POTOSHI Trump akimfokea aliyekuwa Makamu wa Rais Kenya, Rigathi Gachagua

POTOSHI Trump akimfokea aliyekuwa Makamu wa Rais Kenya, Rigathi Gachagua

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu habari,
Nimekwama hapa kupata details za kutosha kuhusu haya mazungumzo ya Rais wa Marekani Donald Trump na aliyekuwa makamu wa rais Kenya Rigathi Gachagua



1756382622516.png
 
Tunachokijua
Donald Trump ni Rais wa 47 wa Marekani ambaye alichaguliwa katika cheo hicho kupitia uchaguzi dhidi ya aliyekuwa makamu wa Rais Kamala Harris mwezi Novemba 2024, na kumfanya kuwa rais aliyechaguliwa kuhudumu mihula miwili isiyo isiyofuatana. Rais Trump alianza kutumikia muhula wake wa pili katika ikulu ya White House baada ya kuapishwa tarehe 20 Januari 2025 pamoja na Seneta wa Ohio, J.D. Vance, kama Makamu wa Rais.

Rigathi Gachagua alikuwa ni Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya ambaye alichaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Rais William Rutto kupitia tiketi ya chama cha United Democratic Party (UDA) na kushinda uchaguzi uliofanyika mwezi agosti 9 2022 hatimaye kuapishwa mnamo september 13, 2022.

Baadaye Gachagua, aliondolewa madarakani baada ya Seneti kuidhinisha uamuzi wa Bunge la Kitaifa wa kumng’oa Naibu Rais huyo kwa kupiga kura ya kumwondoa rasmi madarakani.

Video inayomhusisha Rais Trump na Rigathi Gachagua

Kumekuwepo na video inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Rais Trump akijibizana na Rigathi Gachagua ambapo Trump anamshutumu Gachagua kwa kuchochea siasa za kikabila na mgawanyiko na kuuliza ni kwa nini anawahusisha Wamarekani katika masuala ya Kenya.


Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search umebaini kuwa video hiyo ilichapishwa katika mtandao wa YouTube Agosti 18, 2025 ambapo ilikuwa Rais Trump na Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, walipokutana Ikulu ya White House katika chumba cha Oval Office kujadili namna ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine. Hata hivyo Gachagua hakuwepo kwenye mazungumzo hayo wala hata kwa kutajwa.

Vilevile kipande kinachomuonesha Gachagua kimebainika kuwa ni sehemu ya mahojiano aliyofanyiwa kupitia televisheni ya NTV Kenya inayoonekana kupandishwa Youtube Tarehe 27 Juni 2025 ambapo hakutoa kauli zilisikika ktika video hiyo.

Aidha sauti inayosikika haiendani na miondoko ya midomo jambo linaloonesha kuingizwa kwa sauti isiyohusika katika video hiyo hivyo kupotosha uhalisia.

Pia kifaa cha utambuzi wa maudhui yaliyotengenezwa kwa Akili Unde kinabainisha kuwa sauti katika video hiyo asilimia 99 imetengenezwa kwa Akili Unde.​

screenshot-2025-08-28-125118-png.3456242
Back
Top Bottom