mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,811
- 11,032
Hata kinyume chake ni shida tu, yaani kama hazikuwepo halafu ghafla zikajaHaswa kama zilikuwepo alafu ghafla uelekeo ukabadilika.

Aisee safi sana hiyo, Ushirikiano ndio sababu ya kuwa pamoja.Wanaume ni providers kwenye nyumba hii ni natural, mwanaume anapokosa kipato inamsumbua sana psychologically, unaweza kukuta hata anashindwa majukumu mengine ya ndoa kwa msongo wa mawazo.
Hii story ya rafiki yako Eve ilimtokea binamu yangu. Yeye aliligundua hilo mapema na aliamua kumpa mshahara mume wake na wanapanga budget pamoja. Walitoa pesa za matumizi ya ndani na mama alibaki na kidogo ya mfukoni na baba pia. Yule mwanaume alikua na masters in engineering lakini aliamua kutafuta course ambayo ingempa ajira kwa haraka mjini Dar ili asiwe mbali na familia. Alianza kusoma IFM na mke akawa analipa ada. Sasa hivi yote ni historia lakini ni muhimu kumpa ushirikiano mwenza anapokuwa na matatizo.
Kabisa mkuuAisee safi sana hiyo, Ushirikiano ndio sababu ya kuwa pamoja.
Balaa tupu yaani, mzima lakini my dada?Hahaaaa!! Zikiwepo taabu, zisipokuwepo pia taabu.
Habari za muda huu wapendwa wa jukwaa hili!!
Miaka kadhaa iliyopita nilikutana na rafiki yangu Eva(sio jina halisi), tumekuwa marafiki sasa takribani miaka10. Eva aliolewa mara tu tulipohitimu chuo,mumewe alikuwa ameajiriwa kitengo kizuri tu katika kampuni fulani kwahiyo pesa haikuwa tatizo. Miaka miwili baada ya kuhitimu masomo yake na akiwa ktk ndoa alifanikiwa kupata kazi katika kampuni fulani ambapo mumewe alichangia kwa kiasi fulani yeye kuipata kazi hiyo.
Ndoa yao ikiwa na miaka mi4 na wakiwa na watoto wawili, mumewe alipatwa na matatizo kazini na akasimamishwa kazi. Kama ilivyo ada ya sisi waajiriwa kujisahau angalau kuwa na kamradi na kuridhika na mshahara tu ndivyo ilivyokuwa kwa Eva na mumewe. Hali ilibadilika ghafla nyumbani maana walishazoea maisha ya aina fulani hivi.
Hali ilikuwa mbaya zaidi kwa upande wa mwanaume kama kichwa cha familia, alivurugwa na frastrations kiasi kwamba ikapelekea hata maelewano baina yao kuwa mabovu. Ilifikia hatua Eva alikata tamaa na kutaka kuachana na mumewe. Maana alijiona mwenye mzigo mzito wa kulea familia nzima na mume asie na kazi.
Ndipo siku moja alinipigia simu na kuniomba tuonane as ana mazungumzo muhimu nami,she needs a person to talk to as anahisi kuchanganyikiwa. Alinielezea hali nzima ya nyumbani na jinsi alivyo na wakati mgumu hivyo ameamua aachane na mumewe maana hawezi tena. Nilimuuliza kama kweli hilo ndilo analolitaka na kama anaona ni uamuzi sahihi. Akadai japo ni uamuzi ambao haufurahii lakini inabidi auchukue.
Nilijaribu kumuuliza ni njia gani haswa ambazo amekwisha zitumia kumsaidia mumewe,alinijibu kuwa amemshauri atafute kazi nyingine na ikibidi amtafute councelor amsaidie. Hapo ndipo nilipogundua tatizo lilipo. So nilimwambia natambua she is frastrated ila mumewe yuko frastrated zaidi yake. Na the best councelor kwake kwa sasa ni yeye mkewe, na kitendo cha kuamua kumuacha kingemuumiza zaidi maana ndicho kipindi anachomuhitaji zaidi. Na ndio kipindi anapaswa kuitimiza ahadi yake na kiapo chake cha kuwa nae ktk shida na raha.
Tuliongea mengi mno ila nilimsisitiza kwanza yeye binafsi kuikubali hali ile na kuchukua hatua za kumsaidia mumewe kwa kuwa karibu nae, kuwa the best friend she could ever be, wazungumze na watafute suluhisho ikiwezekana waangalie nje ya kuajiriwa. Na kingine ni kujiadjust kuishi kulingana na hali halisi waliyonayo haswa kwa kipindi hicho cha mpito.
Nashukuru after a very long talk alinielewa na kuamua kuvaa viatu vyake kama mke na kupambana ktk kumsaidia mumewe huku akihangaika kuilea familia.
Leo ni miaka mitatu tangu wapitie ktk mapito hayo na kwasasa hali ni shwari na kwakweli wanakoelekea kunatia moyo. Jana ilikuwa ni annivesary yao ya miaka7 ya ndoa yao na alinitumia ujumbe wa kunishukuru kwa kuwa a good friend she cud ever have, na akanieleza kuwa ilibidi amueleze ukweli mumewe kuwa walipokuwa wakipitia kipindi kigumu alifikia uamuzi wa kumuacha ila thanks to me nilimsaidia kuweza kuutengua uamuzi huo, ila mumewe alimjibu kuwa anamshukuru yeye zaidi kwani pamoja na ushauri wangu bado muamuzi wa mwisho alikuwa yeye na angeweza kuukata ushauri huo.
Nilifurahi sana kusikia kuwa i did something ktk maisha yake(japo sikuwa hata na wazo tena) na nilimuomba kushare this in here maana inaweza kumsaidia mtu ambae anapitia maybe situation kama yake au inayokaribiana na hiyo na aweze kuona kuwa hapaswi kukata tamaa as there is always a way, mambo yanapoonekana kuwa magumu sana basi mwisho wa ugumu huo hauko mbali na ndicho kipindi mnapaswa kuwa pamoja na imara zaidi na zaidi ili kuvuka salama.
Niwatakie week end njema.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]why kila story jamii forums mtu akimaliza chuo tu lazima hapate kazi mbona mtaa watu hawana kazi huku
hii chai hii
na wewe umeolewa au???Habari za muda huu wapendwa wa jukwaa hili!!