TTCL imesababisha nifukuzwe Kazi

TTCL imesababisha nifukuzwe Kazi

Ndugu hp4510

Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) inaomba radhi kwa matatizo na usumbufu uliotokea.

Maoni yako ni muhimu kwetu na yametupa changamoto ya kuendelea kuboresha zaidi huduma zetu na kuchukua hatua stahiki kwa wafanyakazi wetu.
Tafadhali kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia customercare@ttcl.co.tz au unaweza kupiga namba 100 (Kwa kutumia laini ya TTCL) au 0222 100 100 (kwa kutumia mitandao mingine) ili tuweze kushauriana zaidi.

Pia unaweza kutembelea Kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo Posta, Mtaa wa Samora ili uweze kuonana na Meneja wa TTCL mkoa wa DSM kati, Ndugu Diwani Mwamengo kwa kushauriana zaidi, Ndugu Diwani anapatikana kwa simu namba 0732 100 008.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
18/08/2016

Leo mchana nilikwenda pale kituo cha kijitonyama, nikamkuta mdada anaitwa Leila I think ni mweupe, na akarekebisha tatizo langu na kwa maelezo yake ni kuwa line ilikuwa haijafanyiwa anything..... I think mnatakiwa kuajiri vijana wa kazi ambao sio wa kufanya kazi kwa mazoea... thank you
 
TTCL walijichimbia kaburi la ushindani walipo kuja na vilaini vyao we una Samsung huwezi tumia line ya TTCL wakapoteza vichwa sijui waliponzwa na wale wahindi wa Bharti? Wamezinduka bado wameng'ang'ania vilaini vyao hivyo licha ya kupewa ruzuku walipaswa kuanzisha ushindani na tigo, voda, airtel wanapigwa bao na Halotel wapo mpaka vijijini ambako mitandao mingine unapanda juu ya mti.
 
Hapana, umefukuzwa kazi kwa ajili ya ujinga wako, Mimi sio system admin Ila nisingeweza kufanya hiyo assumption! As a system admin hapo ulipofukuzwa kazi Ni sawa. Hata Mimi ningekufukuza.

Kwa hizi line za simu waweza Kukuta kariKoo ipo active na masaki haipo active kwenye swala la data. Haya yote system admin anatakiwa kujua.

Halafu hiyo organization itakuwa gumashi, why don't you guys have a reliable internet everyday hapo oficin mpaka wakati wa conference? Na wasiwasi, Muheshimiwa Kigwangala wacheki hawa watu!
Acha upuuzi Kingwangala awacheck kama nani? Amekwambia anapiga ramli kwa Internet?
 
Ndugu hp4510

Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) inaomba radhi kwa matatizo na usumbufu uliotokea.

Maoni yako ni muhimu kwetu na yametupa changamoto ya kuendelea kuboresha zaidi huduma zetu na kuchukua hatua stahiki kwa wafanyakazi wetu.
Tafadhali kwa mawasiliano zaidi, wasiliana nasi kupitia customercare@ttcl.co.tz au unaweza kupiga namba 100 (Kwa kutumia laini ya TTCL) au 0222 100 100 (kwa kutumia mitandao mingine) ili tuweze kushauriana zaidi.

Pia unaweza kutembelea Kituo chetu cha huduma kwa wateja kilichopo Posta, Mtaa wa Samora ili uweze kuonana na Meneja wa TTCL mkoa wa DSM kati, Ndugu Diwani Mwamengo kwa kushauriana zaidi, Ndugu Diwani anapatikana kwa simu namba 0732 100 008.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
18/08/2016

Badilikeni teknolojia mnayo tumia sio kabisa hivi anae tumia iPhone unategemea aje anunue line ya TTCL?
 
TTCL tafuteni vijana kama wakina jackson mmbando walete maboresho ya kweli, mnabadilisha logo wakati mentality ni zile zile, hamfanyi promotion etc still mnataka kuungwa mkono..
 
Back
Top Bottom