Mtu asipo kuwa mwaminifu kwa kitu kidogo jua majanga hayo
ha haaaa, ukiona hivi ujue nina mpango wa kuaga naenda kwa mjomba kwa muda wa wiki 2.Hahahaaaaaa!!! Leo sijui FP umeamkia wapi dada yangu?
Vipi dada unaenda kwa shangazi au kwa kaka?
Back to topic.
Uaminifu umekuwa ni kitu hadimu sana katika maisha yetu ya kila siku. Ni watu wachache sana ambao katika maneno yatokayo mdomoni mwao kila neno huwa la kweli. Watu tumekua na udanganyifu katika maisha yetu ya kila siku, hii inatokana na jinsi tulivyojichagulia kuishi.
Binafsi nimekua mdanganyifu pale ninapoona mambo yanakuwa magumu, ila naamini sio mimi tu, tupo wengi wenye tabia hii ya udanganyifu.
Mfano:Mmeahidiana na Boss wako mkutane mahali fulani kwaajili ya kitu fulani, ila muda unakwenda halafu unakuta Boss amefika kabla yako na anapokupigia simu kukuuliza uko wapi? Unamjinu upo maeneo ya karibu na pale mlipoahidiana mkutane, wakati unawezakuta hiyo simu aliyokupigia Boss wao ndo imekukumbusha kwamba mlikua na appointment.
Hapo tunaona udanganyifu unaweza kukusaidia kufanikisha dhumuni mlilokuwa mnataka mlikamilishe au inaweza kukufanya upoteze uhusiano mzuri na wenzako pale utakapomdanyanya na akakusubiri kwa kipindi kirefu nila wewe kutokea.
Tumuomba Mungu atuomdolee tabia ya udanganyifu akilini mwetu huku nasi tukihjitahidi kujifunza kusema kweli ambayo itatuweka huru.
ha haaa, mimi sijui kwa nini sitishikagi na x. nipo hivyoHmmm...lakini kweli aisee. Manake ukimweleza mwenzio anaweza akapatwa hisia zisizo kabisa na kuzusha sokomoko lisilo na kichwa wala miguu. Yaani haya mapenzi haya...
Kuna tija kuyasema hayo yote?Hata ukimkuta Juma/Amina njiani bora useme kama mlikutana na kuzungumza zaidi ya salam tu
Bora ajue unamwambia ukweli japo hampendi hiyo rafiki, kuliko kuonekana unaficha ficha
ha haaa, hiyo kali.....
kuna mkaka alipigwa kwara na mkewe asionane na mimi. mimi nikamwambia kwa kweli naheshimu sana ndoa za watu, mimi nawe hatuna chochote kitakachoharibika kama hatutakutana, nikamwambia tusionane tangu hiyo siku. Kuna siku tulionana barabarani na tukasalimiana, sasa sijui alienda mwambia mkewe kuwa tulionana? lol!
una sababu ya kudanganya ingawa siyo ya lazima saana......Nadhan ukiwa na mtu mwenye mawivu ivi vtu vinakuwepo kupunguza maugomvi .hata mimi huwa nadanganya coz my bf anamaswali ya kero yanayopelekea tugombane.et"kila cku kwa aunt yako mnaendaga kuongea nini"mtu wa ivi lazma udanganywe cjui hamjiamini yan mnakera ndo sababu.
ha haaaa, hao ni wa kuwaambia, akikudanganya unamwambia kabisa hapa dada umedanganya, ataona aibu ukishamwambia mara 27 atapunguzamimi mdada wangu ananayenisaidia home!uuuuuuuwih!anadanganya kila kitu!anaweza akaulizwa uko chumbani hachelewi kusema alitaka kwenda maliwato!eheehehhehhehe nishamzoea lakini hii tabia inanikera sana kwa kweli!zitu vingine yuko poa hadi raha!ila mwongo jamani! uuuuuuwih!sijui nafanyaje!
kweli unapaswa kufanya kitu ambacho mpenzi hakipendi? ndo utajiona unampenda?Unapoamua kusema uongo, mara nyingi unajaribu kutokumuudhi mwenzako kwa suala ambalo unajua hapendezwi nalo. Unakuwa unajua kwamba ukimwambia ukweli .. kwa kitu ambacho hapendi ataudhika, hivyo unadanganya. lakini madhara ya uongo ni makubwa zaidi kuliko kama ungemweleza ukweli, ingawaje pia angechukia.
Kuna tija kuyasema hayo yote?
ha haaa, mimi sijui kwa nini sitishikagi na x. nipo hivyo
akikutana naye huwa ananiambia tu na sometimes anampigia akiwa naye namsalimu na kumwambia anichungie asiibiwe na watu, lol!
ha haaa, hapo tunakubaliana na mimi kabisa.... kama una sababu inayokufanya ukadanganya kwa "mambo ya kawaida" ndo hivyo, otherwise sioni kabisa sababu@FP,
Hakuna mtu anayesema uongo bila ya kuwa na sababu...No, NEVER...!
Halafu pia, ni vigumu sana "kusoma ubongo" wa mtu mwingine, so, swali la "kufikiri" kuwa "x" nikimwambia hivi "atanielewa" siyo kweli hata kidogo. Na ndiyo maana unachoita "mambo ya kawaida", si sawa, hakuna "mambo ya kawaida".
Uongo mwingine unatengenezwa na mazoea katika mahusiano, na ni vizuri uwepo ili "kupitisha siku"...!
"Chakula tayari"? haiwezi kujibiwa na kauli ya "bado"....!
"Upo wapi"? haiwezi kujibiwa na kauli ya "nipo gesti hausi"...!
"Unafanya nini"? haiwezi kujibiwa na kauli ya "nina-do"...!
"Watoto wameshakula"? haiwezi kujibiwa na kauli ya "bado"...!
Kuna swali ambalo unaulizwa, na unajibu bila hata kufikiria, kwa maana unafahamu yule aliyekuuliza anataka jibu gani...!
Ukiona mtu anakudanganya kwamba anaenda sehemu fulani kumbe haendi huko bali anaenda kwengineko, basi wewe mke utakuwa na negative attitude na hiyo sehemu (labda hamuelewani vizuri na wifi zako) sasa anahisi akikwambia anaenda huko utakasirika na utahisi kana kwamba atakwenda kujazwa maneno ya kinafiki ambayo yatahatarisha ndoa yenu, na mfano wa hivyo.. Mimi mawazo yangu ni kwamba wanandoa hawatakiwi kuwa na "conflict of interests" muwe kitu kimoja murekebishe penye tatizo, basi kudanganywa hakuna tena.Poleni na majukumu wanaMMU...
Leo hili jambo la trust kwenye mahusiano limekuwa likijirudiarudia sana katika kichwa changu. Mahusiano mengi sana yanavunjika sababu ya kukosa uaminifu. Kuna vitu vingi nimekuwa nikijiuliza na kujijibu na vingine kukosa kabisa majibu. Kwa mtazamo wangu UAMINIFU ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Mara nyingi napenda sana niwe katika hali ambayo namuamini mpenzi wangu, pia napenda sana kwa gharama yoyote ile kumfanya mpenzi wangu aniamini. Kama nikigundua ana wasiwasi na kitu ninachomwambia huwa najitahidi kumwuliza aniambie nifanye nini ili aniamini sababu sipendi akae akiwa na wasiwasi, na ukweli nitafanya hicho kitu ili tu aridhike.
Inawezekana mimi nipo complicated kidogo, huwa napenda sana mtu aniambie ukweli hata kama ni mbaya kiasi gani. Kwa kuujua ukweli nakuwa na uhuru wa nini la kufanya baada ya hapo.... kukusamehe na kuendelea na mahusiano au kukusamehe na kusitisha mahusiano (kusamehe kwangu huwa siyo option, lazima nisamehe ili niweze kuendelea na mambo yangu mengine).
Katika huu uzi nitazungumzia sana uaminifu wa mambo ya kawaida tu, siyo kutoka nje ya mahusiano (cheating). Utakuta sometimes mtu anaamua tu kudanganya kwa sababu yoyote anayoijua. Kwa mfano mtu anamwambia mpenzi wake naenda sokoni wakati anaenda salon, au naenda kwa dada wakati anaenda kwa shangazi.
Hivi ikatokea ndo upo kwa shangazi halafu dada akaja nyumbani kukuulizia wakati wewe uliaga kwenda kwa dada itakuwaje? hata kama kweli mpenzi ataamini kuwa ulikuwa kwa shangazi, utakuwa umejenga hisia gani kwake kuhusu wewe? kwa nini umdanganye?
Wenzangu mnalizungumziaje hili?
Karibuni kwa mjadala
ha haaaa, ukiona hivi ujue nina mpango wa kuaga naenda kwa mjomba kwa muda wa wiki 2.
hizi simu za mkononi ndo nazo zimeleta janga kubwa sana la uongo..... watu wanadanganya sana location. mi nadhani sasa ile ambayo wanatumia kulocate location ya mtu iwe ina-reflect kwenye simu zetu, i.e. nikimpigia mtu niwe nina uwezo wa kuona yuko wapi naye aone niko wapi........
Halafu hii ya kuaga unaenda kwa shangazi kumbe unaenda kwa dada sio nzuri kabisa kiufupi uongo si kitu chema na ukisha kosa uaminifu ni vigumu sana mtu kukuamini tena hata kama siku nyingine utasema ukweli. Hasa kwenye mahusiano ndio mbaya kabisa
ha haa, una hasira ya kudanganywa mchana kweupeeeeeeeeeee!AH!kunyonyesha huko ananyonyesha kituo!
atupishe kule!hebu aje hapa!
ish kwani hapa mbn kama nna hasira sana!
we mke mwenza hebu kuja huku!
ha haa not only good memory but also good justification......... otherwise unaumbukaKabisa. Wengi ambao wamezoea uongo ndio pia mstari wa mbele kwenye cheating. Behavior breeds behaviour. Nishaona wengine wanasema uongo hadi wanaamini huo uongo ndio ukweli. Problem with lying u gotta have a good memory...
ndo maana najiuliza kama alimwambia mkewe. mimi mume wangu hana shida na tulishaongea kuhusu hilo siku nyingi tuKama ingekuwa zaidi ya salam, mazungumzo marefu, au mnakwenda for a bite umueleze yako, alipaswa aseme huko
Manake msije mkaonekana ndio mkaonekana mlikuwa na la kuficha
ha haa, una hasira ya kudanganywa mchana kweupeeeeeeeeeee!
si ndo maana dada mkubwa nikaamua nianzishe hii mada tujuzane kwanza! labda wadau watatusaidia kupunguza hasira yetu
ha haa, binamu huo uongo wa majanga hata mimi nimesema naukubali, kwenye majanga there is no way utasema ukweli, utaonekana mwehu ukisema ukwelikatika haya maisha yetu tunayoishi kuna mazingira hayakwepeki kusema japo kauongo, la msingi ni kuwa usiwe uongo wa majanga, ili hata akija kugundua huko mbeleni ukimweleza kisa cha kudanganya angalau akuelewe kuwa nia yako haikuwa mbaya.