Why Am team Trump?

  • Thread starter Comred Mbwana Allyamtu
  • Start date

Comred Mbwana Allyamtu

Comred Mbwana Allyamtu

Verified Member
Joined
Jun 28, 2016
Messages
213
Likes
240
Points
60
Age
31
Comred Mbwana Allyamtu

Comred Mbwana Allyamtu

Verified Member
Joined Jun 28, 2016
213 240 60
KWANINI NIMEKUWA UPANDE WA DORNARD TRUMP?. NA JE KAMA AFRIKA NA ASIA NINI FAIDA YAKE?

Na Comred Mbwana Allyamtu.

Kwanza nianze na kauli hii ambayo Ilipata kutamkwa na mwasisi wa ufunuo wa dhana ya taifa la israel Benjamin Hezre Theodore mwaka 1890 alisema namnukuu....."Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili kwa mwanadamu yoyote"....

Ningependa kauli hii ndio iwe muongozo wa hoja yangu ya Leo.. Ambayo yawezekana marafiki zangu wengi walishindwa kutambua Juu ya mimi kuwa muungaji mkubwa mkono wa rais mteule wa marekani bwana Dornald Trump, Wako baadhi wamekuwa wakinilaumu Mara kadha kwa nini mimi niwe upande wa Trump? Tena walikwenda mbali kwa madai ya kile wanachokiita kuwa Trump ni "mbaguzi na muhafidhina" lakini kama haitoshi watu wangu wakaribu wamekuwa wakiaamini kuwa mimi ni Mwanamapinduzi mwenye kuamini katika Afrika kwanza (Afrocentrism) iweje niwe team Trump?.... Mtu alionekana wazi kabisa kuwabagua watu weusi na kutoa lugha zenye fedheha kwa waafrka. Lakini hao hao wamesahau ule msemo wa kiswahili unaosema "Kuchagua ni kutaka..." Hivyo ilikuwa haki yangu ya kidemokrasia kuchagua kule nitakako baada ya kuona upande wa Trump ni bora zaidi kuliko huo upande mwingine kama nitakavyo zieleza hapo baadae,

Pili hao hao wanasahau kuwa Trump ndie aliokuwa chaguo la wamarekani ambaye wao wamarekani ndio walimuona anawafaa sasa iwaje mimi niseme afai? Marekani ndio waliomuanda kuja kusimamia masrahi ya USA kama ilivyo kawaida yao (1797 George Washington alisema namnukuu..."Katika Kulinda masrahi ya nchi yao ni bora zaidi kuliko haki ya walio wengi"). Na ndivyo imekuwa hivyo katika chaguzi zote marekani wamekuwa wakifanya kuhakikisha kuwa wanampata mtu mwenye kulinda masrahi yao, Katika utalatibu uliotumika kumpata Trump ndio utalatibu ambao ni tamaduni ya marekani kuwapata viongozi wao kwa zaidi ya miaka 230 sasa na ndio utaratibu ambao Wao huamini ndio njia sahihi au mfumo bora kwao katika uchaguzi kutoa fursa ya kumpata MTU anayeweza kulinda masrahi ya taifa lao. Na mfumo huo ndio umemuibua Trump kuwa mshindi. lakini jambo linalonishangaza sasa ni pale wachambuzi kadha nje ya marekani wameukosoa ushindi wa trump na kujifanya wao ndio waliostahili kuwa waamuzi wa mustakabali wa marekani Juu ya mambo yao ya msingi. Lakini toka lini "adui akakuombea mema?" Mimi ninaamini wamarekani ni watu makini sana sio raisi kukosea kufanya maamuzi tena katika mambo mkubwa kiasi cha kuifanya White house ikaliwe na mwendawazimu, Pia kwangu naamini hilo sio jambo lahisi na ukweli halisia ndio hivyo eti mfumo wa marekani upenyeze mwendawazimu kuwa rais wa taifa lao? tena Taifa kubwa duniani? Bado siwezi kuamini kuwa wajumbe maalumu 538 tena walio bobea katika ubobezi wa masrahi ya taifa lao kumuidhinisha Trump kuwa raisi tena isitoshe wananchi wenyewe kwa wingi wao wameamua kumchagua Trump kwa kumpigia kura nyingi za wajumbe maalumu wa kuchagua nani awe raisi wa taifa lao. Lakini pia walipendekeza kuwa pamoja na kumuona Trump ndie anaefaa kuwa msimamizi wa masrahi yao Bado walipendekeza kuwa Clinton ni MTU pia wanaompeda lakini hafai kuwa msimamizi wa taifa lao na ndio maana hawakumchagulia wajumbe wengi wa electoral college. alafu eti wale wachambuzi uchwara wanakuja kuukosoa uhalali wa ushindi wa Trump

Najua kuna watu wengi bado wanakanganywa na namna mfumo wa marekani unavyo fanya kazi Labda sasa inabidi kuelezea kwa kifupi kuhusu mfumo huo unaokanganya. Kimsingi, Wamarekani hawamchagui Rais wao moja kwa moja, badala yake kila jimbo lina watu wanaofahamika kama electors (wachaguzi) ambao hukutana mwezi Desemba mara baada ya kura zilizopigwa na kila aliyejiandikisha kupiga kura Novemba 8 ya mwaka wa uchaguzi. Kama tulivyoona kwenye matangazo ya runinga, kila jimbo lina idadi yake ya "wachaguzi." Na jumla ya wachaguzi hao kutoka majimbo yote 51 ya Marekani ni 538. "Wachaguzi" hao nao huchaguliwa na vyama vyao. Kila chama kina kanuni zake za uchaguzi wa "wachaguzi" hao. Uchaguzi wao hufanyika kwa hatua mbili. Kwanza, chama huchagua orodha ya "wachaguzi watarajiwa" na pili, "wachaguzi halisi" huchaguliwa na wapigakura siku ya uchaguzi. Majina ya wanaogombea kuwa “wachaguzi" yanaweza kuonekana katika karatasi ya kura au yasionekane, kutegemea kanuni husika.Hakuna sheria inayowabana "wachaguzi" kumpigia kura mgombea aliyeshinda popular vote. Na ni katika mazingira haya ndio maana kumekuwa na jitihada za kuwashawishi "wachaguzi" hao kutompigia kura Trump, ili kumkwamisha na hatimaye kumwezesha Hillary achaguliwe. Hata hivyo, uwezekano wa hilo kutokea ni mdogo. Kihistoria, asilimia 99 ya "wachaguzi" hupiga kura kwa mshindi wa "popular vote".

Kila jimbo lina "ikulu" yake (state capitol), na hapo ndipo "wachaguzi" kutoka kila jimbo hukutana Desemba kupiga kura zao. Masanduku ya kura walizopiga hufunguliwa mwezi Januari katika kikao cha "Baraza la Wawakilishi". Iwapo katika matokeo kutakuwa hakuna mgombea mwenye kura nyingi, au wagombea wawili watakuwa na kura sawa, Baraza la Wawakilishi litamchagua Rais miongoni mwa wagombea watano wenye kura nyingi zaidi. Kila jimbo hupewa "kura za wachaguzi" (electoral votes) kulingana na jumla ya maseneta na wawakilishi. Kiwango cha chini kwa kila jimbo ni kura tatu. Majimbo makubwa huwa na kura nyingi kwa vile uwakikishi katika Baraza la Wawakilishi hutegemea idadi ya wakazi katika jimbo husika. Tukirejea kwenye matokeo ya uchaguzi, Trump alipata kura za “wachaguzi” 290 huku Hillary akiambulia 228. “Wachaguzi” katika kila jimbo watakutana Desemba 17 kupiga kura zao, huku matarajio makubwa yakiwa wataheshimu jinsi wingi wa kura za “wachaguzi” alizoshinda Trump.

Kwa hiyo japo kinadharia kuna uwezekano wa “wachaguzi” hao kuamua kumnyima kura Trump na badala yake kumpa kura hizo Hillary, hali itakayosababisha matokeo ya uchaguzi huo kubadilika, uwezekano huo kiuhalisi ni mdogo mno. Hivyo kutokana na mfumo huo wananchi wengi walimpigia kura Trump kumpatia wajumbe wengi wa electoral college ili wajumbe hao waweze kumuwezesha Trump kifika ikuru ya White house. Kumekuwa na watu wanaojiita wachambuzi wakiwadanganya watu eti "Mfumo mbovu wa uchaguzi marekani ndio Tatizo" Mara ohhh!! wanadai "Clinton ndie aliepata kura nyingi za wananchi hivyo ndio chaguo la watu" lakini hao usahau kuwa marekani RAIA upiga kura mbili siku ya uchaguzi kwanza... "upendekeza nani wangeona anafaa kuwa rais Wao" kimsingi kura hii haina maana yoyote sababu hii ni mapendekezo tu yatakayo wapa mwanga wajumbe maalumu wa electoral college kwenye maamuzi ya kura zao wakati watakapo kutaka tarehe 17 ya mwezi December. Na katika kura hii ya mapendekezo ndio Clinton alipo ongoza kwa Karibu 49.4% ..... Lakini kura ya Pili ni ile RAIA hao hao wa marekani hupiga kura kuchagua majina ya wajumbe maalumu wa electoral college ambao wamekuwa wakipendekezwa na vyama vyao kwa kwenda sasa kufanya chaguzi wa nani awe rais wao rasmi Hapa sasa ndio RAIA uchagua hao wajumbe kwa minajili ya wajumbe hao kwenda kumchagua raisi Wao kama nilivyo eleza hapo juu. katika hadhila hii ndio wananchi walichagua wajumbe wengi wa upande wa Trump kwa kuwa waliamini "Trump ni chaguo la masrahi ya taifa lao na Clinton ni pendekezo la Demokrasia yao"

Mbali na hapo kumekuwa na watu nje ya marekani wameona masrahi yao ni bora kuliko ya wamarekani kwa kuwa tu Trump kuonekana kupuuza mambo ya mataifa yao na kutimiza ya nyumbani mwake (Meke America Great Again) sasa tujiulize kiongozi yupi mzuri kati ya yule anayemulika maswala ya nyumbani kweke au yale ya nje na kuwa Acha wanae nyumbani hoihahe? Na ni kipi bora kati ya kuanza kumulika miguuni mwako ung'atwapo na nyoka? Ndio hata Uingereza wana msemo usemao "Charity begin at home" na hii ndio siasa ya Trump. Hata sisi Afrika tunayo haja ya kujifunza siasa ya kuwekeza Sera zilizo na masrahi pana nyumbani. mimi nina imani siasa za kutazamia maswala ya nyumbani ndio siasa bora kwa usatawi wa taifa lolote duniani... Mfano mzuri ni Taifa la China.

Sasa Baada ya kutazama hilo la kwanza hapo juu Labda sasa ni vyema Leo kwa kina kabisa nikubainisha ni kwanini nilikuwa team Trump, Na kwanini nilisimama kidete kumuunga mkono?...

Kwanza kama nilivyoanza kueleza Juu kabisa kuwa katika hoja hii lazima tukumbuke kauli hii "Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili kwa mwanadamu yoyote".... Hivyo ili Afrika tuwe mtambuka lazima tukutane na dhana kinzani ambayo itatufanya tufanye mabadiliko makubwa kistratejia Kwa miongo kadhaa Afrika tumekuwa tegemeze Karibu kwa kila kitu kutoka marekani. Sasa nadhani ni kipindi cha Afrika kuamka kuanza kufikilia kupokea mageuzi ya kistratejia ili kujijenga katika dhana ya kujitegeme nakumbuka mafanikio makubwa ya taifa la Israel ya leo ni matokeo ya hii iliyo semwa na Rais wa kwanza wa taifa hilo David Gurion alisema "If you don't want to be corrected then your stupid" ndio maana Leo taifa hilo limepiga hatua baada ya kupitia ugumu wa manyanyaso ya mda mrefu. Hivyo Trump kabainisha wazi kuwa katika serekali yake jambo la kutenga fedha kwa ajili ya Afrika halitakwepo hivyo Afrika wajitegeme wenyewe. Sasa Afrika watafute fedha kupitia raslimali zao. Nadhani kwa mda mrefu viongozi wa Afrika walikuwa wakiifanya marekani kama kisingizio cha maendeleo yao... Mara utawasikia wakisema "Miradi mwaka huu umesimama kwakuwa wafadhili wetu mara wamesimamisha mfuko wao" mara ohh!! Fesha za wahisani zimechelewa Sasa Trump kasema nchi yake isiwe kisingizio kwa maendeleo ya bala la Afrika wote tunajua kuwa hakuna bala lenye rasilimali nyingi kuliko Afrika lakini rasilimali hii imekuwa ndio kichocheo cha vurugu na machafuko yote Afrika na ndio maana Trump Mara kadha alikuwa akimkosoa Obama kuwa kitendo cha kuivamia Libya ni kosa kubwa katika ustawi wa AFRIKA na alikwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa AFRIKA ingekuwa Salama kama Ghadafi angekuwa hai. Hivi kwa msingi huu kwanini ni siwe team Trump?

Mara kadhaa Trump amekuwa akilaani utawala uliopita wa marekani hasa chini ya Bush na Obama kuendelea kufadhili makundi ya waasi kama UNITA kule Angola, TING kule Chad, Lenamo kule msumbiji, waasi wa BIAFRA kule Nigeria, na vuguvugu la Arabic uprising hivi majuzi kule Afrika kaskazini kuanzia Tunisia,Algeria, Libya na Egypt. Afrika kuchochea vita vya ndani ikiwa ni pamoja na kulaani utawala wa kidikiteta yani wale viongozi wa mda mrefu pamoja na kuwaonya kuwa iwapo atashinda atawashugurikia ipasavyo wakina museveni, Mugabe, na wengine wanao tumia nguvu katika uvunjifu wa Demokrasia. Katika utawala wake Trump kakili kamwe kuwa hato wavumilia kabisa viongozi madikiteta. Hivi kweli nishindwe kuwa team Trump?.

Katika kipindi chote Trump amekuwa akilaani viongozi wa Afrika kuficha fedha za umma nje ya bala la Afrika hii ni aiubu kwa viongozi wa Afrika na ndio maana Trump aliwakumbusha viongozi hao kuwa wategemee kukutana na mazuio ya account zao.. Huko walizo zificha. kweli utasema Trump sio mkombozi wa Afrika? Pamoja na yote hayo Bado Trump alitoa kauli elekezi kwa Afrika kuwa "Afrika lazima ijitegemee kama hamtoweza kujitawala wenyewe basi kuna haja ya kutawaliwa tena" ndivyo Trump alisema mara kadha kila alipoulizwa maswali Juu ya muelekeo wa serekali yake kwa AFRIKA. Amekuwa akisema kuwa sisi Afrika ni wavivu wapenda ngono na wajinga binasfi nakubaliana na maneno haya kwani si juzi tu utafiti moja umebainisha kuwa kati ya watanzania wanne mmoja ni kichaa? kwani si ndio Afrika rushwa imekuwa dhana ya kununua uongozi? Na sindio Afrika ndio raia kwa asilimia kubwa wamekuwa wakithamini rushwa Karibu kwa kila kitu hasa wakati wa uchaguzi na huku wakijua madhara ya rushwa? Na kusahau kuwa Pesa haina thamani kuliko utawala wa kusimamia umma?

Hivi sindio Afrika viongozi wamekuwa wakivunja sheria na katiba za nchini zao kwa masrahi yao binafsi? Kwani si Burundi juzi tu Khurunzinza kumeshuhudiwa mauaji ya rai kwa yeye kutaka kusalia madalakani?. kongo-DRC si juzi tu tumesikia tuliyoyasikia kwa Kabila kung'ang'ania madalakani, hatujasahau sudani, Rwanda, Liberia, Mali, Zimbabwe na Afrika ya kati kumeshuhudiwa mauaji kadhaa yaliyochagizwa na viongozi Wao. Na sindio afrika uganda raisi mseveni anatuhumiwa kutembea na mke wa daktali wake Kiza Besige? Na ndio Afrika rais Sani Abacha wa Nigeria alikufa kifo cha aibu chanzo cha kifo chake ni kumeza vidonge vya Viagra? Utaniambiaje AFRIKA sisi sio watu wangono? Hivi Bado tutasema wafrika wanaakili? Sio wavivu? Na sio wapenda ngono? Trump ni msema kweli na "msema kweli daima uchukiwa"

Nikweli marekani imekuwa taifa ajizi katika kuvuruga amani ya ulimwengu ili yenyewe iweze kunufaika katika ushawishi wa kidunia na asilimia tisini na Tisa 99% ya viongozi wote Afrika ni vibaraka wa USA pamoja na hiyo ilikuwa ni ngumu sana kwa mataifa ya AFRIKA kujinasua kutoka kwenye ajizi hiyo kutokana na Sera ya marekani kuwekeza katika siasa za mambo ya nje, lakini serekali ya bwana Trump ni tofauti kidogo yeye anaonekana kujihusisha na maswala ya ndani ya nchi yake kwa madai yakwamba eti taifa lake limekuwa likipoteza mabilioni kuwekeza nje huku mwake kukiangamiaa kiuchumi...na ndio maana kaanza kutishia kuwa utawala wake utajiondoa kwenye NATO, PTA, world climate change na hata kupunguza ushawishi wake UN. Kwa kufanya hivyo atainusuru AFRIKA kwa maana sasa mitazamo ya bwana mkubwa huyo Juu ya AFRIKA na ushawishi wake utakuwa umepungua hivyo AFRIKA itabaki Salama.

Katika eneo la Pili ni bala la Asia, huku kumekuwa ndio muathilika mkubwa wa katika ubeberu wa marekani kwanza katika migogoro ya kisiasa pili ni kwenye eneo la kiuchumi na hii imekuwa ikisababishwa na ajizi ya ushawishi wa marekani katika bala hilo, wote ni mashahidi wa vita ya Afghanistan kwa kile kilichoitwa Talibani, Iraq na Saddam Hussein, Parestina na migogoro ya Israeli na hamasi, Jordan na Israeli, mara Qatar na sasa mivutano ya nyukilia wa Irani yote haya ni marekani kujiimalisha kihimaya na kidola katika eneo hilo. Siasa ya eneo la mashaliki ya kati imekuwa na sura pana hasa marekani kuifanya eneo hilo kuwa kipaumbere mamba moja kwa sababu kadha wakadha
Kwanza ni kudhibiti himaya ya kiarabu yenye msingi wa Dini ya uislam na ndio maana mara kadha Trump amekuwa akiwashutumu waislam na kuwakabili dhidi ya sera ya wahamiaji wa Kiarabu kutoka huko mashaliki ya kati kuingia marekani yote haya ni kutokana na kile kinachoitwa kudhibiti kuimalika kwa himaya yakialabu Uislam- kialabu toka kusambalatishwa kwa ile iliyokuwa ikiitwa Ottoman empire hivyo toka mwaka 1922 na baadae mwaka 1967 na kisha mwisho wa mikakati madhubuti wa kuisimamia dunia wa mwaka 1987 (world strategic metropolitan plantform) uliosainiwa kule Tel Aviv baada ya kuandaliwa Washington tarehe 23/8/1985 katika mkataba huu iliwekwa mikakati ya kuidhibiti dunia kupitia himaya ya marekani. Hivyo katika siasa za hivi Karibu kumeibuka hali ya sintofahamu kwa kile Trump alichokiita kuwa marekani tena haito fadhili waasi wa IS na makundi mengine kwani Trump amedai kufanya hivyo ni kuchochea na kuvurugika kwa uchumi wa marekani kwani imekuwa ikitumia Pesa nyingi kushugurikia dipromasia ya nje.
Katika hali hiyo Trump amekuwa akidai kuwa Iraq ingekuwa Salama kama Saddam Hussein angelikuwa hai na dunia ingekuwa Salama kama mashaliki ya kati ingeachwa ijiamulie mambo yake yenyewe. Najua kwa kuiacha mashaliki ya kati kwanza vita vitakama sababu ajizi ya USA haitokuwepo Pili usalama na usatawi wa amani utaimalika kwa sababu misukomo ya kibeberu haitokuwepo. Kumekuwa na mararamiko kuwa Trump kaweka marufuku kwa watu weusi na waislam kutoingia marekani mimi nadhani hilo ni jambo la busara maana huku kwetu kumekuwa na kasumba za vijana wote kuwaza ndoto ya kuishi marekani na kushindwa kubaki mwakwao kujishugurisha na shuguli za kiuchumi. Hata waislam kwani ni lazima waende marekani? kwani nini wanachokosa huko makwao mpaka uwe ni lazima kwenda marekani? Mimi nadhani lazima tubadilike sasa tuanze kuona mambo yetu ni ya msingi kuliko hayo ya wamarekani tuone kuwa halina haja ya kujifunza au kuishi marekani najua China wamefanikiwa kwa sababu ya msingi ya kujenga dhana ya kustawishwa nyumbani ( build home) kwa kufanya hivyo ndio tutakuwa tumeondokana na utumwa wa akili na kujitawala kifikra.

Tatu sasa AFRIKA na Asia ni wakati wa kufanya Mapinduzi ya Kifikra (Conceptional Revolution) katika kufanya Mapinduzi makubwa ya kifikra ni katika kutambua kuwa marekani sio mbia wetu wala rafiki yetu wa kweli Bali yeye ni rafiki yetu sababu tu anachuma rasilimali yetu pale kwenye masrahi yake na kumbukumbu AFRIKA haijafutika katika kuona ni Namna gani marekani imekuwa ikichochea umwagaji wa damu AFRIKA toka mwaka ya 1960 kwa kufadhili kuuwawa kwa Patrice Lumumba kule kongo-DRC, kuhusika katika mauaji ya Sylivanus Olimpio kule Togo, kuchochea mauaji ya Agustino Neto kule Angola kwa kumtumia Jonas Savimbi, kusimamia kupinduliwa Nandi Azikiwe wa Nigeria mwaka1966, kufadhili Mapinduzi ya Nkhurumah pale Ghana, kupanga na kutekeleza mauaji ya Samora Machel na kupinduliwa kwa Haile Serasie wa Ethiopia. haitoshi miaka ya 1970 mpaka 1999 tume shuhudia mauaji ya kimbali Rwanda, kuuwawa kwa Kabila senior, kifo cha John Garang, vita huko Sierra Leon, Liberia, Nigeria na ivory coast yote haya ni strategies za ajizi ya marekani hakuna anaeweza kuwa na roho ya undugu na marekani zaidi ya kuwa na chuki. Kwa kipindi hicho chote marekani imekuwa ikitumia siasa za ulagha ya unafiki na kuraghai ili kuonesha kuwa wenyewe hawausiki na chochote kinachoendelea Afrika lakini kinacho nifurahisha sasa katika kampeni za Trump ambaye ameshinda amejalibu kuonesha wazi kuwa Wao hawana undugu wa urafiki na taifa lolote na kila taifa lijitegeme lenyewe.

Kitendo cha marekani kubainisha kuwa hawitaji wahamiaji haramu wa kiafrika maana yake ni kuwa sisi tubaki kwetu tusaidie kukuza uchumi wa mataifa yetu. Katika kubainisha ukweli kuwa sisi ni watu wa hovyo kwa maana ni wapuuzi, wajinga na wapenda ngono tusi Hili linatosha kuwa funzo kwetu katika kupokea mabadiliko ya kiutambuzi na kuanza kuwa binadamu "mtambuka". mimi ninachojuwa ni kuwa *"Kumtambua adui Wako ni kushinda vita tayali"* hivyo sisi kama Afrika lazima tujue hivyo kuwa rafiki waliomtegemea ndio adui mkuu alio watafuna kwa miaka mingi na sasa ndio wakati wa kuanza kujinasua kwenye minyororo na kuishinda hii Vita ya Ukoloni mambo leo

Siasa hii ya uhafidhina iliyodhilika na kutamala kwa kasi katika mataifa ya kibepari (World Of Capitalism) imeanza kushika hatamu sasa katika mataifa yote makubwa duniani na hii ni kwa sababu dunia sasa inaanza kupokea athali za umajumui wa Kijamaa (Pan-world Socialism) hasa hasa kutoka China taifa linaloanza kijiimalisha katika kuidhibiti dunia hivyo viongozi wa mataifa wa kibepari wameanza kupata vizingiti ndani ya nchini zao kwakua mataifa yao kuonekana kupoteza gharama kubwa kushugurikia mambo ya kimataifa kama Vita na mapambano ya nje, Wahamiaji halamu, Sera za kibiashara, kuongezeka ushawishi katika kushugurikia masuala ya nje huku ndani ushugulikiaji ukidorora. Muktadha huu ndio umeweza kuvutia kuungwa mkono na sehemu ya hadhira, kupandikiza hasira ili kuipa nguvu hadhira kuchukua hatua hata kama zinapanda athari.

Kwa ujumla, Aina hii mpya ya siasa Kwa upande mwingine, ndio iliobadilisha hali ya mambo na kutoa ushindi wa kambi iliyotaka Uingereza ijitoe EU (kupitia hoja zao za kupandikiza chuki) na ushindi wa Trump huko Marekani ni ujio wa mapinduzi ya kimfumo; upinzani wa umma dhidi ya tabaka la wanasiasa, wasomi na taasisi za kisiasa na uchumi. Hii ingepaswa kuwa habari njema kwa AFRIKA pia kupokea mabadiliko hasa sasa kuanza kungana ili kujenga dhana ya Africanism ili sasa tupambane na uonevu,chuki,ukandamizwaji,unyonywaji na ubeberu ambo sasa wanasiasa hao wapya wemeonyesha kuto shiliki tena katika mambo yetu wanasiasa hao wanataka kujikita zaidi kwenye siasa zao za ndani. Na ndio maana mara Trump alipo shinda tu Obama akaamua kwenda Ujerumani ili kuipa jukumu taifa hilo kuendeleza siasa za kuinyonya dunia kwa masrahi yao.

Na kufanya hivyo ni kwa sababu tu ni kwamba wanaoendesha kampeni ya mapinduzi haya ya kihafidhina ni wanasiasa hatari kabisa katika nchi zao na kimataifa. Hasa katika kupambana na mataifa makubwa na siasa za ndani. Na ndio maana hata katika hatua hiyo tumeshuhudiwa kwamba Ushindi wa Trump umepokelewa kwa shangwe kubwa na viongozi wa vyama vya kisiasa vya kibaguzi na vyenye mrengo mkali wa kulia, kama Marine LePen wa Ufaransa, Victor Orban wa Hungary, Frauke Petry wa Ujerumani, Heinz-Christian Strache wa Austria na Geert Wilders wa Uholanzi. Na kwa Uingereza, mwasisi wa harakati za nchi hii kujitoa EU, Nigel Farage, amekuwa mwanasiasa wa kwanza wa nchi hii kukutana na Rais-Mteule, Donald Trump. Katika kumpongeza na kupeana mikakati kadhaa.

Mwisho japo sio kwa umuhimu wake ni vyema kwanza tukatambua kuwa "Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili kwa mwanadamu yoyote" na ndio maana katika maisha inapotokea dhana kinzani ya mazoea yakawaida mwanadamu huwa anapokea mabadiliko kadhaa kama wataalamu wa fizikia wanavyoeleza ( any reaction is equal opposite......) Kwa maana hii bila kuwepo ubaguzi wa rangi kule marekani miaka ya 1933-1970 enzi za harakati za maltin Luther king Leo hii Obama asingekuwa raisi mweusi wa kwanza kuongoza taifa kubwa kiushawishi duniani. Na kama kusinge kuwepo ubaguzi wa rangi kule Afrika ya kusini Nelson Mandela asingekuja kupata heshima duniani alionayo Leo..... Hivyo mimi naamini kupitia siasa hizi Kali za mlengo wa kushoto zitazaa kitu kikubwa Afrika na Asia hasa hasa bata Arab.

Katika kutamatisha makala hii Juu ya kile nilichoona katika siasa na mustakabali ya siasa za marekani batani AFRIKA na Asia ni kwanamna nilivyo eleza hapo Juu sasa ebu tushilikishane mawazo Juu ya huu mtazamo wangu.....

"Mungu ibriki Afrika na Asia, Mungu ibariki Demokrasia ya Afrika na Asia"

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu

copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
 

Forum statistics

Threads 1,272,952
Members 490,211
Posts 30,465,665