TTCL imesababisha nifukuzwe Kazi

TTCL imesababisha nifukuzwe Kazi

Mimi Nilikuwa ni system adm wa kampun moja ya wazungu hapo Masaki, sasa jana bosi wangu alikuwa na mkutano wa online na mkurugenzi mkuu ambae yupo Marekani.

Kutokana na umuhimu wa hayo maongezi yao ikabidi bosi wangu aniombe ushauri kuhusu ni mtandao gani ambao una strong internet connection.

Kutokana na matangazo ya TTCL ya siku hizi, nikaona hawa jamaa watakuwa wamebadilika sana, kumbe Dah Nilikuwa naingia choo cha kike, nikamshauri bosi wangu kwa mbwembwe nyingi kuwa TTCL ni best kampany.. mmh nikapewa pesa za kwenda kununua line ya TTCL, nikaenda moja kwa moja makao makuu pale Samora, kufika pale nikanunua line kwa sh 2000 na muda wa maongezi....

Huwezi kuamini ishu ya kusajili line tu ilinichukua masaa 3 mpaka bosi akawa ananipigia simu kwamba vipi tena mbona unachelewa?

Ikabidi niondoke kurudi ofisini na yule mhudumu akaniambia niweke line kwenye simu na itafunguka tu yenyewe, nikafika ofisini nikampatia bosi wangu ile line na nikampa maelezo kuwa aweke kwenye simu na itafunguka tu yenyewe....

Dah mpaka saa 12 jioni hakuna kitu, bahati nzuri nilichukua namba ya yule dada alienihudumia nikampigia simu, jibu lake ndio niliishiwa pozi zote...

Akasema kesho asubuhi niende na hiyo line oh my god bosi akaanza kubadilika rangi akaanza kupiga simu kwa wazungu wenzake na kila mzungu akawa anatoa lawama kwangu kuwa why nilichagua TTCL ikiwa wenyewe tu wafanyakazi wa TTCL hawatumii huo mtandao....

So kwa hasira bosi kanifukuza kazi coz nimempa ushauri wa kampuni ambayo Nilikuwa najua fika kuwa huduma zake ni mbovu.

Ushauri wangu kwa TTCL ni kwamba fungeni hiyo kampuni yenu mpaka hapo ambapo mtakuwa tayari kuingia kwenye soko la ushindani.


Hapana, umefukuzwa kazi kwa ajili ya ujinga wako, Mimi sio system admin Ila nisingeweza kufanya hiyo assumption! As a system admin hapo ulipofukuzwa kazi Ni sawa. Hata Mimi ningekufukuza.

Kwa hizi line za simu waweza Kukuta kariKoo ipo active na masaki haipo active kwenye swala la data. Haya yote system admin anatakiwa kujua.

Halafu hiyo organization itakuwa gumashi, why don't you guys have a reliable internet everyday hapo oficin mpaka wakati wa conference? Na wasiwasi, Muheshimiwa Kigwangala wacheki hawa watu!
 
Eti ooh mkongo wa taifa...mi sijaona hasa performance ya kuridhisha
We acha tu nilitegemea pia mkonga wa taifa utakuwa kama ngonjera zengine.tuliambiwa gas ya mtwara ingetupa umeme wa uhakika lakin wapi sembuse huo mkonga.
 
huyu namuona ni muongo sababu ...90% ya bank zote tanzania wanahudumia TTCL 90% YA mashirika na taasisi ziwe za kiserikali au private wanahudumia wao kwenye data ....wanawauzia voda,smile,airtel kupitia NICTBB....inawezekana kama ni kweli anayoyasema huyo aliemuhudumia sio mtu wa mwisho kuna ma supervisor wao pale kwa ushindani wa soko la data kwa tanzania sidhani kama hio ingechukua mda mrefu...labda mleta mada ana agenda binafsi hayo mashirika mengine yanatangaza 4g wakati 3G YENYEWE yameshindwa ....tukianza kutafuta madhaifu ya haya mashirika basi ttcl ina nafuu.....ttcl wako vizuri sana kwenye data na wana facility zote kwenye mobile voice ndio wanataka kuingia kwa sasa ingawa wamechelewa mno
Upo nje ya mada!!!, mtoa mada anaongelea "usajili wa line". Wewe unaongelea "internet service"
In short: jamaa katumia siku nzima kusajiri line na bado hakufanikiwa . Kibaya zaidi akadhauriwa aende kesho yake asubuhi...Na hicho ndicho kilichomfukuzisha kazi
 
Unanunua line ya TTCL kwa 2000 ufanye mawasiliano USA??? Walau ungesema ulienda kununua device zao za 4G kwa ajili ya kufanya hayo mawasiliano walau ningekuamini lakini line ya simu???? Hiyo line then uipeleke kuweka kwenye device gani??? Muongo mkubwa wewe
Kwani mawasiliano USA ni ya internet tuu??? Hawaruhusi kupiga simu? au mpaka awaambie nilinunua muda wa maongezi nikashindwa kuuingiza kwasababu usajiri ulishindikana kwa zaidi ya siku nzima??
 
TTCL ni jibu lililoiva siku nyingi, sijui Magu anasubiri nini kulitumbua, yaani huduma zao ni kichekesho
 
Mimi niliyasikia hayo matangazo nikaenda kuchukua line pale tegeta kibo, cha kushangaza nilikuwa na 5000 wakasema hawana chenji,ikabidi nitafute chenji, nafika kwetu naweka line kwenye modem, hata network ya 2g hamnaaa! Haisomi kabisaaa! Nilichoka!
 
Mimi Nilikuwa ni system adm wa kampun moja ya wazungu hapo Masaki, sasa jana bosi wangu alikuwa na mkutano wa online na mkurugenzi mkuu ambae yupo Marekani.

Kutokana na umuhimu wa hayo maongezi yao ikabidi bosi wangu aniombe ushauri kuhusu ni mtandao gani ambao una strong internet connection.

Kutokana na matangazo ya TTCL ya siku hizi, nikaona hawa jamaa watakuwa wamebadilika sana, kumbe Dah Nilikuwa naingia choo cha kike, nikamshauri bosi wangu kwa mbwembwe nyingi kuwa TTCL ni best kampany.. mmh nikapewa pesa za kwenda kununua line ya TTCL, nikaenda moja kwa moja makao makuu pale Samora, kufika pale nikanunua line kwa sh 2000 na muda wa maongezi....

Huwezi kuamini ishu ya kusajili line tu ilinichukua masaa 3 mpaka bosi akawa ananipigia simu kwamba vipi tena mbona unachelewa?

Ikabidi niondoke kurudi ofisini na yule mhudumu akaniambia niweke line kwenye simu na itafunguka tu yenyewe, nikafika ofisini nikampatia bosi wangu ile line na nikampa maelezo kuwa aweke kwenye simu na itafunguka tu yenyewe....

Dah mpaka saa 12 jioni hakuna kitu, bahati nzuri nilichukua namba ya yule dada alienihudumia nikampigia simu, jibu lake ndio niliishiwa pozi zote...

Akasema kesho asubuhi niende na hiyo line oh my god bosi akaanza kubadilika rangi akaanza kupiga simu kwa wazungu wenzake na kila mzungu akawa anatoa lawama kwangu kuwa why nilichagua TTCL ikiwa wenyewe tu wafanyakazi wa TTCL hawatumii huo mtandao....

So kwa hasira bosi kanifukuza kazi coz nimempa ushauri wa kampuni ambayo Nilikuwa najua fika kuwa huduma zake ni mbovu.

Ushauri wangu kwa TTCL ni kwamba fungeni hiyo kampuni yenu mpaka hapo ambapo mtakuwa tayari kuingia kwenye soko la ushindani.
Ndio maana Magufuli kaomba msaada Rwanda
System Admin gani upo nje kabisa ya soko?
Ni bora angekupiga risasi kabisa,unajua hiyo kampuni imepoteza kiasi gani kwa dili liliotaka kuzungumziwa
 
Pole sana kwa matatizo, nilipata tatizo na laini yangu ya 4G nikarudi pale ofisini kwao kumbe issue ilikua kwenye simu yangu sasahivi mambo ni poa, so ni bora ukarudi kwao kama uliweza kwenda hadi Samora sidhani kama utashindwa kurudi tena wakakusaidia
 
Mimi Nilikuwa ni system adm wa kampun moja ya wazungu hapo Masaki, sasa jana bosi wangu alikuwa na mkutano wa online na mkurugenzi mkuu ambae yupo Marekani.

Kutokana na umuhimu wa hayo maongezi yao ikabidi bosi wangu aniombe ushauri kuhusu ni mtandao gani ambao una strong internet connection.

Kutokana na matangazo ya TTCL ya siku hizi, nikaona hawa jamaa watakuwa wamebadilika sana, kumbe Dah Nilikuwa naingia choo cha kike, nikamshauri bosi wangu kwa mbwembwe nyingi kuwa TTCL ni best kampany.. mmh nikapewa pesa za kwenda kununua line ya TTCL, nikaenda moja kwa moja makao makuu pale Samora, kufika pale nikanunua line kwa sh 2000 na muda wa maongezi....

Huwezi kuamini ishu ya kusajili line tu ilinichukua masaa 3 mpaka bosi akawa ananipigia simu kwamba vipi tena mbona unachelewa?

Ikabidi niondoke kurudi ofisini na yule mhudumu akaniambia niweke line kwenye simu na itafunguka tu yenyewe, nikafika ofisini nikampatia bosi wangu ile line na nikampa maelezo kuwa aweke kwenye simu na itafunguka tu yenyewe....

Dah mpaka saa 12 jioni hakuna kitu, bahati nzuri nilichukua namba ya yule dada alienihudumia nikampigia simu, jibu lake ndio niliishiwa pozi zote...

Akasema kesho asubuhi niende na hiyo line oh my god bosi akaanza kubadilika rangi akaanza kupiga simu kwa wazungu wenzake na kila mzungu akawa anatoa lawama kwangu kuwa why nilichagua TTCL ikiwa wenyewe tu wafanyakazi wa TTCL hawatumii huo mtandao....

So kwa hasira bosi kanifukuza kazi coz nimempa ushauri wa kampuni ambayo Nilikuwa najua fika kuwa huduma zake ni mbovu.

Ushauri wangu kwa TTCL ni kwamba fungeni hiyo kampuni yenu mpaka hapo ambapo mtakuwa tayari kuingia kwenye soko la ushindani.



Ndugu hp4510

Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) inaomba radhi kwa matatizo na usumbufu uliotokea.

Maoni yako ni muhimu kwetu na yametupa changamoto ya kuendelea kuboresha zaidi huduma zetu na kuchukua hatua stahiki kwa wafanyakazi wetu.
Tafadhali kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia customercare@ttcl.co.tz au unaweza kupiga namba 100 (Kwa kutumia laini ya TTCL) au 0222 100 100 (kwa kutumia mitandao mingine) ili tuweze kushauriana zaidi.

Pia unaweza kutembelea Kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo Posta, Mtaa wa Samora ili uweze kuonana na Meneja wa TTCL mkoa wa DSM kati, Ndugu Diwani Mwamengo kwa kushauriana zaidi, Ndugu Diwani anapatikana kwa simu namba 0732 100 008.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
18/08/2016
 
Utakuwa ni Admin wa Mpitimbi.Ni nani aisyejua kwamba kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi wa mawasiliano na yenye kutoa huduma mbovu sana za internet ni hiyo TTCL
 
Back
Top Bottom