Tuache Kuforce Mambo, Mziki wa Kisingeli hauna Ladha

Tuache Kuforce Mambo, Mziki wa Kisingeli hauna Ladha

Yaani mimi nimetokea hata kuzichukia radio zinazopiga muziki huu wa kishenzi wenye makelele matupu. Kwanza siamini kama huu ni muziki kwa yale makelele maana muziki inatakiwa ziwe ni sauti zenye mpangilio maalumu. Mnanda niliuelewa lakini siyo mikelele Uchwara hiyo iliyopewa promo na EFM kua ni muziki
 
Moja kwa moja kwnye Hoja.
Nimejaribu kuufuatilia mziki wa kisingeli na kujiridhisha kua mziki huu unakuzwa kwa ushabiki wa Media na wasaka Tonge , ila ni mziki usio na ladha kamili ya Burudani. Na Umetokea kwa Bahati mbaya.
1.style moja ya kuimba.. ukijaribu kusikiliza waimbaji wote wa kisingeli wanamtiriko mmoja wa maishairi, unaweza kusikiliza Nyimbo tatu kwa muunganiko na ukaambiwa Umesikiliza nyimbo tatu na usikubali,ukidhani ni moja.
2. style moja kucheza..kama ni video zote zinafanana lazima vimbu litimuke, kushika viono na kuinama .. wote the same same stle.

Naonaga ni kelele tu.

USHAURI.

Kisingeli ubaki kua Mziki wa kawaida tu in a free style way huko uswahili ila si kuulazimisha kua mziki official kwnye

Burudani ya mziki TZ.
Ukweli mzuri ila unauma. [emoji122]
Mimi nafikiri ungeshauri uboreshwe na si kuupiga vita. Tanzania hatuna muziki wetu wenye vionjo vya kiasili..labda kidogo wale wana Njenje (The Kilimnjaro band) ambao wanapiga muziki wenye vionjo tofauti. Hawa waliobaki band zetu wote wanataka wafanane na wakongo. Muziki wa kisasa nawenyewe wanataka wawe wamarekani, siku hizi wanahamia kinageria zaidi.. Nawakumbuka Tatunane wale walifanya muziki wa kitanzania haswa kuuboresha kwa kuchanganya na ala za kisasa na walifanya vizuri. Singeli hii ni mchiriku ulioboreshwa, ni ngoma za asili za kizaramo. Ngoma za kizaramo zinakwenda zikibadilika.. nakumbuka wakati kulikuwa na Gombe sugu, ukaja mdundiko, ukaja mnanda au mchiriku, na hii singeli ni haohao..ukiuliza wote hao wakina Shorwe mwamba,msaga sumu, manifongo wote hao utakuta asili yao huku pwani. Sio mbaya kama ukaboreshwa na sisi watanzania tukawa na asili yetu ya muziki.
 
Napenda sana ile radha ya msaga sumu!
ingawa huwa wanasema sio singeli.....ila jamaa anakaubunifu flani kwenye mziki wake
 
Moja kwa moja kwnye Hoja.
Nimejaribu kuufuatilia mziki wa kisingeli na kujiridhisha kua mziki huu unakuzwa kwa ushabiki wa Media na wasaka Tonge , ila ni mziki usio na ladha kamili ya Burudani. Na Umetokea kwa Bahati mbaya.
1.style moja ya kuimba.. ukijaribu kusikiliza waimbaji wote wa kisingeli wanamtiriko mmoja wa maishairi, unaweza kusikiliza Nyimbo tatu kwa muunganiko na ukaambiwa Umesikiliza nyimbo tatu na usikubali,ukidhani ni moja.
2. style moja kucheza..kama ni video zote zinafanana lazima vimbu litimuke, kushika viono na kuinama .. wote the same same stle.

Naonaga ni kelele tu.

USHAURI.

Kisingeli ubaki kua Mziki wa kawaida tu in a free style way huko uswahili ila si kuulazimisha kua mziki official kwnye

Burudani ya mziki TZ.
Ukweli mzuri ila unauma. [emoji122]

Siupendi huo mziki wa singeli
 
Naunga mkono hoja,miziki ya kipuuzi kama ilivyo tu taarab haitoweza kudumu
 
Kisingeli ni burudani ya mjini....weee wamuleba tulia.....
 
Hayo masingeli kwa wenyeji wa pwani wasituletee upuuzi sisi watu wa mikoani. Nikiwa nimefungulia redio au Tv wakiweka visingeli vyao huwa nazima au kubadilisha station au channel haraka sana
 
Weka tuweke mwambaaaa!! Oshh osssh...watoto wa palestina watoto wa kitengo masadali... Nakubaliii mwamba eeee weka tuweke!!!
 
neno ''masela'' kwenye kisingeli ni kama ''nigga'' kwenye hip hop..
 
Mimi nafikiri ungeshauri uboreshwe na si kuupiga vita. Tanzania hatuna muziki wetu wenye vionjo vya kiasili..labda kidogo wale wana Njenje (The Kilimnjaro band) ambao wanapiga muziki wenye vionjo tofauti. Hawa waliobaki band zetu wote wanataka wafanane na wakongo. Muziki wa kisasa nawenyewe wanataka wawe wamarekani, siku hizi wanahamia kinageria zaidi.. Nawakumbuka Tatunane wale walifanya muziki wa kitanzania haswa kuuboresha kwa kuchanganya na ala za kisasa na walifanya vizuri. Singeli hii ni muziki nafikiri ni mchiriku ulioboreshwa, ni ngoma za asili za kizaramo. Ngoma za kizaramo zinakwenda zikibadilika.. nakumbuka wakati nakua kulikuwa na Gombe sugu, ukaja mdundiko, ukaja mnanda au mchiriku, na hii singeli ni haohao..ukiuliza wote hao wakina Shorwe mwamba,msaga sumu, manifongo wote hao utakuta asili yao huku pwani. Sio mbaya kama ukaboreshwa na sisi watanzania tukawa na asili yetu ya muziki.
Kwakweli nisiwe mnafiki tu , kabla ya kushauri Uboreshwa , naomba ufutwe kabisa na Kitengo cha Utamaduni na saana kijikite Upya kusaka mziki halisi wa bongo kama kweli tunaujitaji ... but kisingeli BiG NO .... tunaipigia Dunia Kelele .
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom