CURRENT ISSUE
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 256
- 57
Dalili zote zinaonyesha kuwa waziri mkuu wa Zimbabwe yatamkuta yaliyomkuta Raila wa Kenya.Maeneo mengi aliyokuwa na wabunge sasa yamechukuliwa na chama tawala cha rais Mugabe.Wananchi walijitokeza kwa wingi sana kuchagua kiongozi wampendaye,na kwa matokeo ya ubunge yanavyoonyesha,kwa upande wa rais watampa Mugabe na ndio maana Tsvangirai ameanza kutoa shutuma mbalimbali.Hivyo kwa matokeo haya Watanzania tunapaswa kujifunza kwa wenzetu.Tusikurupuke kuchagua tu,tufanye tathmini ya nani anafaa kuwa kiongozi wa taifa letu.Uchaguzi wa 2014 utusaidie kufanya hilo,tusiruhusu kujifunza kwa njia ngumu kama waliyotumia Zimbabwe.Wamejifunza hivi walivyofanya baada ya umwagaji wa damu mwaka 2008,hivyo hivyo na Kenya.Chonde chonde watz tusiingie kwenye hali hiyo,tufanye maandalizi mapema ili kuepusha vurugu,tuwape walio shikilia mpini tayari.