Ni desturi ya muda mrefu kwa viongozi wa mataifa bila kujali dini zao wala madhehebu kumtembelea baba mtakatifu, kumsalimia na kupata baraka. Hivyo hivyo na papa nae anayo desturi ya kuyatembelea mataifa, kuyaombea na kuyabariki. Anafanya haya kwa mamlaka yake kama kiongozi wa taifa la vatikano, halifa wa petro mtume na mchungaji Mkuu wa Kanisa la Yesu Kristo. Haya hayahitaji nguvu kuyasadiki, kama si kwa moyo wala akili, macho yataona na masikio yatasikia kuwa ukweli ndio huo, hilo hata shetani analijua ndo maana tunawaona maajenti wake kila kona hadi huku mitandaoni wakitimiza maagizo ya baba yao Mkuu wa malango ya kuzimu, walifanya hivyo, wamefanya hivyo, wanafanya hivyo na watafanya tena na tena, uhakika kwa kanisa ni ahadi ya Bwana wake kwamba "HAWATASHINDA" Viva Christ, Viva Ecclesia.