo Lema anaita wenzake waoga huko Twitter wakati yeye kakimbia nchi!!!! Kwa sasa ni kumpata mtu muadilifu ndani ya CCM atuongoze, na tunaye Samia
 
  • Thanks
Reactions: Ame
UPUUZI MTUPU!

Nashindwa hata kuelewa kama ni kudeka au ni kutaka kudeka... kabla ya Rais Magufuli watu walilalamika sana na kutaka Rais mkali asiyecheka cheka, na mtu ambaye aliwaambia mapema kabisa kuwa yeye akiwa Rais watu "watalimia meno". Watu walishangalia na kutabasamu wakidhani aliwatania wakati hakuwahi kuwa na rekodi ya utani utani hivi. Watu waliomjua Magufuli waliombea aje awe Rais na wengine walidhania labda akiwa Rais atakuwa tofauti; well hakuwa na zaidi akawa mkali kuliko watu walivyomdhania. Wakaanza kulia...

Labda sala zao zilijibiwa Rais Magufuli akafariki akaja "Mama". Mama ambaye wengine walikuwa wanaombea kila kukicha aje kuwa Rais. Akawa Rais na mara vigelegele vya shangwe vikaibuka "mama mama". WEngine wakajikuta wanaimba kama Christian Bella "Nani kama mama". Wengine wakasema "mama tugombeze tu lakini tupe na soda kidogo"! Wengine wakasema baada ya mama kutengua watu fulani "mama umekunywa chai?" Yaani, mama hakuwa na kosa na asingeweza kuwaudhi. Kila kitu ikawa "ametufuta machozi" mara "sura zinatabasamu" mara "fedha imeanza kuingia mitaani" mara "mwendazake kaenda na yake". Wengine tunawaangalia tu...

Nilisema wakati ule "taifa liko salama" na sikuwa na shaka kuwa ajenda inayoendelea kutekelezwa ni ile ile ya Magufuli; watu wakanijia juu; nikawaangalia nikasema watu wanakumbukumbu ndogo. Watu wengine wakawa wanazungumza (na wengine wanaendelea kuzungumza) kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi akiwa amebeba ajenda ya Upinzani. Mara mambo ya Katiba Mpya yakafutika; mara wakamwona kawageuka. Wengine walidhania sasa kila kitu kiko kama zamani; watu wakalijaribu zari; wakambeep mama na kuwa wamesahau kabisa aliwaambia "ukinizingua na mimi nitakuzingua"!

Sasa hata miezi haijaisha watu wamegeuka kabisa; sasa mama "anahujumiwa" mara "mama siyo Rais" kuna watu nyuma yake. Wanamkumbusha kuwa yeye ni Rais kamili; wakati yeye mwenyewe aliwaambia ni Rais kamili. Kwa maneno mengine hakuna kinachotokea nje yake. Kama Rais Magufuli alibebeshwa kila kinachofanyika nchi nzima ndugu zetu wanataka kumnyima Rais Samia haki hiyo hiyo! Ndani yake kuna dharau fulani hivi na kebeji; kwamba kwa vile ni mwanamke basi hawezi kuwa mkali na kufanya vitu vinavyoonekana vya ukali; wanaona mama mpole mbona kawa mkali!

Unaweza kuona ni kudeka fulani hivi tulikokuwa tunataka.. watu wanataka wadeke; wasifokewefokewe... na mama wala hafoki.. lakini watu hawadeki sana... watu wanataka wasinuniwenuniwe, hawataki wasemwesemwe (wengine wakisemwa wanaweza kuanguka kama yule jamaa yake Jaffo).

Sijui wanataka nini; tuache ufyatu... ulichopewa ndicho ulichonacho...
 
Mwenyekiti wa CCM anaweza kumuondoa spika wa bunge au mbunge yoyote wa chama chake bungeni.

Rais anateua jaji mkuu, jaji Kiongozi, DPP na majaji wa mahakama zote bila uthibitisho wa bunge.

Rais anateua katibu wa bunge.

Rais anateua wakuu wote wa mikoa na wilaya.

Rais anaweza kulivunja bunge

Endelea...
Acha kunyooshea wengine vidole, huko ulipo kupo salama Mr. yoda?
 
Katiba Mpya itafanya nini na kwanini unafikiri CCM ina maslahi ya kuwa na Katiba Mpya? Wameweza kutawala kwa miaka sitini hivi kwanini leo waamue kuja na Katiba Mpya kabisa?

Mkuu

Labda tu waulize

wanataka rasimu ipi ya katiba?

Ile ya CCM iliyoua UJAMAA..?

Rasimu ya Warioba inayonyima CCM USHINDI?

Rasimu ya Samwel 6.......

Shukrani
 
Nashindwa hata kuelewa kama ni kudeka au ni kutaka kudeka... kabla ya Rais Magufuli watu walilalamika sana na kutaka Rais mkali asiyecheka cheka, na mtu ambaye aliwaambia mapema kabisa kuwa yeye akiwa Rais watu "watalimia meno". Watu walishangalia na kutabasamu wakidhani aliwatania wakati hakuwahi kuwa na rekodi ya utani utani hivi. Watu waliomjua Magufuli waliombea aje awe Rais na wengine walidhania labda akiwa Rais atakuwa tofauti; well hakuwa na zaidi akawa mkali kuliko watu walivyomdhania. Wakaanza kulia...

Labda sala zao zilijibiwa Rais Magufuli akafariki akaja "Mama". Mama ambaye wengine walikuwa wanaombea kila kukicha aje kuwa Rais. Akawa Rais na mara vigelegele vya shangwe vikaibuka "mama mama". WEngine wakajikuta wanaimba kama Christian Bella "Nani kama mama". Wengine wakasema "mama tugombeze tu lakini tupe na soda kidogo"! Wengine wakasema baada ya mama kutengua watu fulani "mama umekunywa chai?" Yaani, mama hakuwa na kosa na asingeweza kuwaudhi. Kila kitu ikawa "ametufuta machozi" mara "sura zinatabasamu" mara "fedha imeanza kuingia mitaani" mara "mwendazake kaenda na yake". Wengine tunawaangalia tu...

Nilisema wakati ule "taifa liko salama" na sikuwa na shaka kuwa ajenda inayoendelea kutekelezwa ni ile ile ya Magufuli; watu wakanijia juu; nikawaangalia nikasema watu wanakumbukumbu ndogo. Watu wengine wakawa wanazungumza (na wengine wanaendelea kuzungumza) kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi akiwa amebeba ajenda ya Upinzani. Mara mambo ya Katiba Mpya yakafutika; mara wakamwona kawageuka. Wengine walidhania sasa kila kitu kiko kama zamani; watu wakalijaribu zari; wakambeep mama na kuwa wamesahau kabisa aliwaambia "ukinizingua na mimi nitakuzingua"!

Sasa hata miezi haijaisha watu wamegeuka kabisa; sasa mama "anahujumiwa" mara "mama siyo Rais" kuna watu nyuma yake. Wanamkumbusha kuwa yeye ni Rais kamili; wakati yeye mwenyewe aliwaambia ni Rais kamili. Kwa maneno mengine hakuna kinachotokea nje yake. Kama Rais Magufuli alibebeshwa kila kinachofanyika nchi nzima ndugu zetu wanataka kumnyima Rais Samia haki hiyo hiyo! Ndani yake kuna dharau fulani hivi na kebeji; kwamba kwa vile ni mwanamke basi hawezi kuwa mkali na kufanya vitu vinavyoonekana vya ukali; wanaona mama mpole mbona kawa mkali!

Unaweza kuona ni kudeka fulani hivi tulikokuwa tunataka.. watu wanataka wadeke; wasifokewefokewe... na mama wala hafoki.. lakini watu hawadeki sana... watu wanataka wasinuniwenuniwe, hawataki wasemwesemwe (wengine wakisemwa wanaweza kuanguka kama yule jamaa yake Jaffo).

Sijui wanataka nini; tuache ufyatu... ulichopewa ndicho ulichonacho...
Wewe jamaa sijui ni uzee au ndio uwezo umeporomoka. Aiseee
 
Mchumi Dr Blasius Kahyoza amechambua uhitaji na umuhimu wa katiba mpya kwa kigezo cha uchumi, mambo muhimu katika mtazamo wake ni;

Moja, Hoja ya gharama kubwa kutengeneza katiba mpya ni ukosefu wa uelewa kwa sababu wanaosema hivyo hawatazami faida kubwa za mbeleni za jinsi katiba mpya itakayotoa uhuru mkubwa wa haki za kiuchumi itakavyongeza pato la nchi kama sio kwao kwa watoto wao na vizazi vijavyo. Hivyo hakuna gharama yoyote inayoweza kuwa kigezo cha kuikaata katiba mpya kwa sababu faida zinazidi gharama yoyote.

Mbili, Si rahisi kwa uchumi wa nchi yetu kuwa imara na endelevu bila katiba mpya iliyo imara kwa sababu misingi ya uchumi huwa inategemea sana miondombinu ya kujitawala ambayo huwa inasimikwa na katiba. Anasema ukiacha nchi zenye utajiri mkubwa wa mafuta historia inaonyesha wazi nchi nyingine zote zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kwa haraka zilitanguliwa na mageuzi makubwa ya miondombinu ya tawala zao kupita Katiba.

Tatu, Wanaosema tujenge kwanza uchumi kisha katiba ije baadaye wanasahau taifa hili limeujenga uchumi huo wanaouzungumzia kwa miaka 60 sasa na limefanya kila kitu isipokuwa kubadilisha katiba ili kufikia hayo maendeleo makubwa linalotamani kuyafikia.

Dkt. Kahyoza anauliza Kama tumefanya kila jambo tulillofikiri ni muhimu kupata maendeleo makubwa na bado imeshindikana busara za kawaida si zingesema tufanye jambo lingine ambalo hatujawahi kulijaribu pamoja na kuzungumzwa sana na wengi amabalo ni kufanya mageuzi makubwa ya miondombinu ya utawala wetu kwa kubadilisha katiba yetu?
Ukitaka kupata kitu ambacho hujawahi kukipata lazima ufanye kitu ambacho hujawahi kukifanya.
 
Kifupi hawajui wanachotaka.....

Hizi tabia zao zimenifanyi niamini JPM alifaa kuiongoza hii nchi hata miaka 50 ndio vile tu mapenzi ya Mungu....kifupi tunahitaji Rais mtemi
mndava na katili ili akili zikae sawa kidogo..
 
Toka mwanzo nilitamani mama awe mkali, hata ikiwezekana kuliko Magufuli, maana nilijua kuna watu watam-look down. Watu walidhani kwa kuwa ni mwanamke basi hawezi kuwa steong na mwenye misimamo imara, imekula kwao.
Waliokuwa wanaimba 'mama anaupiga mwingi' ndiyo hao hao sasa wanalia kilio cha mbwa, midomo juu kwa sababu walijiaminisha mama ni dhaifu kwa hiyo wakadeka.
Way to go mama, simamia unachokiamini 💪🏿
 
Back
Top Bottom