Tsh bilioni 208 kutumika kujenga Mahakama za Mwanzo 60 mpya Tanzania

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
995
2,695
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Profesa Elisante Ole Gabriel amesema zaidi ya Tsh bilioni 208 zimetengwa kujenga Mahakama za mwanzo 60 na vituo jumuishi vya haki 12 katika mkakati wa maboresho ya awamu ya pili ya kufikisha huduma za Mahakama vijijini.

Profesa Gabriel alibainisha hilo walipofunga kikao kazi cha kujadili mapitio ya mpango mkakati huo akibainisha kuwa kuna vituo jumuishi vya mahakama sita na Mahakama za mwanzo zaidi ya 960.

"Mahakama za wilaya zipo 120, za hakimu mkazi 30 na za kanda ni 18. Watanzania wategemee maboresho makubwa katika utoaji haki wenye uwazi, wakufikika kirahisi na wenye ubora unaofaa," alisema.

Alisema maazimio ya kikao hicho ni kuhakikisha kunakuwa na ushirikishaji wa watu katika ngazi zote katika utendaji kazi wa mahakama.

Kwa upande wake, Dk Angelo Rumisha alisema maboresho hayo yalianza tangu mwaka 2015 na katika awamu hii ya pili uboreshaji ni mkubwa.

"Hadi mwaka 2024 tunakusudia kuanzi sha huduma za Mahakama Kuu katika mikoa yote ya Tanzania kutoka mikoa tisa ya sasa," alisema Dk Rumisha.

DK Rumisha alisema kwa sasa wanatoa huduma zinazomlenga mwananchi kwani upo mpango wa mahakama kuwafuata wananchi kupitia mahakama zinazotembea zikilenga kufikisha elimu ya utoaji haki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom