Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,330
- 2,283
Kama ilivyo kwa taasisi za serikali kwa uzembe TTCL nao wamo. Nilienda 7SABA maonyesho nikakutana na maafisa nikakaribishwa vizuri na kutanfaziwa faiba mlangoni, nikaipenda. Nikaulizia taratibu nikaambiwa unajaza fomu anakuja savea na kuangalia eneo kisha unaletewa huduma. Nikauliza inaweza kuchukua muda gani mpaka kufungiwa? Akajibu ndani ya wiki moja tu.
Akachukua taarifa zangu, nikafika nyumbani nikajaza ombi online. Nikasubiri wiki ya kwanza hola, ya pili hola, nikaenda makao yao posta nikajibiwa ombi limepokelewa kanda yako. Nikaelekezwa niende huko.
Nikakaa tena wk 2 nyingine ndio nikaenda mpaka Nyerere rd karibu na kiwanda cha sigara nikauliza kuhusu ombi langu. Nikaambiwa kweli ila "NITAFIKIWA TU" foleni kubwa kidogo afu pia kuna changamoto ya vifaa kwa hiyo niwe mvumilivu.
Toka mwezi wa saba muda muda huu naandika hata simu sijawahi kupigiwa miezi minne, kweli wako serious na kazi kweli?
Nikakimbilia voda supakasi siku 4 tu mzigo ninao mkononi. Kuna jamaa nae alituma maombi amehangaika mwishowe kakimbilia airtel.
Kwa sasa zuku fiber ndio habari ya mjini kwa waoishi ushuani na maeneo yenye watu wengi, kama Ttcl ingekuwa makini na malengo ingekuwa kwa haraka sana sababu Ttcl kwa mwezi ni 55000 tu unafungiwa wakati zuku ni 75000.