Tuache kufurahia mizaha mpaka kwenye mambo Matukufu ya Mungu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,568
44,777
Kuna watu sio tu ni waovu, na wakosaji, bali wamevuka hiyo mipaka hadi kufikia hatua ya kuleta mizaha mpaka kwenye mambo matukufu ya Mungu, kudhihaki, kukejeli, kukashfu Neno la Mungu, na wokovu kwa ujumla kwao ni jambo la kawaida.

Watu wanaifanyia biblia comedy kwenye majukwaa na watu wamelipa kiingilio, wameketi pale chini wanacheka na kufurahia.

Biblia ni kitabu cha story za vichekesho? Wanaonekana kwenye tv au youtube.

Na wengine wanatunga hizi memes za status Na wengine wanasambaza. Mambo hayo Ni machukizo.

Sote tunakosea ila Sasa tusifike stage ya kuleta mizaha kwenye mambo matakatifu ili kusudi ufurahishe watu tu.

Mfano Kuna mtu kapost eti "vile umeenda mbinguni halafu umekuta kitabu cha dhambi kimepotea" hiko kibwagizo kina picha Kama watu wanacheka na kufurahia.

Bnafsi naona sio sahihi ni mbinu tu za adui kutusahaulisha mambo ya msingi.
 
Ni kweli mkuu, kumekuwa na maigizo meng sana tena yasiyo yalazima, kwamfano christmass watu wakaanza post picha za Yesu feki wanasema birthday boy mara watafute picha za Yesu feki akiwa kifua wazi etc ila voti kama hivi viliandikwa vitatokea ili mwisho kila goti limkili kuwa yeye ni Mungu...
 
Kwanza kabisa, define Mungu ni nini halafu thibitisha yupo.

2 Wathesalonike 2:1-17

Yule Mtu Wa Kuasi

Ndugu, kuhusu kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanyika kwetu pamoja mbele zake, tunawasihi, msiyumbishwe kwa urahisi wala msitiwe wasiwasi na roho wala neno au barua inayosemekana kuwa imetoka kwetu, isemayo kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwako.Mtu yeyote na asiwadanganye kwa namna yoyote kwa maana siku ile haitakuja mpaka uasi utokee kwanza, na yule mtu wa kuasi adhihirishwe, yule ambaye amehukumiwa kuangamizwa kabisa.

Yeye atapingana na kujitukuza juu ya kila kitu kiitwacho Mungu au kinachoabudiwa, ili kujiweka juu katika Hekalu la Mungu, akijitangaza mwenyewe kuwa ndiye Mungu.

Je, hamkumbuki ya kwamba nilipokuwa pamoja nanyi niliwaambia mambo haya? Nanyi sasa mnajua kinachomzuia, ili apate kudhihirishwa wakati wake utakapowadia.

Maana ile nguvu ya siri ya uasi tayari inatenda kazi, lakini yule anayeizuia ataendelea kufanya hivyo mpaka atakapoondolewa.

Hapo ndipo yule mwasi atafunuliwa, ambaye Bwana Yesu atamteketeza kwa pumzi ya kinywa chake na kumwangamiza kabisa kwa utukufu wa kuja kwake.

Kuja kwa yule mwasi kutaonekana kana kwamba ni kutenda kazi kwake Shetani ambaye hutumia nguvu zote, ishara, maajabu ya uongo, na kila aina ya uovu kwa wale wanaoangamia kwa sababu walikataa kuipenda kweli wapate kuokolewa.

Kwa sababu hii, Mungu ameruhusu watawaliwe na nguvu ya udanganyifu, ili waendelee kuamini uongo, na wahukumiwe wote ambao hawakuiamini ile kweli, bali wamefurahia uovu.
 
Ni kweli mkuu, kumekuwa na maigizo meng sana tena yasiyo yalazima, kwamfano christmass watu wakaanza post picha za Yesu feki wanasema birthday boy mara watafute picha za Yesu feki akiwa kifua wazi etc ila voti kama hivi viliandikwa vitatokea ili mwisho kila goti limkili kuwa yeye ni Mungu....

Picha ya Yesu feki!! Picha ya Yesu halisi ni ipi?
 
Mafurahisha sana nyie watu 😀😀😀

Kwahiyo Mungu kashindwa kujitetea hadi mnakuja kulialia huku? Acheni upumbavu

Nasema upumbavu sababu hamjifunzi tu bado mmeendelea kushikilia hizi hekaya
 
Ni kweli mkuu, kumekuwa na maigizo meng sana tena yasiyo yalazima, kwamfano christmass watu wakaanza post picha za Yesu feki wanasema birthday boy mara watafute picha za Yesu feki akiwa kifua wazi etc ila voti kama hivi viliandikwa vitatokea ili mwisho kila goti limkili kuwa yeye ni Mungu...
Huyo original tutampataje?
 
N

Naomba utuwekee picha ya Yesu original,
 
Mafurahisha sana nyie watu 😀😀😀

Kwahiyo Mungu kashindwa kujitetea hadi mnakuja kulialia huku? Acheni upumbavu

Nasema upumbavu sababu hamjifunzi tu bado mmeendelea kushikilia hizi hekaya
Ulitaka ajitetee vipi wakati yeye mwenyewe ameruhusu hilo litokee, angetaka lisingetokea.

Ila nyinyi vijana huu ugonjwa wa akili utafutieni dawa.
 
Ulitaka ajitetee vipi wakati yeye mwenyewe ameruhusu hilo litokee, angetaka lisingetokea.

Ila nyinyi vijana huu ugonjwa wa akili utafutieni dawa.
Sasa kama yeye ndio karuhusu nini kinawapa mchecheto? Huoni kama nyinyi ndio mna ugonjwa wa akili? 🤔
 
Wewe babu yako wa ishirini, tukikwambia tunampataje,utatujibu vipi? Vijana mnauliza maswali ya kipuuzi mno, halafu nyote mnafanana mpaka wakubwa zenu nao akili zao visoda.
Yesu kawa babu siku hizi sio Mungu tena?

Hatari na nusu!
 
Kwa nini umie na kukasirika wakati watahukumiwa na kuchomwa moto.We kipende kitabu,sali sana, toa sadaka sana uende peponi ukale bata. Wazinfu wazini sana,walevi walewe sana,waongo waongope sana,wezi waibe sana kwa sababu kuna adhabu watachomwa moto wa mileke huku wewe ukila raha ya nini ukasirike.Kama watu wakiacha kukashifu wachungaji watamuhubilia nani?
 
Sasa kama yeye ndio karuhusu nini kinawapa mchecheto? Huoni kama nyinyi ndio mna ugonjwa wa akili? 🤔
Itakuwa hujui maana ya tamko mchecheto, hapo ni mja anawaonea huruma waja wenzake,juu ya yale yatakayo wapata kwa dhihaki hiyo.

Wagonjwa wa akili ni nyinyi mnaye mkana msiye mjua. Tafakari utaona uninga wako ulipo.
 
Yesu kawa babu siku hizi sio Mungu tena?

Hatari na nusu!
Ona sasa hata hili limekushinda, vipi uweze kumjadili Mola kisha upatie...?

Nilochofanya mimi ni kukuonyesha ya kuwa swali ulilo uliza ni swali la kipuuzi, swali ambalo haulizi ila mgonjwa wa akili au mtu muovu tena mjinga. Ulitaka uletewe Yesu halisi ? Jambo ambalo haliwezekani, ndiyo nikakukataka na wewe utuletew babu yako wa 20 katika nasaba yako, kama utaweza. Sasa sababu hamtafakari basi mnauliza maswali ambayo laiti kama mngetafakari msingeuliza maswali hayo sababu majibu unayo.
 
Back
Top Bottom