Tuache siasa kwenye ujenzi: Majibu ya nyufa hizi, yatolewe na The Professionals, AQRB, ERB, CRB, na sio mtuhumiwa TBA!

Wanabodi,
Baada ya kuthibitishwa hizi nyufa ni za kweli kwenye hostel za UDSM, TBA imetoa ufafanuzi nyufa hizi kitu cha kawaida, hivyo wananchi tusiwe na wasiwasi.

Nimekuwa inspired kupandisha uzi huu, kwa bandiko hili TBA yakiri kubomoka kwa mabweni ya UDSM, yatoa sababu zake

Kwa vile sisi sii wataalamu, TBA ndio wataalamu, kunapotokea tuhumu kama hizi, na mtuhumiwa ni TBA kuwa amejenga chini ya kiwango, au amelipua, then mtu sahihi wa kusema nyufa hizo ni kawaida sio mtuhumiwa TBA, bali sasa, the assurances kuwa all is well, nyufa hizo ni kitu cha kawaida, utolewe na the professionals kuanzia kwa Bodi ya AQRB wathibitishe ile bilioni 10 inaweza kujenga majengo hayo na yakawa madhubuti, ERB wawathibitishe TBA waliwatumia watu sahihi, na CRB wathibitishe walikagua ujenzi step by step na kujiridhisha, ndipo TBA waruhusiwe kuziba nyufa hizo, vinginevyo sio tusipoziba ufa, tutatenga ukuta, tunaweza kuja kujenga ukuta wa damu!.

Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tuache kuingiza siasa kwenye kila kitu!, ujenzi wa majengo hayo uligubikwa na siasa nyingi, ili kukidhi matakwa ya kisiasa, yametumia gharama ndogo za ajabu, ili kuonyesha jinsi tunavyoibiwa kwenye ujenzi.

Tufanyeni siasa kwenye siasa, lakini tusiingize siasa kwenye kazi za watu just for the sake of political capitalization, hatma ya hizi hostels, utatoa funzo moja zuri sana kuhusu kuingiza siasa kwenye ujenzi.
Sometimes cheap is expensive, huu ni ufa tuu, ila ulivyo mkubwa, hii ni dalili hapa mbele ya safari tutakuja kujenga ukuta, hala hala tuu, usiwe ukuta wa damu!.
Paskali
Watoe Majibu ni Kodi Zetu hizo je nani atagharamia
 
Nilitegemea watafuta kiki kama waziri wa ardhi angefanya ziara ya kushtukiza leo,nahic kagundua km baba j..ca ndo muhusika no moja kauchuna
 
Rekebisha kwenye aya ya mwisho neno "Professionalism" na kuweka "profession za watu" pia wewe ni mwandishi mkubwa sitegemei makosa ya kiingereza kama haya
English men are also victims of their own language.characteristics of languages one is lernability .There fore spelling and grammar people have to learn , even in kiswahili. Acha ushamba angalia CONTENT
 
Wala haihitajiki PhD kujua kuwa kuna tatizo nyumba yako inapopata ufa. Ni mjinga tu atadharau ufa. Na ndio maana tuna methali: usipoziba ufa, utajenga ukuta. Hii methali ilitoka kwa wahenga wasiokuwa mainjinia.
 
Paskali huwanasoma uandishi wako humu kwa mada tofauti tofauti, lakini hapa naona unaisemea serikali. Hii kazi ina mtu wake serikalini. Minadhani ingekuwa busara kwa nafasi yako ukawa unamuuliza huyo Dr.Abbas ni nini serikali inasema kuhusiana na swala fulani, halafu ukatuletea majibu yao, badala ya wewe kutolea ufafanuzi na kuleta fikra zako kwenye issue za serikali. Unayo haki kuhoji lakini sio kutoa majibu yao au kwa niaba yao.
Ni kweli, yeye kwa nafasi yake angetakiwa awafwate huko akawaulize wamweleweshe alafu aje atuelezee
 
Nilimtukana sana fundi wangu baada ya kukuta hali hii kwenye banda langu. Leo kanipigia simu karudisha matusi yote, ni baada ya kusikia kauli ya mhandisi kuhusu nyufa za mabweni kua ni kawaida
 
TBA wanasema ni nyufa, ni kweli zipo na zina sababu ya kuwepo hapo!! DARUSO wamekuja na jipya, wanasema ni maungio ya majengo! Duh

KUHUSU TAARIFA ZA MAJENGO MAPYA YA MAGUFULI

Daruso tumefuatilia kwa karibu zaidi kujiridhisha juu ya picha zilizosambazwa kama mipasuko ya mabweni (hostels)mpya yaliyojengwa na udhamini wa Rais wa Tanzania DK.John Pombe Joseph Magufuli katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Yale ni majengo ambayo yamejengwa ukiyaona unaweza ukadhani ni jengo moja Lakini ukweli yanasehemu ambayo yanatenganishwa(separation points) amabayo ndiyo iliyo pigwa picha kama mpasuko (cracks) baada ya ubao uliokuwa umewekwa pale kuondolewa,na kulifanyika kitu tunachokiita kuongeza ukubwa wa uwazi huo kwa njia ya ku "ZOOM " na hivyo kuupotosha umma

Kamati imeundwa nadhani itatoa ripoti ya kitaalamu kuhusu Hilo Lakini kwa ujumla kutoka kwa meneja wa magufuli hostel,wahandisi wa chuo kikuu,wahandisi wa Project hio na sisi wenyewe kama viongozi wa Daruso ambao hatuwezi kukubali watu wetu wakae sehemu ambayo sio salama tumejiridhisha pasi na shaka Kuwa hakuna tishio la kiusalama kwa wakazi wa mabweni hayo kama ambavyo watu wanajaribu kutaka kuuaminisha umma.

Kama Daruso hatuwezi kamwe Kuwa sehemu ya kuunga mkono watu ambao wamekuwa wakipinga ujenzi wa hio project ya hostel hizi Kama mtaji wao wa kisiasa hostel hizi zinabeba watu 3840 ikiwa Ni idadi kubwa kuliko watu wanaokaa main Campus,Kwani wakati ambao sisi tumejengewa mabweni haya Ni Wajibu wetu kama jumuiya ya Chuo kikuu cha Dar es salaam Kama kweli sisi ni waungwana kushukuru kwa Ujenzi huo Kwani Mhe Rais Angeweza kujenga sehemu zingine Lakini akaamua kujenga kwetu na sio kila kitu Ni siasa Kwani kwa ujenzi huo Mhe Rais amegusa Maisha ya wanafunzi na wazazi kwa ujumla wake Kwani wazazi walitakiwa kuhakikisha watoto wao wanawatafutia sehemu za kukaa.

Mwisho nitoe rai kwa wana Daruso kufuata kanuni,taratibu,sheria na miongozo ya chuo kikuu cha Dar es salaam pale ambapo wamebaini kuna Mambo yanahitaji kutatuliwa Kwani sheria ziko wazi kuhusu nani Ana mamlaka ya kuzungumza juu ya mambo ya chuo na si kila mtu anaweza akazunhumza anachojisikia kwa niaba ya Taasisi hii.

Ukizingatia taasisi za Elimu Ni miongoni mwa taasisi zinazohitaji amani na utulivu (peace and tranquility) kwa Kiwango kikubwa kama mazingira rafiki kwa wanafunzi kupata Elimu Yao,hivyo Ni waombe ridhi wote walioshitushwa na taarifa hiyo.

Mungu Ibariki Africa,Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Daruso

Na
Rais wa Daruso Ndugu Jeremiah John Jilili
0687548035
Eti hawa ndo wasomi wa UDSM .. huyu rais ameaibisha UDSM
 
Back
Top Bottom