Castr
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 39,007
- 79,104
Hili shoga la Mwanza au Tarime.Mwanaume wa mkoa anamlimia wa DarView attachment 900210
Hili shoga la Mwanza au Tarime.Mwanaume wa mkoa anamlimia wa DarView attachment 900210
Arusha mkuu[emoji1] [emoji1]Hili shoga la Mwanza au Tarime.
Arusha mkuu[emoji1] [emoji1]
Ahahahahaaaa wanatafuta huruma ya serikaliWanaume wa Dar kwa kulia lia bwana! Eti mwenzako kafungua uzi anaomba serikali iwasaidie msitaniwe! Dah!
Hivi mwanaume kabisa mwenye majukumu ya kifamilia unaweza kula chips ukasema umeshiba na ukaenda kufanya mishe zako kawaida? Acha upuuzi mkuu wa kushabikia vitu visivyofaa,sema ukweli ili uokoke!Kuna utani mbaya unaoendelea kushika hatamu kuhusu Mwanaume wa Dar. Utani huo usiofaa, unamdhalilisha na kupotosha sifa muhimu za mwanaume anayeishi na kutafuta maisha katika Jiji kubwa la kibiashara la Dar es Salaam.
Sisi kama Great Thinkers tukiendelea kukaa kimya, in the long run utani huu unaweza kupunguza ari ya vijana wengi kupambana na maisha, kuathiri baadhi ya biashara hivyo kupunguza mapato katika jiji hili tegemezi la taifa.
Mathalani, soko la viazi ni kubwa sana katika jiji hili kutokana na zao hilo kutumika katika kuandaa chakula cha haraka (fast food) kwa ajili ya wale wasiopata muda wa kukaa jikoni na kujiandalia chakula cha mchana/jioni kutokana na mishe mishe zao.
Viazi (chips) ni biashara kubwa na imeajiri wengi, hivyo kutania kwamba chakula hiki hakifai kuliwa na wanaume, kunaweza kusababisha athari kubwa ya kiuchumi kwa wakulima na wachuuzi kule Mbeya kwa rafiki yangu Ipyana, japo kwa sasa tunaweza kuchukulia kama mzaha. Isitoshe, sijaona maelezo yoyote ya kitaalamu yanayoonesha kuwa chakula hiki hakifai kwa matumizi ya binadamu, achilia mbali mwanaume.
Mifano ipo mingi na inafahamika. Kwa mfano baadhi ya vipindi vya televisheni, radio, mavazi, na kazi kadha wa kadha zinadharauliwa kwamba zinafanywa na Wanaume wa Dar - yaani eti kuna biashara/kazi hazifai kufanywa na Mwanaume. Dunia hii ya sasa?!
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo kulikuwa na utani wenye maslahi. Sifa kubwa ya Mwanaume wa Dar ilikuwa ni mtu mwenye matumizi makubwa ya akili (bongo) ambayo ilichochea kwa kiasi kikubwa vijana kuwa active kwenye mishe zao. Misemo kama kuzaliwa mjini pekee ni form 6 iliongeza motisha ya uchakakarikaji. Na hiyo ni miongoni mwa sababu kubwa iliyolikuza Jiji hili na kustawi kibiashara.
Nihitimishe kwa kukumbushia sifa za kweli za Mwanaume wa Dar:
1. Ni mzaliwa au mkazi wa kudumu wa Jiji la Dar es Salaam.
2. Msomi, mwerevu na mchangamfu kwa kila mtu.
3. Mwenye ndoto, mipango na malengo ya kufanikiwa kimaisha.
4. Ana hulka ya uchakarikaji, uthubutu na mtumiaji mzuri wa fursa za kiuchumi.
5. Mwenye maarifa na ujuzi wa mambo yanayoendelea duniani. Ni mtu mjanja na anayeendana na kasi ya sayansi na teknolojia.
Kimsingi, hii picha inayotengenezwa sasa kuhusu mwanaume wa Dar haina uhalali wowote. Ni matokeo ya kiwango cha ujinga uliokithiri katika jamii zetu na wanaouendekeza utani huo ni watu duni kifikra.
Tuukatae utani huu usio na manufaa yoyote zaidi ya kudhalilisha. Tuukatae kwa sababu unaturudisha nyuma.
Na unamvika pete demu harafu unapiga magoti? Kweli wanaume wa Dar mnashida aisee.....badilikeniSasa kama mnajiliza kwenye send - off, mtaachaje kutaniwa?
Mpumue kwa kumalizia hela kwenye kuhonga uko serious kweli wewe?Mkuu unafanya wazee wa dar yetu tupate kupumua kidogo,maana khaaa!
Mnawafanya waishi maisha magumu sababu hela zote wanamalizia kwenye kuhonga huku wao wakila chips,eti wanakusifu unawatetea jamani!!Pumueni Dada zao tunawapenda Sana. Achaneni na kaka zetu
ndo maana mr.jiwe anataka kuhamia domuMathalani, soko la viazi ni kubwa sana katika jiji hili kutokana na zao hilo kutumika katika kuandaa chakula cha haraka (fast food) kwa ajili ya wale wasiopata muda wa kukaa jikoni na kujiandalia chakula cha mchana/jioni kutokana na mishe mishe zao.
Mkuu umewaza kitu sijawahi fikiria, aloo kuna ukweli ndani yake, jamaa keshastuka.ndo maana mr.jiwe anataka kuhamia domu
Kitu kingine ni kwamba wanaumme wa Dar hawaoi mke, bali wanaoana na wake zao.Kuweka kumbukumbu sawa.
Neno mwanaume wa Dar lilianzishwa na wanaume wanaoishi Dar wenyewe.. Kumbukumbu zinaonyesha ilikuwa ni jambo la ufahari na ujanja kwa mwanaume anayeishi Dar kujitambulisha kuwa anaishi Dar na wakati huo huo kuwaona wanaume kutoka mikoani kama washamba fulani.
Kila mtu alitamani kujitambulisha kama mkazi/ mwenyeji wa Dar hata kama hakuwahi kuishi, kufika au kuifahamu Dar. Yaani sifa ya kuishi Dar ilikuwa inatosha hata kupata rafiki wa kike au rafiki wa kiume kirahisi sana.
Bahati mbaya sana zama zimebadilika sana, kuishi Dar sio issue tena, wengi wa watanzania wanaoishi mikoani walishawahi kufika au kuishi Dar na pia mikoa mingi imepanuka kimaisha pamoja na uwepo wa mitandao ya kijamii kufanya watu kujihisi hakuna tofauti yoyote kubwa ya maana kimaisha na mitindo tena kati ya Dar na mikoani. Dar hakuna jipya tena.
Jambo baya la kusikitisha ni kuwa, wanaume wa Dar wamekuwa watumwa wa mitindo mibovu ya kuiga kuiga maisha ya kimagharibi kama ndio ujanja wakati kiuhalisia ni ujinga, utoto na ulimbukeni. Kwa mfano wa mambo haya.
1/Kusuka nywele.
2/Kujichubua ngozi.
3/Ushoga.
4/Kujirahisisha.
5/Kuvaa hereni.
6/Kufanya 'makeup'
7/Kupenda vitu vyepesi na laini laini kama Chips, Chocolate.
8/Kutaka kulelewa na wanawake.
9/Kuvaa nguo za kubana.
10/Kuvaa nguo chini ya makalio.
11/Kuonyesha nguo za ndani(Kama chupi, Boxer)
12/Kuanika picha na video za mahusiano yao ya kimapenzi mitandaoni.
13/Kuanika vifua vyao(Six packs!)
14/Kupenda kick.
Aisee juzi nilikuwa pub moja opposite na mlimani city, nakuta almost watu wote wanakunywa Savannah na Heineken kwa mbali mpaka nikashangaa, pub nzima niliona meza moja tu imelaza bapa na meza yetu ndo tunakunywa bia zetu hizi ngumngum. [emoji23][emoji23][emoji23]madada poa na mashoga kibaoo, wanaume wanakuja bar na vikaptula vifupii, wakilewa wanavikunja kama vile mtu alievaa surual akiwa anapita kwenye matope mapaja yote nje[emoji23][emoji23][emoji28][emoji28][emoji28]. Aisee dar kutamu sana unaingia sehem unaagiza safar lager watu wanakutolea macho ka unakunywa sumu!!Mwanaume wa Dar eti anaenda bar anaagiza Savannah?
Huu utani ni kama Simba na Yanga mkuu....
Hautakuja isha kamwe!!!
Pamoja na changamoto hizo ila bado vibanda vya chips vinazidi kuota kama uyoga, na wanaume wana kula kama kawaida.
So, hiyo ni misemo tu bro, japo ukweli unauma.