Mambo Manne ya kukusaidia. Kwanini Mungu anataka ulinde ubongo na mfumo wako wa fahamu kabla ya chochote

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,596
15,394
Mungu anawasiliana na wewe kupitia ubongo na mfumo wako wa fahamu.

Hili ni eneo ambalo ibirisi amelitafiti kwa Muda mrefu na amekuzungushia vitu vingi kushusha uwezo wako wa kusikia sauti ya Mungu.

Mit 4:23 SUV​

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Note: Moyo ni akili, kitovu cha maamuzi. Katika ulinzi kuna kulinda kwa kuzuia mashambulizi ya nje yasifikie target.

Kuna kulinda kwa kukiimalisha kinacholindwa. Mfano Benk kuna FFU nje lakini strongroom ina vault kubwa ambalo hata ukiua walinzi nje kufungua ni issue. Uzi huu umejielekeza kwenye kuimalisha kinacholindwa ulinzi wa ndani. Ulinzi wa ubongo kiini cha maamuzi yako.

Ulindeje ?
1: Kula vizuri. Kuna watu ni wadhambi kwa sababu hawajui kula. Wanakula vyakula na kunywa vyakunywa vinavyoziba njia za kupitishia sauti ya Mungu.

2: Fanya mazoezi. Mazoezi yanaufungua mwili na kuufanya mfumo wako wa fahamu kuwa janja (smart). Hapa namaanisha zoezi lq bei rahisi tu, kutembea kwa miguu kikakamavu.

3: Soma Biblia Kifalme. Soma kama unapokea maelekezo ya mfalme wa wafalme. Kwa maombi utapokea maelekezo mengi sana.

4: Jizungushie watu chanya na mazingira chanya. Epuka watu hasi maana shetani ni hasi na Mungu ni chanya. Mambo hasi yanafunga wepesi wa kupokea maelekezo chanya ya Mungu.

Fanyia kazi haya kwanza.
Yatakusaidia.

Ni hayo tu.
 
images%20(4).jpg
 
Back
Top Bottom