Tuache kufurahia mizaha mpaka kwenye mambo Matukufu ya Mungu

Mafurahisha sana nyie watu

Kwahiyo Mungu kashindwa kujitetea hadi mnakuja kulialia huku? Acheni upumbavu

Nasema upumbavu sababu hamjifunzi tu bado mmeendelea kushikilia hizi hekaya
mbona kama unalazimisha mambo mzee, kama ni upumbavu wao kuamini katika Mungu, wewe unakuhangaisha nini huo upumbavu?
 
Itakuwa hujui maana ya tamko mchecheto, hapo ni mja anawaonea huruma waja wenzake,juu ya yale yatakayo wapata kwa dhihaki hiyo.

Wagonjwa wa akili ni nyinyi mnaye mkana msiye mjua. Tafakari utaona uninga wako ulipo.
Acha ujinga! Sasa nisiyemjua kwanini nisimkane ingali simjui?
Siteki kuwa mnafiki kama wewe maana unaonekana unawakana unaowajua na kuwakubali usiowajua
 
Mkuu.. Athiest Ukikaa kiti Cha mbele..tayari kwa mapambano
Ajabu kwa hoja huwa wepesi sana watu hawa.

Hawa wakupigwa makofi. Maana wanahoji juu ya mambo ambayo laiti kama wangejipa muda kidogo tu wakutafakari aisee wangekiri na wasingeuliza maswali ya kipuuzi kama haya. Sasa unakuta mtu anauliza swali la uongo ya kwamba arifisha Mungu ni nini ?
 
Kuna watu sio tu ni waovu, na wakosaji, bali wamevuka hiyo mipaka hadi kufikia hatua ya kuleta mizaha mpaka kwenye mambo matukufu ya Mungu, kudhihaki, kukejeli, kukashfu Neno la Mungu, na wokovu kwa ujumla kwao ni jambo la kawaida.

Watu wanaifanyia biblia comedy kwenye majukwaa na watu wamelipa kiingilio, wameketi pale chini wanacheka na kufurahia.

Biblia ni kitabu cha story za vichekesho? Wanaonekana kwenye tv au youtube.

Na wengine wanatunga hizi memes za status Na wengine wanasambaza. Mambo hayo Ni machukizo.

Sote tunakosea ila Sasa tusifike stage ya kuleta mizaha kwenye mambo matakatifu ili kusudi ufurahishe watu tu.

Mfano Kuna mtu kapost eti "vile umeenda mbinguni halafu umekuta kitabu cha dhambi kimepotea" hiko kibwagizo kina picha Kama watu wanacheka na kufurahia.

Bnafsi naona sio sahihi ni mbinu tu za adui kutusahaulisha mambo ya msingi.
Naonaga munasema eti mambo yenu yapo kiroho zaidi na si kimwili hata mtu akichana Biblia hamna tatizo leo vipi mumekuwa kimwili
 
Acha ujinga! Sasa nisiyemjua kwanini nisimkane ingali simjui?
Ndivyo walikufundisha wakubwa zako ya kuwa usiye mjua ndiyo umkane ? Acheni tu vazi la Ujinga mpambike nalo. Wenzenu huwa wasiyemjua hawamkani mpaka wamjue, yaani wanahoji.

Hivi unapata wapi nguvu ya kukina usicho kijua. Yaani hili hilo linawezekana vipi ? Ndiyo maana kwenu linawezekana sababu akili zenu mbovu.

Kijana jaribu kutafakari.
 
Ajabu kwa hoja huwa wepesi sana watu hawa.

Hawa wakupigwa makofi. Maana wanahoji juu ya mambo ambayo laiti kama wangejipa muda kidogo tu wakutafakari aisee wangekiri na wasingeuliza maswali ya kipuuzi kama haya. Sasa unakuta mtu anauliza swali la uongo ya kwamba arifisha Mungu ni nini ?
Hawa ndo wasiotafakari...Tuwaombee waione Haki na waifuate kabla ya umauti.
 
Siteki kuwa mnafiki kama wewe maana unaonekana unawakana unaowajua na kuwakubali usiowajua
Safi kabisa, kina nani nawajua nawakana na kwa lipi na kina siwajui nawakana ?

Ukithibitisha hili naacha kutumia jf, na wewe utakuwa shahidi namba moja juu ya hili.
 
Tuthibitishie au umejuaje hili ?

Ila sijawahi kuona katika mgongo wa ardhi hii watu wajinga kuwazidi nyinyi.
Ulienda shule kweli?

Nathibitishaje kitu ambacho hakipo. Ingekua hesabu ningeweza kuthibitisha hasi, kwenye probability unaweza kuthibitisha negative, lakini assumption is constant.

Sasa mungu hawajawi kuwepo, hawahi kuonekana, hajawahi kusikkika ukiachia hizi hadithi za wanaoitwa mitume na manabii, unataka nimthibishe?

Hivi ulienda shule kweli ama ndio sampuli ile ile mnaoenda shule kusoma mfaulu mitihani?

Rudi shule uongeze maarifa.
 
2 Wathesalonike 2:1-17

Yule Mtu Wa Kuasi
Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi, msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako.Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa. Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.
Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia. Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa.Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo, na kila aina ya uovu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa. Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo, na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabisa, define Mungu ni nini halafu thibitisha yupo.
 
Hata nikiwa agnostic, hojaji iko palepale na halijajibiwa bado.
Mimi... mapambano na mabishano haya ya Dini YAMENISHINDA....nshachagua njia yangu...Nayo Ni Quran na Sunna za Mtume Mohammed (P.BU.H)
Hapo hakuna atakae nitoaaa
 
We
Kuna watu sio tu ni waovu, na wakosaji, bali wamevuka hiyo mipaka hadi kufikia hatua ya kuleta mizaha mpaka kwenye mambo matukufu ya Mungu, kudhihaki, kukejeli, kukashfu Neno la Mungu, na wokovu kwa ujumla kwao ni jambo la kawaida.

Watu wanaifanyia biblia comedy kwenye majukwaa na watu wamelipa kiingilio, wameketi pale chini wanacheka na kufurahia.

Biblia ni kitabu cha story za vichekesho? Wanaonekana kwenye tv au youtube.

Na wengine wanatunga hizi memes za status Na wengine wanasambaza. Mambo hayo Ni machukizo.

Sote tunakosea ila Sasa tusifike stage ya kuleta mizaha kwenye mambo matakatifu ili kusudi ufurahishe watu tu.

Mfano Kuna mtu kapost eti "vile umeenda mbinguni halafu umekuta kitabu cha dhambi kimepotea" hiko kibwagizo kina picha Kama watu wanacheka na kufurahia.

Bnafsi naona sio sahihi ni mbinu tu za adui kutusahaulisha mambo ya msingi.
Wewe ni mjinga Sana ,,Yani unaamini mambo yaliyoletwa na wazungu ili uendelee kupumbazika
 
Back
Top Bottom