Kama kawaida nchi hii ni mwendo wa kula tu, Fedha za wavuja jasho wa nchi hii zinaliwa tu kiurahisi rahisi na hakuna mtu wa kuhoji na hakuna mtu atakayechukuliwa hatua. Ndio maana ukarabati wa magogoni hautakaa uishe.
Matukio kama yako mengi! Nafikiri huu ni Ukiukwaji wa Uadilifu na maadili mema ya Kijamii na kitaifa! Viogozi wakishindwa kuyasemea haya ... Wataaminikaje ..kuja kuusema ndoa za jinsia Moja?
Mkuu Azimio Jipya kila ukisoma hapa unapata jipya ambalo lionazidi kukuumiza kichwa
Leo tena ile hela ya EPA kuna kampuni zimeikwapua karibu Bil 20 na hazina mpango wa kurudisha
Aliyekuwa kwenye kitengo cha EPA enzi hizo BOT ndio yeye yeye alioletewa pesa hizo eti za kuendeleza kilimo kwanza TIB na kakopesha makampuni ambayo hayana uwezo wa kulipa .Mtuhumiwa unamkabishi the same money iliyosemekana alioversee kutolewa kwake
Na ndio maana hawa wazungu wanatuona hamnazo wanatupa masharti ya ajabu maana wanaona akili hatuna
Soma sehemu ya gazeti hili. Heri tubaki masikini.... Ili KUSIMAMIA UTU NA MAADILI YA MTANZANIA ... Mbona kichekesho ... Kufujwa kwa Hizo fedha za EPA ... hakuonekani na kuchukuliwa kuwa ni janga ya kupotea kwa MAADILI YA UTU NA MAADILI YA MTANZANIA?
MEMBE: HERI TUBAKI MASKINI
na Tamali Vullu
RAIS Jakaya Kikwete amekataa kumpokea balozi mpya kutokanchi moja ya kigeni baada ya kubainika kuwa amefunga ndoa na shoga.
Siri hiyo iliwekwa wazi jana na Waziri wa Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa Benard Membe alizungumza na waandishi wa habarikuelezea msimamo wa Tanzania kuhusiana na kauli ya Uingereza ya kuzitaka nchizinazopokea misaada kutoka nchini humo kuhalalisha vitendo vya ushoga.
Membe alisema tukio hilo lililomshtua Rais lilitokeamwanzoni mwa mwaka huu, pale alipopokea barua kutoka nchi moja (hakuitaja)ikimtaka wampokee balozi wao mpya na mkewe, lakini walipobaini kuwa mke huyo nimwanaume Rais Kikwete alikataa.
Alisema baada ya kugundua hali hiyo, Kikwete akiwa haaminikile alichokisia alitamka maneno machache "Toba Yarabi" na kuagiza balozi huyoasikubaliwe kabisa. Waziri huyo alisema hata baada ya nchi hiyo kukataliwa,ilibembeleza sana kwa siku kadhaa ikidai kuwa kusingekuwa na madhara yoyote kwabalozi huyo kufika nchini na mke wake (shoga) na kwamba angetimiza wajibu wakekikamilifu. "Waling'ang'aniamsimamo wao, lakini baada ya siku nne walituelewa na kusema kuwa sisi nimarafiki wao na hivyo waliheshimu msimamo wa Tanzania na kuahidi kuwawasingemleta tena balozi huyo na mkewe," alisema.
Membe alisema amelazimika kusema jambo hilo kuonyesha kuwaTanzania inapinga kwa nguvu zote tabia za ushoga na kueleza kuwa haiko tayarikutunga sheria ya kuruhusu ushoga nchini.
Akizungumza kwamkazo, Membe alisema Tanzania iko tayari kwa lolote na hata kubaki na umaskiniwake kuliko kupokea misaada yenye masharti ya hovyo.
"Tunataka kutunzaheshima yetu. Kama wanadhani misaada itatolewa kwa masharti hayo wakae na fedhazao, hatukubali kutekeleza jambo hilo," alisema.
Akiungana na viongoziwa dini walioitaka serikali isikubali wala kutishwa na nchi hiyo, Membe alisemaTanzania haiwezi kutekeleza sharti hilo
hata kama ni maskini na itaendeleakuheshimu misingi ya maadili ya taifa inayokataza mambo ya ushoga.
"
Hii ni nchi inayofuata maadili na haiko tayari kupokeaushauri katika suala hilo...hata nchi ikiwa kubwa kiasi gani, linapokuja sualala utaifa, hatutakubali kuyumbishwa hata kidogo," alisisitiza Waziri Membe.
Waziri Mkuu waUingereza, David Cameron, hivi karibuni alitishia kusimamisha misaada kwa nchizinazopinga haki za mashoga na kuzitaka zile zinazopokea misaada kutoka nchinihumo ikiwamo Tanzania zikubali sharti hilo.
Membe alisema kuwa staili ya sasa ya kuunganisha misaada nasuala la ushoga ni tamko hatari ambalo linaweza kuvunja uhusiano na nchinyingine.
"Tamko hili linawezakuvunja Jumuiya ya Madola na ikitokea ikawa hivyo, Waziri Mkuu wa Uingerezaanapaswa kuwajibika," alisema Waziri Membe.
Aliongeza kuwa katiya nchi 54 za jumuiya hiyo, 13 pekee ndizo zinazounga mkono suala hilo na kuonyakuwa suala hilo si la kushabikia hata kidogo. Hata hivyo, waziri huyo alisema suala hilo halikuwa ajendakatika mkutano uliomalizika hivi karibuni nchini Australia, bali Waziri Mkuuhuyo aliibua katika vikao vya viongozi wakuu wa nchi.
"Suala la ushoga halikuwa ajenda na wala halikuzungumzwakwenye mkutano ule; alichofanya Waziri Mkuu huyo ni kuibua suala hilo katikavikao vya viongozi walipokuwa wakijadili haki za binadamu. Hii ndiyo sera yachama chake cha Conservative.
"Hata hivyo jambo hilo lilikataliwa na lilipofika kwenyemkutano walizungumza kwa mafumbo, lakini tulikataa," alisema.
Alisema sheria za nchi za mwaka 1971 ambazo Tanzaniaimeziridhia kutoka kwa Waingereza zinakataza suala hilo na kutamka kuwalinapofika suala la ndoa au mahusiano ya kimapenzi linahusisha watu wa jinsiatofauti.
"Wote tunajua msingi wa familia ni mume na mke ambaowanaweza kuzaa watoto...pia sheria ya makosa ya jinai inaeleza msimamo ndiohuo, hivyo kwenda kinyume ni makosa ambayo mtu anaweza kufungwa kifungokisichopungua miaka 30 jela," alisema na kuongeza kuwa kwa msimamo huo serikalihaivitambuia vikundi vya kishoga vilivyoko nchini.
MY TAKE
Ni kweli hapa Tanzania kwa sasa kuna Utamaduni wa kutetea MAADILI YA KITAIFA ... kwa hali yeyote ile hata ikibidi kuukubali kuyafia? Kwani kudiriki kusema kuwa hata kama ni kuwa UMASIKINI na tuwea lakini UTU KWANZA, UBINADAMU KWANZA NA UZALENDO KWANZA ....haya ni ya kweli?
Waziri anaamini kwa anachokisema?