Trump afungua jukwaa lake la mawasiliano

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
90
150
Aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump ameanzisha tovuti yake ya mawasiliano kwa lengo la kuchapisha taarifa “moja kwa moja kutoka mezani kwake.”

Trump, ambaye alifungiwa katika mitandao ya kijamii kwa kudaiwa kuchochea vurugu katika Jengo la Bunge la Marekani Januari 6 mwaka huu, anatumia tovuti hiyo kutoa taarifa zake, ambazo nyingi zinaendeleza alichokuwa akikisema wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kuwa ushindi wa Rais Biden haukuwa wa halali na kuwa kura ziliibiwa katika uchaguzi huo.

Jason Miller, mmoja wa washauri wa karibu wa Trump, ambaye aliwahi kusema kuwa Trump atafungua mtandao wake wa kijamii, amesisitiza kuwa tovuti hii si mtandao wa kijamii “mkubwa” ambao Trump aliuahidi awali, lakini amesema atatoa taarifa hivi karibuni kuhusu mtandao huo.

Wasomaji wa tovuti hii, iliyotengenezwa na kampuni ya huduma za kidigitali ya Campaign Nucleus inayomilikiwa na msimamizi wa zamani wa kampeni za Trump, wanaweza kusambaza taarifa hizo kupitia Facebook na Twitter.

Tovuti ya Trump inakuja saa chache kabla ya uamuzi wa bodi ya Facebook kutangaza ikiwa akaunti ya Trump ya Facebook itafungiwa moja kwa moja katika mtandao huo au la. Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa hii leo (Mei 5, saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki). Ikiwa atafunguliwa, Facebook itakuwa na siku 7 za kurudisha akaunti yake.

YouTube imesema kuwa inaangalia hali ya mambo na itarudisha akaunti yake ikiwa itajiridhisha kuwa hakuna tishio la kweli la kuchochea vurugu kutokana na maudhui ya Trump. Twitter kwa upande wake, imemfungia moja kwa moja Trump, aliyekuwa na wafuasi milioni 88 kutoka katika jukwaa lake.

Hata hivyo, msemaji wa Twitter amesema maudhui kutoka tovuti mpya ya Trump hayatazuiwa kupelekwa Twitter ikiwa hayatavunja sheria za mtandao huo.

Chanzo: BBC


1620192927328.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom