ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,321
- 50,538
Wakuu habari za majukumu,
Jana mida ya sa 11 jioni nimekutana na kimbwanga sio kidogo, nilikua najisaidia chooni (ni cha shimo kipo nje).
Ile nimeingia tu kusema nichuchumae nifanye yangu, la haulaaa! Kumbe kulikua na nyoka amejificha nyuma ya Mlango sikumbuki rangi yake kutokana na kupagawa ila size yake ya kawaida sio mkubwa kivile, nilimwona tu akafanya kama anajibana ukutani, mimi nikapiga kelele (mama weeeeeh)..
Bahati nzuri hakuniuma ila alirusha kitu kwa juu nadhani ndo sumu yenyewe uzuri na yenyewe ikanikosa nilipoona kachelewa timing mimi huyo ni kakimbia kuelekea nje speed speed..nikaupigiza mlango japo niliumia kidole kwenye ngazi za kuingilia chooni nikamfungia kwa ndani.
Muda huo huo kulikuwa na mafundi kwa nje wanatengeneza gari nikawaita haraka tukaue nyoka tumeingia chooni tumemtafuta tumemkosa. Mazingira ya nyumbani sio rahisi kwa kweli nyoka kuingia ndani hata ya get la nyumba. Basi kama unavojua waswahili sisi wapana hatuna dogo wakaja watu tumewaambia wamehusanisha tukio na imani za kishirikina. Nimekosa amani kwa kweli
Wajuvi wa mambo hizo niambieni kama ni tukio la kawaida au laaah!
Kinachonisumbia zaidi ni jinsi nyoka huyo alivopotea kimagendo. Watu wote tumeshangaa tu najiuliza ina maana karudi ndani ya shimo au na ndipo ilipo maskani yake kwenye kinyesi? Maswali mengi no ufumbuzi na watoto wa nyumbani wameogopa kuingia toilet wanaenda kwa jirani.
Kina mshana Jr haya sio mambo ya giza kweli