Tuache Ufyatu: Ni Kama Bado Tunadeka...

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Nashindwa hata kuelewa kama ni kudeka au ni kutaka kudeka... kabla ya Rais Magufuli watu walilalamika sana na kutaka Rais mkali asiyecheka cheka, na mtu ambaye aliwaambia mapema kabisa kuwa yeye akiwa Rais watu "watalimia meno". Watu walishangalia na kutabasamu wakidhani aliwatania wakati hakuwahi kuwa na rekodi ya utani utani hivi. Watu waliomjua Magufuli waliombea aje awe Rais na wengine walidhania labda akiwa Rais atakuwa tofauti; well hakuwa na zaidi akawa mkali kuliko watu walivyomdhania. Wakaanza kulia...

Labda sala zao zilijibiwa Rais Magufuli akafariki akaja "Mama". Mama ambaye wengine walikuwa wanaombea kila kukicha aje kuwa Rais. Akawa Rais na mara vigelegele vya shangwe vikaibuka "mama mama". WEngine wakajikuta wanaimba kama Christian Bella "Nani kama mama". Wengine wakasema "mama tugombeze tu lakini tupe na soda kidogo"! Wengine wakasema baada ya mama kutengua watu fulani "mama umekunywa chai?" Yaani, mama hakuwa na kosa na asingeweza kuwaudhi. Kila kitu ikawa "ametufuta machozi" mara "sura zinatabasamu" mara "fedha imeanza kuingia mitaani" mara "mwendazake kaenda na yake". Wengine tunawaangalia tu...

Nilisema wakati ule "taifa liko salama" na sikuwa na shaka kuwa ajenda inayoendelea kutekelezwa ni ile ile ya Magufuli; watu wakanijia juu; nikawaangalia nikasema watu wanakumbukumbu ndogo. Watu wengine wakawa wanazungumza (na wengine wanaendelea kuzungumza) kana kwamba Rais Samia alishinda uchaguzi akiwa amebeba ajenda ya Upinzani. Mara mambo ya Katiba Mpya yakafutika; mara wakamwona kawageuka. Wengine walidhania sasa kila kitu kiko kama zamani; watu wakalijaribu zari; wakambeep mama na kuwa wamesahau kabisa aliwaambia "ukinizingua na mimi nitakuzingua"!

Sasa hata miezi haijaisha watu wamegeuka kabisa; sasa mama "anahujumiwa" mara "mama siyo Rais" kuna watu nyuma yake. Wanamkumbusha kuwa yeye ni Rais kamili; wakati yeye mwenyewe aliwaambia ni Rais kamili. Kwa maneno mengine hakuna kinachotokea nje yake. Kama Rais Magufuli alibebeshwa kila kinachofanyika nchi nzima ndugu zetu wanataka kumnyima Rais Samia haki hiyo hiyo! Ndani yake kuna dharau fulani hivi na kebeji; kwamba kwa vile ni mwanamke basi hawezi kuwa mkali na kufanya vitu vinavyoonekana vya ukali; wanaona mama mpole mbona kawa mkali!

Unaweza kuona ni kudeka fulani hivi tulikokuwa tunataka.. watu wanataka wadeke; wasifokewefokewe... na mama wala hafoki.. lakini watu hawadeki sana... watu wanataka wasinuniwenuniwe, hawataki wasemwesemwe (wengine wakisemwa wanaweza kuanguka kama yule jamaa yake Jaffo).

Sijui wanataka nini; tuache ufyatu... ulichopewa ndicho ulichonacho...
 
Tumefanya kila kitu kama taifa, tumetaka Marais wakali na Wapole na wote tumewapata ila mambo hayabadiliki sana. Tunatakiwa tufanye mabadiliko makubwa ya miondombinu ya kujitawala, nayo ni Kuandika KATIBA MPYA ilyo bora kwa mustakbali mwema wa taifa letu.
 
Mchumi Dr Blasius Kahyoza amechambua uhitaji na umuhimu wa katiba mpya kwa kigezo cha uchumi, mambo muhimu katika mtazamo wake ni;

Moja, Hoja ya gharama kubwa kutengeneza katiba mpya ni ukosefu wa uelewa kwa sababu wanaosema hivyo hawatazami faida kubwa za mbeleni za jinsi katiba mpya itakayotoa uhuru mkubwa wa haki za kiuchumi itakavyongeza pato la nchi kama sio kwao kwa watoto wao na vizazi vijavyo. Hivyo hakuna gharama yoyote inayoweza kuwa kigezo cha kuikaata katiba mpya kwa sababu faida zinazidi gharama yoyote.

Mbili, Si rahisi kwa uchumi wa nchi yetu kuwa imara na endelevu bila katiba mpya iliyo imara kwa sababu misingi ya uchumi huwa inategemea sana miondombinu ya kujitawala ambayo huwa inasimikwa na katiba. Anasema ukiacha nchi zenye utajiri mkubwa wa mafuta historia inaonyesha wazi nchi nyingine zote zilizopiga hatua kubwa kimaendeleo kwa haraka zilitanguliwa na mageuzi makubwa ya miondombinu ya tawala zao kupita Katiba.

Tatu, Wanaosema tujenge kwanza uchumi kisha katiba ije baadaye wanasahau taifa hili limeujenga uchumi huo wanaouzungumzia kwa miaka 60 sasa na limefanya kila kitu isipokuwa kubadilisha katiba ili kufikia hayo maendeleo makubwa linalotamani kuyafikia.

Dkt. Kahyoza anauliza Kama tumefanya kila jambo tulillofikiri ni muhimu kupata maendeleo makubwa na bado imeshindikana busara za kawaida si zingesema tufanye jambo lingine ambalo hatujawahi kulijaribu pamoja na kuzungumzwa sana na wengi amabalo ni kufanya mageuzi makubwa ya miondombinu ya utawala wetu kwa kubadilisha katiba yetu?
 
Tumefanya kila kitu kama taifa, tumetaka Marais wakali na Wapole na wote tumewapata ila mambo hayabadiliki sana. Tunatakiwa tufanye mabadiliko makubwa ya miondombinu ya kujitawala, nayo ni Kuandika KATIBA MPYA ilyo bora kwa mustakbali mwema wa taifa letu.
Tatizo siyo katiba mpya, tatizo ni upinzani fake tulionao, leo hii Mdee aliyepiganiwa na kuaminiwa kila kona yupo wapi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom