True story;inasikitisha sana,nani alaumiwe

Kima mdogo

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
303
46
Wanandoa hawa walikutana na wakiwa na hali duni kimaisha, wakaoana na kujaliwa kupata mtoto 1 wakike,kadri siku zilivyoenda MUNGU akawajalia wakafanikiwa kimaisha na wanamiliki mali kadhaa,miaka 7 ikapita mke akabeba mimba kwa bahati mbaya mimba ikatoka, akamweleza mama mkwe wake hapo ndo matatizo yalipoanza,Mama mkwe na Mume wakaanza kumsengenya kuwa hazai,mama mkwe akafikia hatua ya kusema mwanae aoe mwanamke mwingine,Mke akawa analia na Mungu kila siku,Siku 1 mama mke akaja akamkuta mke huyo anaumwa akasema wala haumwi ni mamizimu ya huko kwao,huyu dada aliumia sana kwani hajui uchawi wala mizimu akamweleza mumewe maneno aliyoongea mama yake,mume kumuuliza mama yk akakataa katakata na kudai kuwa mwali wake kamsingizia ili asije kwa mwanae, kwa bahati nzuri Mke akapata ujauzito mume wake akaanza kumnyanyasa,kumtukana na kumnyima hela ya matibabu kwa shinikizo la mama yk kuwa alimsingizia, mke huyu akawa analia kila siku hali iliyomletea matatizo makubwa madaktari wakamzalisha mtoto wa miez 7
 
Hili ni moja ya majanga ya kitaifa. Nazifahamu familia zaidi ya nne ambazo mama wakwe wamekuwa powerful sana katika nyumba za watoto wao sijui ni lini wanaume wetu watakuwa na sifa kama zile za Babu DC, looh!!
 
Wanandoa hawa walikutana na wakiwa na hali duni kimaisha, wakaoana na kujaliwa kupata mtoto 1 wakike,kadri siku zilivyoenda MUNGU akawajalia wakafanikiwa kimaisha na wanamiliki mali kadhaa,miaka 7 ikapita mke akabeba mimba kwa bahati mbaya mimba ikatoka, akamweleza mama mkwe wake hapo ndo matatizo yalipoanza,Mama mkwe na Mume wakaanza kumsengenya kuwa hazai,mama mkwe akafikia hatua ya kusema mwanae aoe mwanamke mwingine,Mke akawa analia na Mungu kila siku,Siku 1 mama mke akaja akamkuta mke huyo anaumwa akasema wala haumwi ni mamizimu ya huko kwao,huyu dada aliumia sana kwani hajui uchawi wala mizimu akamweleza mumewe maneno aliyoongea mama yake,mume kumuuliza mama yk akakataa katakata na kudai kuwa mwali wake kamsingizia ili asije kwa mwanae, kwa bahati nzuri Mke akapata ujauzito mume wake akaanza kumnyanyasa,kumtukana na kumnyima hela ya matibabu kwa shinikizo la mama yk kuwa alimsingizia, mke huyu akawa analia kila siku hali iliyomletea matatizo makubwa madaktari wakamzalisha mtoto wa miez 7
Kwa hiyo na hadithi yako ndiyo imeishia hapo?
 
hivi wa mama wanafanyaga nini kwenye nyumba za watoto wao?? katembee siku mbili rudi kwako! MUUMBA WANGU JUU NAMUOMBA SANA ANIPE JAPO BANDA LA KUZEEKEA! sitaki kuwa kikwazo kwa ndoa za wanangu, AMEN!
 
hivi wa mama wanafanyaga nini kwenye nyumba za watoto wao?? katembee siku mbili rudi kwako! MUUMBA WANGU JUU NAMUOMBA SANA ANIPE JAPO BANDA LA KUZEEKEA! sitaki kuwa kikwazo kwa ndoa za wanangu, AMEN!

kweli mamito kuna wa mama wengine wachimvi kwa kuharibu ndoa za wanae...... kuna wengine hadi raha utafikiri mtu na bintiye wa kuzaa lakini hao ni moja ya elfu
 
Mtu akioa/kuolewa lazima aondoke kwa wazazi wake nae ambatane na mke wake! Huyo kijana anatakiwa afanyiwe SENDOFF PARTY achane na mama yake.
 
hivi wa mama wanafanyaga nini kwenye nyumba za watoto wao?? katembee siku mbili rudi kwako! MUUMBA WANGU JUU NAMUOMBA SANA ANIPE JAPO BANDA LA KUZEEKEA! sitaki kuwa kikwazo kwa ndoa za wanangu, AMEN!
Hivi unayeongea haya ni Mzazi kweli? Huwa nashangaa watu ambao hawataki wazazi wao waje kwenye familia zao, eti aje tu kusalimia siku 2 ya tatu arudi! What a nonsense! Hivi hujui kuwa wazazi wakizeeka wanageuka kuwa watoto wanaohitaji uangalizi wa karibu wa walezi wao? Yaani unataka hata kama Mzazi anaumwa akaugulie kwake, kweli? Ni upuuzi gani huu? Hivi wazazi nao wangekutelekeza ulipokuwa mdogo ukaugulie kwa watu ungefika hapo ulipo? Huna tofauti na kijana aliyekua kwa kulelewa kwa taabu na Mama yake halafu akiwa mkubwa na kuoa mwanamke anaingia na kumwambia "unajua Mama yako ni mchawi?". Mme ***** naye huyu anakubali, aaaah kweli, ndio maana hata hatuendelei au tunazaa watoto wanakufa, mara na mimi nilishawahi kusikia, mara na majirani/ndugu huwa wanamsema hivyo hivyo, n.k. Hivi angekuwa mchawi ungekua? Yaani Mama aone umuhimu wa kukulea wewe halafu aje aroge watoto wako? Mbaya zaidi wewe uliyekaa na Mama yako kwa miaka zaidi ya 25 hukujua uchawi wake ila alipoingia Mke ndipo yeye akaugundua kuwa Mama yako ni mchawi tena ndani ya miezi 3 tu! Na kibaya zaidi, Mama za akina Baba ndio huwa eti wanavuruga ndoa za kijana wao, ila wazazi+ndugu wa mke wao hawana shida!!!!!!! Eti Mama aliyeweza kulea ndoa yake kwa zaidi ya miaka 40 akiwa na Baba yako leo hii wewe mwenye kandoa ka mwaka 1 unamuona huyo Mama hajui maana ya ndoa, mara kapitwa na wakati (wakati yeye alipokuwa anaishi wewe hukuwepo, hata hiki kipindi unachoishi wewe na yeye anaishi... sasa sijui hapa nani aliyepitwa na wakati!). Na wanaume wapuuzi kama Cacico wanaitikia, "sawa mke wangu, nitamsafirisha mama yangu arudi kijijini, kwanza msimu wa mvua umekaribia aende akaandae na mashamba!". M.p.u.m.b.a.v.u wewe, yaani mimi nikiwa na kijana wa namna hii hakika nam-disown na kamwe asije akakanyaga hata kwenye kaburi langu! To me, parents first, any other creature should come afterward! Jaribuni huo upuuzi wenu muone kama mtakuja lea hata watoto wenu kwa amani! Chezea wanawake wewe? Muulize Adam na Samson juu ya nguvu ya Mwanamke!
 
Hivi unayeongea haya ni Mzazi kweli? Huwa nashangaa watu ambao hawataki wazazi wao waje kwenye familia zao, eti aje tu kusalimia siku 2 ya tatu arudi! What a nonsense! Hivi hujui kuwa wazazi wakizeeka wanageuka kuwa watoto wanaohitaji uangalizi wa karibu wa walezi wao? Yaani unataka hata kama Mzazi anaumwa akaugulie kwake, kweli? Ni upuuzi gani huu? Hivi wazazi nao wangekutelekeza ulipokuwa mdogo ukaugulie kwa watu ungefika hapo ulipo? Huna tofauti na kijana aliyekua kwa kulelewa kwa taabu na Mama yake halafu akiwa mkubwa na kuoa mwanamke anaingia na kumwambia "unajua Mama yako ni mchawi?". Mme ***** naye huyu anakubali, aaaah kweli, ndio maana hata hatuendelei au tunazaa watoto wanakufa, mara na mimi nilishawahi kusikia, mara na majirani/ndugu huwa wanamsema hivyo hivyo, n.k. Hivi angekuwa mchawi ungekua? Yaani Mama aone umuhimu wa kukulea wewe halafu aje aroge watoto wako? Mbaya zaidi wewe uliyekaa na Mama yako kwa miaka zaidi ya 25 hukujua
chezea mama wakwe wewe
 
Bila shaka huyo mama ni mjane, angekuwa na mumewe huo muda wa kwenda kunyanyasa mkwewe wala usingekuwepo
 
kweli mamito kuna wa mama wengine wachimvi kwa kuharibu ndoa za wanae...... kuna wengine hadi raha utafikiri mtu na bintiye wa kuzaa lakini hao ni moja ya elfu

Mara nyingi hawa wanakuwaga wakina-mama wale ambao walijifanya 'hawataki' waume/kuolewa bali wanataka mtoto tu, anapompata huyo mtoto ndio anamuwa 'man of her life'...sasa akiona tu kakua anahamisha 'attention' kwa mwanamke mwingine (mkewe) basi hapo ndio 'kuweweseka' na 'kisebusebu' juu. Na mara nyingi hao wanaume kwa sababu wamekulia katika mazingira ya mama tuuu, wanawasikiliza hata wanpoona kuwa mama hapa yuko wrong! Matokeo ndio haya...

Hii tabia ambayo imezoeleka sana siku hizi wanawake hasa 'independent' (sio magolikipa) kujifanya hawahitaji mwanaume maishani mwao wanahitaji tu mtoto....itakuja kutuletea mabalaa sana huko baadae, wanaume wa design hii na magay/lesbian wengi tu watajaa!
 
Haya ndiyo makosa yanayotokana na kuruhusu third party [be it yr mom+rltives or hers}
Marriage is a bond between 2 parties a man and a woman only.
Ukiruhusu ndugu marafiki kuingilia maisha yenu mwisho siyo mzuri. Kwenye hili mwanamume ndiye anayepaswa kuonyesha njia?
Ukisha kuwa firm matatizo yote yataisha. Mimi hayo yalinikuta kwani nimeoa mwanamke ambaye tumetofautiana dini, mila, utamuduni. Tulivyooana tuu matatizo yalianza toka kwa dada zangu zikafika hadi kwa mama yangu. aliyekuwa ananielewa alikuwa ni baba yangu tuu. One fine day tulikuwa na family gathering na kwa bahati mbaya dada yangu mmoja akasema neno dhidi ya mke wangu ambalo kwa kweli ilikuwa ni kumuonea kitu nilicho kifanya na kwanza kuwaambia ndugu zangu wote kuwa huyo ndiye mke wangu mpendwa na niko tayari hata kuwakosa wao kama itafika mahala ambapo itabidi nichague. Na niliwaambia sitaki kusikia mtu yeyote anamdhalilisha mke wangu hata akiwa ni mama yangu. Kama kuna tatizo niambiwe mimi mwenye mke. Baada ya hapo nilipunguza kabisa hata kuwatembelea ndugu zangu lakini mwisho wa yote hivi sasa mke huyohuyo ndiye kipenzi cha mama yangu na dada zangu.
 
Imeandikwa wapi labda kuwa mwanaume akioa aendelee kukaa na mama yake au kupokea amri zake?
Tunapenda sana kupotoshana.we kama unaishi na watu vizuri utatunzwa tu kokote uliko,tena watakuwa na hamu na wewe.

Imeandikwa mtu aliyebarikiwa huacha urithi kwa watoto wa watoto wake,badala yake unakimbia majukumu yako unaanza kubebesha watu mizigo na wivu wa watu wenye laana.
Acheni kutesa wanawake wenzenu bila sababu nyie wamama wakwe,hamna hata kigezo kinachowalinda kufanya hivo,ni kuwa wicked tu.

Wanawake wengi huwa wanaheshimu wakwe zao lakini anahesabiwa km ni mtumwa kufanya vile na hana haki yoyote.
Ukiwachunguza hawa wanaotesa wake za watoto wao huko nyuma wao wameishije. Na wakwe utabaki mdomo wazi.
Mi naliona km hili swala ni moja ya majanga tuliyo nayo.
 
Wa kulaumiwa mwanaume kwanini amtese mke wako kwa kusikia maneno ya watu
 
Back
Top Bottom