Tuache siasa kwenye ujenzi: Majibu ya nyufa hizi, yatolewe na The Professionals, AQRB, ERB, CRB, na sio mtuhumiwa TBA!

Wanabodi,
Baada ya kuthibitishwa hizi nyufa ni za kweli kwenye hostel za UDSM, TBA imetoa ufafanuzi nyufa hizi kitu cha kawaida, hivyo wananchi tusiwe na wasiwasi.

Nimekuwa inspired kupandisha uzi huu, kwa bandiko hili TBA yakiri kubomoka kwa mabweni ya UDSM, yatoa sababu zake

Kwa vile sisi sii wataalamu, TBA ndio wataalamu, kunapotokea tuhumu kama hizi, na mtuhumiwa ni TBA kuwa amejenga chini ya kiwango, au amelipua, then mtu sahihi wa kusema nyufa hizo ni kawaida sio mtuhumiwa TBA, bali sasa, the assurances kuwa all is well, nyufa hizo ni kitu cha kawaida, utolewe na the professionals kuanzia kwa Bodi ya AQRB wathibitishe ile bilioni 10 inaweza kujenga majengo hayo na yakawa madhubuti, ERB wawathibitishe TBA waliwatumia watu sahihi, na CRB na mamlaka za ukaguzi wa ubora wa majengo ndio watuthibitishe kuwa walikagua ujenzi step by step na kujiridhisha, ndipo TBA waruhusiwe kuziba nyufa hizo,tena tuombe Mungu, nyufa zenyewe ziishie kwenye kuta tuu, kama kuna nyufa hadi kwenye structural, yatakuwa mengine!, vinginevyo sio tusipoziba ufa, tutatenga tuu ukuta, bali tunaweza kuja kujenga ukuta wa damu!.

Tanzania ili tupate maendeleo ya kweli, ni lazima tuache kuingiza siasa kwenye kila kitu!, ujenzi wa majengo hayo uligubikwa na siasa nyingi, ili kukidhi matakwa ya kisiasa, yametumia gharama ndogo za ajabu, ili kuonyesha jinsi tunavyoibiwa kwenye ujenzi.

Tufanyeni siasa kwenye siasa, lakini tusiingize siasa kwenye kazi za watu just for the sake of political capitalization, hatma ya hizi hostels, utatoa funzo moja zuri sana kuhusu kuingiza siasa kwenye tasnia ya ujenzi.
Sometimes cheap is expensive, huu ni ufa tuu, ila ulivyo mkubwa, hii ni dalili hapa mbele ya safari tutakuja kujenga ukuta, hala hala tuu, usiwe ukuta wa damu!.
Paskali
Kuna normal settlement na abnormal settlement jumlisha na bearing capacity
 
Rekebisha kwenye aya ya mwisho neno "Professionalism" na kuweka "profession za watu" pia wewe ni mwandishi mkubwa sitegemei makosa ya kiingereza kama haya


Wasomaji tumeielewa hoja ya Paskal,ila kwa kuwa umejikita zaidi katika fani,basi muwekee tu kosa kwenye hilo neno alilokosea,lakini wanajukwaa tumemuelewa, sawa mwalimu?
 
Ni ajabu sana tukio kubwa la kuendeleza taifa letu linalakiwa na chuki na kejeri, kubeza juhudi za serkali. Naam, huu ni upinzani, japo ni kwa nia nzuri. Nalinganisha na taarifa kama ni ya kweli kuwa wanafunzi 400 hapohapo UDSM wamejiungacna CCM kwa kuenzi juhudi za Raisn. Hii kama ni kura naona CCM imeshinda 400-1. Nsenda mbali zaidi kusema kuwa huko nyuma watoto waliosoma na kujaa UDSM walikuwa ni walewale ambao sasa ni wapinzani hawana shukurani. Inaonekana elimu ya bure na sekondari za kata zimewawezesha sehemu watoto wa sehemu zilizoachwa nyuma nazo kuanza kufaidika kielimu. Ingekuwa zamani goli zingekuwa 1-0 yaani wasomi ni hawo hawo upinzani lakini sasa ni 1-400. Tuipongeze serkali kwa juhudi kubwa kueneza elimu. Wapinzani ni kiduchu, minority, warashindwa 42-43 kama udiwani. Wapinazani tuwasikiluze nao lakini tuwadharau. Wasitukatishe tamaa tuachane nao.
Unatumia nguvu nyiingi kuwatetea ccm lakini ungejaribu kutumia akili ungeona hii ni kielelezo hao unao watetea, yaani ccm wamechokwa. Ningekuwa mimi ndio ccm ningefanya kazi na vyama vingine Kama lengo ni kuleta maendeleo kwa wananchi na sio kuwatawala. Ule wakati wa umimi umepitwa na wakati fanyeni kazi pamoja na wapinzani nyie ndiio mko madarakani. Lakini hivi mnavyotaka nyie eti muwaridhishe wananchi kwa kufanya kila kitu nakuhakikishia upinzani uko mioyoni mwao hata mgeweza kumtembeza mungu kwenye gari la wazi Tanzania nzima mkamvisha uniform zenu za ccm zama hizi mgepingwa tu.
 
Back
Top Bottom