Mfalme wa Genge
Senior Member
- Mar 30, 2018
- 190
- 224
Imekuwa ni kawaida sana kwa viongozi wetu wa dini kutuhamasisha kutumia haki zetu kama raia wa Tanzania kushiriki katika chaguzi mbalimbali kuanzia kujiandikisha kupiga kura na hata kuchagua viongozi tunaowataka.
Wakati wa zoezi la kujiandikisha kupiga viongozi hawa wa dini walituhamasisha kwenda kujiandikisha na hatukusikia malalamiko yoyote, lakini leo wanatuhamasisha tena kwenda kuchagua viogozi tunawalaumu.
Makanisa mengi tu yamewakumbusha waumini wao kutumia haki zao kikatiba kuchagua viongozi wao. Ukiangalia kwa umakini unaona hapa ni chuki isiyo na msingi kisa Rais Magufuli ameshiriki ibada katika Kanisa hilo. Wakati huo kuna watu wanatumia mbinu chafu tu ya kutaka kuwagombanisha Wakristo ingawa najua si rahisi kihivyo.
Mwaka 2015 tuliona Wachungaji wa Makanisa mbalimbali wakifanya kampeni za uchaguzi lakini kwa kuwa walikuwa wanapendelea upande wao hatukuwasikia wakipiga kelele na kuwataka Waumini wao kutoshiriki ibada katika makanisa hayo.
Bagonzana Shoo wamekuwa wakiongelea masuala ya kisiasa bila kificho tena yenye maneno ya uchonganishi ndani yake lakini kundi hili linalopiga kelele leo limekuwa likishangilia na kuwaona mashujaa. Sasa leo kauli ya Padri ambaye hata hajaonyesha kupendelea upande wowote zaidi ya kuwahamasisha watu kuchagua viongozi imekuwa tatizo.
Acheni kuwachonganisha Wakristo na viongozi wao wa dini.