Trust katika Mahusiano

Trust katika Mahusiano

hehehehehehe! Mwali upo?? Ni salamu tu wangu! Salamu kwa mume wetu na wanangu!
nyie nanyi karibu nitawatimua na huyo mume wenu, ndo maana kuutwaa mnadanganywa mwili na roho, lol!
 
Niliposoma kichwa cha mada nilidhan ni ya zamani kumbe ni yajana tu
'
Dah!Jambo gumu hili,trust!!!!
ha haaa, rafiki ni jambo gumu, lakini tunapaswa kulizingatia sana
 
ha haaa, rafiki ni jambo gumu, lakini tunapaswa kulizingatia sana

Nikuambie kitu,nina zaidi ya miaka 30,lakini kwenye suala la mahusiano sijawahi kukutana na mkweli na zaidi hakuna kitu kinachoitwa trust,hakipo kabisa!
 
....... Mimi hapa ndipo nsipoelewa. Mtu kama anathamni mahusiano yake na kumjali mpenzi wake kama kuna mabadiliko ya ratiba kuna ugumu gani kumweleza?? Eh pengine ndio maana mimi huambiwa ninajiexpress sana................... and may be am dating the wrong men. Honestly sielewi. Yaani nikimweleza mtu ratiba yangu anaona kama am feeding him too much of unnecessary information!!! Labda nianze kudate hawa wa JF ambao wanaonekana kidogo ni waelewa!!:angry:
ha haaa, kila la heri best, pata ambaye mtakuwa mnajieleza wote, lol!
ukiangalia sana hapa ndo unaweza kumhisisha mwenzi wako kuwa una mambo/ajenda za siri.... kwa nini unadanganya movements? kama unaenda sokoni, sema naenda sokoni na uende sokoni........
kuna ile aga ya "natoka kidogo" bila ya kusema unaenda wapi, hiyo naona ingefaa kama hutaki mtu ajue unakoenda, ingawa kuna ving'ang'anizi utasikia "unaenda wapi"
mimi kuna muda nakuwa sijui mume wangu kaenda wapi, either anaweza kuniambia location lakini nasahau muda huohuo au anaweza kusema natoka kidogo jibu langu always linakuwa "uende salama". kizaazaa kinakuja mtu au mtoto ananiuliza baba ameenda wapi halafu natoa jibu sijui, mtu akirudia "hujui?" ndo kila kitu kinarudi sasa.... kumbe nilipaswa ku-cram....., lol!
 
Nikuambie kitu,nina zaidi ya miaka 30,lakini kwenye suala la mahusiano sijawahi kukutana na mkweli na zaidi hakuna kitu kinachoitwa trust,hakipo kabisa!
ha haaa, una mahusiano ya kudumu?
 
Last edited by a moderator:
Kutokuwa mwaminifu, uongo, na mengine ni nadhiri ya mtu kutoka moyoni mwake. Usipojenga wewe uaminifu basi ipo shida. Wapenzi wote wanawajibika katika hili na ni ngumu sana kutanabaisha tatizo lipo wapi.

Tunatofautiana toka mtu mmoja kwenda mwingine na malezi tulikotoka ndo chanzo cha yote haya. Kinachobakia ni awaye yote kujitathimini kwamba; Je, anamthamini kwa kiwango gani mpenzi wake? anaweka mzingira gani ya kuaminika na mpenzi wake? anahitaji mpenzi wake amwamini kwa kiasi gani? anataka nini toka kwa mpenzi wake ili awe wa kumthamini zaidi?

Hii yote ni kutaka kuweka mazingira thabiti na sahili kwa mpenzi wake ili maisha yapate nafuu yake......
mimi naona upo sahihi kabisa hapa......
hapo kwa RED ni muhimu sana, kujenga mazingira ya kuaminiwa........
utakuta mtu unampigia simu anakuambua nipo kwa mama wakati kwa nyuma unasikia muziki mkubwa....au kelele nyingi kama yupo disco au bar, hapo unamweka mpenzi wako kwenye mstari gani? aamini upo kwa mama wakati anasikia hizo fujo zote? mtu anawaza kwa nini ananidanganya? anaona mimi siwezi kufikiria?
 
Poleni na majukumu wanaMMU...

Leo hili jambo la trust kwenye mahusiano limekuwa likijirudiarudia sana katika kichwa changu. Mahusiano mengi sana yanavunjika sababu ya kukosa uaminifu. Kuna vitu vingi nimekuwa nikijiuliza na kujijibu na vingine kukosa kabisa majibu. Kwa mtazamo wangu UAMINIFU ni jambo muhimu sana katika mahusiano. Mara nyingi napenda sana niwe katika hali ambayo namuamini mpenzi wangu, pia napenda sana kwa gharama yoyote ile kumfanya mpenzi wangu aniamini. Kama nikigundua ana wasiwasi na kitu ninachomwambia huwa najitahidi kumwuliza aniambie nifanye nini ili aniamini sababu sipendi akae akiwa na wasiwasi, na ukweli nitafanya hicho kitu ili tu aridhike.

Inawezekana mimi nipo complicated kidogo, huwa napenda sana mtu aniambie ukweli hata kama ni mbaya kiasi gani. Kwa kuujua ukweli nakuwa na uhuru wa nini la kufanya baada ya hapo.... kukusamehe na kuendelea na mahusiano au kukusamehe na kusitisha mahusiano (kusamehe kwangu huwa siyo option, lazima nisamehe ili niweze kuendelea na mambo yangu mengine).

Katika huu uzi nitazungumzia sana uaminifu wa mambo ya kawaida tu, siyo kutoka nje ya mahusiano (cheating). Utakuta sometimes mtu anaamua tu kudanganya kwa sababu yoyote anayoijua. Kwa mfano mtu anamwambia mpenzi wake naenda sokoni wakati anaenda salon, au naenda kwa dada wakati anaenda kwa shangazi.

Hivi ikatokea ndo upo kwa shangazi halafu dada akaja nyumbani kukuulizia wakati wewe uliaga kwenda kwa dada itakuwaje? hata kama kweli mpenzi ataamini kuwa ulikuwa kwa shangazi, utakuwa umejenga hisia gani kwake kuhusu wewe? kwa nini umdanganye?
Wenzangu mnalizungumziaje hili?

Karibuni kwa mjadala

Kwa hiyo hata nikiulizwa umetoka wapi? Nitowe kavu kavu NATOKA KUNYA, eti sababu nimetokea chooni,
nikisema nimetoka kujisaidia itakuwa "too general"
 
ila ujue kuwa huyo unayemdanganya kwa kuepusha drama, akijua umendanganya yatakuwa ni majaaaaaaaaaaaaaaaaaanga sasa.
Hakuna mtu ambae hapendi trust kati ya mahusiano. Kila mmoja anapenda siku zote aambiwe ukweli. Upande wa mahusiano kutokuwepo na trust (nazungumza strictly nje ya) husababishwa na aidha mtu wako mwenyewe ama wewe mwenyewe. Kuna mwingine kweli anaweza sema anapenda awe anaambiwa ukweli no matter what! Cha ajabu ukweli ukitoka hapo si Drama hiyo itakayofuata - Kiasi kwamba huyo mtu anajuta anaona heri kuongopa. Take note sihalalishi kukosekana kwa uaminifu, ila najaribu kueleza why kwa wengine hua hawawi waaminifu.

Kikubwa cha kuelewa mahala ambapo hakuna trust ni ‘Kwa nini huyo mtu asiwe wazi na aongope katika suala ambalo ni la kawaida?”

Kukosekana kwa uaminifu kwa misingi ya wewe (ulie mpenzi wake)

Mara nyingi kuna masuala ambayo kimsingi ukiyaangalia yanaonekana madogo sana. Kama mfano uliotoa kwa kujifanya waenda Sokoni na hali waenda Salon. Hapo ni wazi kuwa sababu kubwa moja wapo inaweza kuwa huyo mwanamke huwa na matumizi makubwa na kuwa moja ya eneo ambayo anatumia sana pesa ni Saloon. Na wajua siye wanawake, kuna style inakuhiraji uende Saloon walau mara tatu kwa wiki. Inapotokea J/2 ulienda Saloon, J/5 ulienda Saloon na Leo Ijumaa unataka kwenda Saaloon na pengine ulishawahi ongea na mtu wako safari za Saloon zipungue (or hata hamjawahi ongea but wajishuku); the safest unaweza kuaga ni kuwa unaenda Sokoni badala ya Saloon.

Yes kaongopa it’s a bad thing, but ukiliangalia kwa upande mwingine unatkuta anaongopa tokana na kuwa Mpenzi wake kamuona si mwelewa, ama tu hataji kuonyesha ni to what extent hilo tendo la Saloon limepewa kipaumbele na the like.
Uongo wa disaini hii kati ya wapenzi wengi hauepkiki.

Kukosekana kwa uaminifu kwa misingi ya mpenzi wako

Kuna wengine siku zote wao kuongopa ama kutokuwa wazi ni hulka yao… Tena pengine inasukumwa saana na selfishness.. Kutotaka ajue vitu vyote anavyomiliki, Kutoka ajue wapi hua anaenda, kutoka ujue tu kwa sababu yoyote ile! Na mara nyingi pia pamoja na kuwa cheating imetolewa katika kuelewa kukosekana kwa uaminifu wa hivi – Mara nyingi cheating ndiyo sababu kubwa sana ya wapenzi kuwa waongo kwa wenza/partners wao.

Mfano kama mliwahi gombana kwa ajili ya mtu uliyemhisi ana interest na huyo mtu anafanya Hotel Magongo, siku akiwa Hotel Magongo si rahisi kusema kuwa yupo hapo. Ama anapokuwekea silent simu ama kutoweza kupokea sababu yupo faragha na mpango wa kando akipokea hawezi sema nilikuwa faragha, atasema lingine lolote ambalo mpenzi wake atalikubali bila shida.
 
ha haaa, ndo maana nikawaita warembo wangu mujionee mwenyewe denti, msije ingia kwa choo cha kiume, lol!

ila kuna uongo hua unafaida
unaweza sema uongo kuepusha kitu flani
so kuna faida na hasara pia za uongo!!
 
Kwa hiyo hata nikiulizwa umetoka wapi? Nitowe kavu kavu NATOKA KUNYA, eti sababu nimetokea chooni,
nikisema nimetoka kujisaidia itakuwa "too general"
mada inaongelea sema unaenda chooni, siyo umetoka wala siyo kufanya nini.....umenipata?
 

ila kuna uongo hua unafaida
unaweza sema uongo kuepusha kitu flani
so kuna faida na hasara pia za uongo!!
Msome royna hapo juu ya post yako......
huo uongo unaoona una faida je siku mtu akigundua ulidanganya atajisikiaje?
 
Last edited by a moderator:
ha haa, hapo mimi pia nipo guilty, sijawahi taja umri wangu wa kikweli lakini kwa wale ambao hawana tija......
tofauti na hao, mimi huwa naongeza angalau miaka isiyopungua 5....
kiukweli huwa sina sababu yoyote ya msingi ya kufanya hivyo, naamuaga tu, ila kwa vile haina madhara naona poa tu

haina madhara ndio, lkn kwanini udanganye? Kwa case yako hiyo ya kuongeza miaka lengo lake ni nini?? Na wewe unajaribu kuprove kuwa mkubwa kuliko hali halisi????? Sikuachi leo mpaka unipe majibu yatakayoniridhisha. LOL
 
leo naomba niseme hii, tangu nimeingia JF miongoni mwa wadada ninao wapenda ww ni mmoja wao. Unajua kwann? Bse una mambo kadhaa ambayo ninayapenda. Maisha yako huigizi (nionavyo mm)
Huu uzi umenigusa sn ila ctachangia bse nimelate na najua wadau wengi watakuwa wamesema mengi.
Ila unajua nn FP, uaminifu ni kitu kizur sn na unakuwa huru na maisha yako. Yaan huna hofu na uyatendayo.
Naunga mkono mada ni nzur.
 
Hivi trust ni ipi?
Ni kuiacha simu ya mpenzio iite aje apokee mwenywe hata wa manane?
Au kung'ang'ana kuipekenyuwa akiiacha mezani, labda kenda kuoga tu ivi?

Akumulikae mchana usiku atakuchoma!
 
leo naomba niseme hii, tangu nimeingia JF miongoni mwa wadada ninao wapenda ww ni mmoja wao. Unajua kwann? Bse una mambo kadhaa ambayo ninayapenda. Maisha yako huigizi (nionavyo mm)
Huu uzi umenigusa sn ila ctachangia bse nimelate na najua wadau wengi watakuwa wamesema mengi.
Ila unajua nn FP, uaminifu ni kitu kizur sn na unakuwa huru na maisha yako. Yaan huna hofu na uyatendayo.
Naunga mkono mada ni nzur.
hata sijui niseme nini hapa...... hii ni surprise.
nimefurahi kutambua unafurahia michango yangu hapa JF, asante sana.
Ukweli huwa nasemaga kama kuna mtu ananifahamu kiuhalisia akisoma post zangu lazima atajua ni mimi. sijawahi kufaulu somo la kuigiza, lol! na najiona nina amani sana kuwa real kuliko kuigiza...
Ukweli watu wengi tunapenda sana kuaminiwa na wenzetu na pia kuwa na mazingira ambayo unajua mwenzio ni mwaminifu, ingawa ni ngumu mno
 
Hakuna kitu kibaya katika mahusiano kama kusema uongo au kugundua umedanganywa...inapunguza trust kati ya wawili
Ni vyema mtu akawa muwazi kwani inaleta uhuru na itamfanya mtu kufanya mambo kkwa uwazi
If you are committed to someone kwanini unafichaficha vitu? Binafsi nalaani mauongo uongo
 
Back
Top Bottom