Tuache siasa kwenye ujenzi: Majibu ya nyufa hizi, yatolewe na The Professionals, AQRB, ERB, CRB, na sio mtuhumiwa TBA!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
37,969
2,000
Wanabodi,
Baada ya kuthibitishwa hizi nyufa ni za kweli kwenye hostel za UDSM, TBA imetoa ufafanuzi nyufa hizi kitu cha kawaida, hivyo wananchi tusiwe na wasiwasi.

Nimekuwa inspired kupandisha uzi huu, kwa bandiko hili TBA yakiri kubomoka kwa mabweni ya UDSM, yatoa sababu zake
TBA yakiri kubomoka kwa mabweni
Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo nchini Mhandisi Elius A. Mwakalinga, amekiri picha zinazosambaa mitandaoni zikionyesha majengo mapya ya mabweni ya UDSM yana nyufa ni za majengo hayo, huku akisema ni kitu cha kawaida kwa majengo makubwa.Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Mwakalinga amesema kutokea kwa nyufa hizo ni moja ya hatua za 'expansion joint' ambazo hutumiwa kwenye ujenzi wa majengo, lakini majengo hayo yamekidhi vigezo vyote na vipimo wakati wa ujenzi wake.

"Kila design tunayofanya ya majengo sasa hivi tunatumia expansion joint, majengo mengi makubwa huwa inatumia hiyo, hivyo ni common na sio creck kubwa sana kama inavoonekana kwenye picha, nilienda ile jana usiku kukagua tukakuta hiyo hali, ni process za majengo ili yaweze kusatle, hivyo watu wawe na amani kabisa wala wasiwe na hofu", amesema Bwana Mwakalinga.

Mwakalinga ameendelea kwa kusema kwamba watu wanaosambaza picha hizo bila kutaka ufafanuzi kutoka kwake wanafanya makosa kwani wanawatia watu hofu kwa jambo la kawaida kwenye hatua za ujenzi, huku wakilaumu kitu ambacho hawana uhakika nacho.

EATV

View attachment 643893 View attachment 643894


Habari zaidi soma=>

Hosteli za Magufuli chuoni UDSM zimeanza kubomoka. Nini chanzo? Watoto wetu watapona?
Kwa vile sisi sii wataalamu, TBA ndio wataalamu, kunapotokea tuhumu kama hizi, na mtuhumiwa ni TBA kuwa amejenga chini ya kiwango, au amelipua, then mtu sahihi wa kusema nyufa hizo ni kawaida sio mtuhumiwa TBA, bali sasa, the assurances kuwa all is well, nyufa hizo ni kitu cha kawaida, utolewe na the professionals kuanzia kwa Bodi ya AQRB wathibitishe ile bilioni 10 inaweza kujenga majengo hayo na yakawa madhubuti, ERB wawathibitishe TBA waliwatumia watu sahihi, na CRB na mamlaka za ukaguzi wa ubora wa majengo ndio watuthibitishe kuwa walikagua ujenzi step by step na kujiridhisha, ndipo TBA waruhusiwe kuziba nyufa hizo,tena tuombe Mungu, nyufa zenyewe ziishie kwenye kuta tuu, kama kuna nyufa hadi kwenye structural, yatakuwa mengine!, vinginevyo sio tusipoziba ufa, tutatenga tuu ukuta, bali tunaweza kuja kujenga ukuta wa damu!.

Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tuache kuingiza siasa kwenye kila kitu!, ujenzi wa majengo hayo uligubikwa na siasa nyingi, ili kukidhi matakwa ya kisiasa, yametumia gharama ndogo za ajabu, ili kuonyesha jinsi tunavyoibiwa kwenye ujenzi.

Tufanyeni siasa kwenye siasa, lakini tusiingize siasa kwenye kazi za watu just for the sake of political capitalization, hatma ya hizi hostels, utatoa funzo moja zuri sana kuhusu kuingiza siasa kwenye tasnia ya ujenzi.
Sometimes cheap is expensive, huu ni ufa tuu, ila ulivyo mkubwa, hii ni dalili hapa mbele ya safari tutakuja kujenga ukuta, hala hala tuu, usiwe ukuta wa damu!.
Paskali
 

samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
7,814
2,000
Mkuu kwani siasa tumeanza leo au jana..

Hao uliowataja ERG,CRB,AQRB hawana tofauti na hao TBA na hawawezi kuwa na tofauti.

Siku Serikali itakapotenganisha siasa na kazi, siasa na maendelo, CCM na Serikali ndio siku Tanzania itapiga hatua kwenye vitu vingi sana, ila kwa sasa tegemea mkwamo kwenye maeneo mengi sana..
 

Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
9,889
2,000
kaenda jioni tu jana bila kufanya any engineering analysis na anawaambia watu ati hizo ni "nyufa za kawaida tu". Tuache politic kweli. Huenda kitu kipo kinasink slowly. Ndo tabu ya Contractor huyo huyo kujifanyia consultation/supervision. Hakuna checks and balances kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom