Trump amlima barua ya onyo kali Ayatollah Khamenei!!

Trump amlima barua ya onyo kali Ayatollah Khamenei!!

Mbona huko Yemen, Somalia na Gaza wanawasha mitambo tu kwenda kushambulia bila kutuma maombi ya kazi?
US yupo katika wakati mgumu, teknolojia za kijeshi zilizotishia dunia zamani, hivi sasa hadi vikundi kama houthi wanazo, mfano drones...

Ukiangalia hio barua ni kama Trump amenyoosha mikono kukubali lakini wakati huo huo hakukubali kuonekana mnyonge.. lakini US ina shida mno amani ipatikane ili shughuli za kiuchumi ziendelee..

Hapo bahari ya Shamu na Ghuba ya aden ni eneo/njia muhimu sana kiuchumi kwa usafirishaji wa bidhaa, hapo Houthi wanapiga meli za kijeshi na za kibiashara zenye mfungamano na Israel, USA na washirika wengine..

Hivi sasa inawabidi wapitie hadi rasi ya tumaini jema South Africa, njia ambayo ni ndefu sana.. hi inapelekea gharama za uchukuzi kuongezeka, bidhaa kupada bei na kuathiri uchumi.. hata kampuni zinazotoa bima za meli zimepanda kwa kiasi kikubwa...

Hapo sio mchezo...
 
Barua ya Trump kwa Khamenei wa Iran:

"Mheshimiwa Ayatullah Khamenei,

Kwa heshima ya nafasi yako na watu wa Iran, ninakuandikia ujumbe huu kwa lengo la kufungua upeo mpya wa mahusiano yetu, mbali na miaka ya migogoro na kutoelewana ambayo tumeshuhudia katika miongo kadhaa iliyopita. Wakati umefika wa kuachana na uadui na kufungua sura mpya yenye msingi wa ushirikiano na kuheshimiana. Leo pia, kuna fursa ya kihistoria mbele yetu.

Marekani, chini ya uongozi wangu, iko tayari kuchukua hatua kubwa kuelekea amani na kupunguza mivutano. Tunaweza kufanya kazi pamoja ili kuondoa vikwazo, kuwezesha uchumi wa Iran, na kufungua milango ya ushirikiano kati ya nchi zetu. Hii sio tu kwa maslahi ya watu wetu, lakini pia kwa maslahi ya utulivu na amani katika Mashariki ya Kati na dunia nzima.

Lakini nakuonya - ikiwa utakataa mkono huu ulionyooshwa, na ikiwa serikali ya Irani itachagua njia ya kuongezeka na kuendelea kuunga mkono mashirika ya kigaidi na matukio ya kijeshi, basi jibu letu litakuwa la kuamua na la haraka. Hatutasalia bila kazi mbele ya vitisho vya serikali yako kwa watu wetu au washirika wetu.

Amani sio udhaifu. Ni chaguo la wenye nguvu. Watu wa Irani ni watu wakubwa wanaostahili maisha bora ya baadaye, mbali na kutengwa, umaskini, na mateso.

Ikiwa uko tayari kujadili, tuko tayari pia. Lakini ikiwa utaendelea kupuuza matakwa ya ulimwengu, historia itarekodi kwamba ulikosa nafasi kubwa sana.

Kwa heshima."

Trump.
Fasihi iliyotumika katika uandishi wa barua hiyo nineipenda!

Ni fasihi bora iliyosheheni lahaja ya kidiplomasia na mamlaka ya wenye nguvu.
 
Trump ni muoga sana ,hapendi umwagaji damu anachofanya ni mikwala tu, ingawa US inauwezo wakutoa kipigo cha mbwa kwakoko kwa iran lakini inategemea na utashi wa rais aliye madarakani ,hapo anachofanya ni kumtishia nyau mtu mzima.
 
Iran kubwa jinga apeleke jeshi kwa wa Houth angalau tuone vita askari wa US wakizichapa.Imepita mudaatujaona mbungi.
 
US yupo katika wakati mgumu, teknolojia za kijeshi zilizotishia dunia zamani, hivi sasa hadi vikundi kama houthi wanazo, mfano drones...

Ukiangalia hio barua ni kama Trump amenyoosha mikono kukubali lakini wakati huo huo hakukubali kuonekana mnyonge.. lakini US ina shida mno amani ipatikane ili shughuli za kiuchumi ziendelee..

Hapo bahari ya Shamu na Ghuba ya aden ni eneo/njia muhimu sana kiuchumi kwa usafirishaji wa bidhaa, hapo Houthi wanapiga meli za kijeshi na za kibiashara zenye mfungamano na Israel, USA na washirika wengine..

Hivi sasa inawabidi wapitie hadi rasi ya tumaini jema South Africa, njia ambayo ni ndefu sana.. hi inapelekea gharama za uchukuzi kuongezeka, bidhaa kupada bei na kuathiri uchumi.. hata kampuni zinazotoa bima za meli zimepanda kwa kiasi kikubwa...

Hapo sio mchezo...
Jana kiongozi wa houthi alisema USA kazingirwa baharini na hatoweza pambana, wakati huohuo times of israel likaripoti kuwaomba Qatar waanzishe mazungumzo na Hamas,leo kuna taarifa za makubaliano ya eid na Trump barua ya mapenzi kwa ayatollah, kuna kitu hakiko sawa kwa mkubwa
 
Hapo usishangae hata Russia ikawa inawafadhili Houthis kwa hali na mali tokana na kileUS wanachokifanya kwenye vita ya Russia na Ukraine.
Hao Houthis hivi sasa wana missiles za kusafiri maelfu ya kilomita kupiga shabaha na kukwepa air defense..
Hii ina maana hawa jamaa wamekuwa hatari..

Hapo mkubwa inabidi awe mpole..
 
Ni kweli ila baada ya kujibiwa, iran haijajibu mpaka leo
Israel ilijibu kwa kuepuka kupiga miundombinu muhimu ya Iran kama visima vya mafuta na vinu vya nuclear, unajua ka sababu gani?
Ulikuwa ni mwanya mzuri kwa Israel kuipiga Iran kwenye miundombinu ya kiuchumi na sites za nuclear kama jinsi wengi ambavyo hamfahamu nini kingewakuta Israel..

Ndio maana waajemi walikausha, hapo penyewe Israel ilikuwa imeshashambuliwa mara mbili..
Kwa hio ukiwa muelewa utaelewa Israel iliepuka vita na Iran..

Kwa miaka mingi Israel ilikuwa ikiwaua wanasayansi wa Iran, Iran wanakausha, kumbuka uvumilivu una mwisho, hivyo Iran wapo macho wakisubiri Israel ijichanganye wapigwe true Promise 3...
 
Back
Top Bottom