Vladmir Putini
JF-Expert Member
- Mar 22, 2022
- 777
- 1,442
Heshima yenu wana JF.
Kuna ka-utamaduni flani kamejengwa na jamii zetu za Kiafrica ambacho ni cha kipuuzi na wahusika inabidi wabadilike.
Kumekuwa na utamaduni kwamba, mwanaume anapo oa halafu mkewe akapata uja uzito, basi anamrudisha kwao (kwa wazazi wa mke) akahudumiwe huko mpaka atakapo jifungua na afya yake kuwa sawa.
Huu ni upuuzi na kuwapa mzigo upande wa mama mkwe wako bila wewe mwanaume kujua.
Kwani wewe mwanaume huwezi kumpeleka huyo mkeo kwenu (wazazi wako) akatunzwe huko?
Unampelekea mama mkwe wako mzigo ambao chanzo ni wewe, mama wa watu huenda umri umeenda miaka zaidi ya 65,70 eti akakutunzie mkeo kisa mja mzito alafu wazazi wako wewe mwanaume wanakula utawala tu, huu ni usenge.
Kwanini usimpelekee mama ako ahangaike nae na badala yake unampelekea mama mkwe wako akahangaike nae tena.
Yaani mke umepewa umeoa, alafu umemjaza mimba unamrudisha kwao akatunzwe, mpuuzi kabisa, mpeleke kwa mama ako huko na yeye akapate shida siyo kumpa mzigo mama mkwe wako.
USHAURI WANGU KWA WANAUME WALIO- OA : Ukiona umeshaoa umemchukua mwanamke kutoka kwao, basi jua kuwa huyo ashakuwa mali yako na kwa shida na raha yeyote unawajibika wewe mwanaume.
Bora kama yamekushinda majukumu mengi labda unayo, in case of ugonjwa, mimba au tatizo lolote linalomhusu mkeo bora umpeleke kwenu (kwa wazazi wako mwanaume) na siyo kumpeleka kwao (wazazi wake mwanamke).
Bora uwape wazazi wako, dada zako, ndugu zako mzigo wa kumtunza mwanamke wako mja mzito kuliko kuwapa mzigo wazazi/ndugu wa upande wa mke wako.
Regardeless unatuma matumizi n.k but usimrudishe mwanamke kwao kwa sababu za ujauzito wako au ugonjwa ili akatunzwe, bali mrudishe kwenu siyo kwao.
Kama unamchukua mtu aje akutunzie kwako basi chukua mtu kutoka upande wa familia yako mwanaume na siyo familia ya mwanamke.
Tumia familia ya mwanamke ikiwa huna chaguo la mwisho tena, yaani no option tena.
Siyo unamjaza mtoto wa watu mimba halafu unakimbilia kumrudisha kwao akajifungue kwa sababu hakuna wa kumtunza hapo nyumbani.
Unaenda kumpa mzigo m-mama wa watu ana miaka 70 ahangaike hadi kumfulia mkeo, kumpikia sometimes na kuchota maji huko vijijini ambako maji ni shida alafu wewe unaona poa kwamba si yupo kwao na huyo ni mwanae, hizi shida mpelekee mama ako mzazi akakomae nae ili uone kuwa siyo rahisi.
Ni upuuzi na ujinga kabisa, au unamchukua mama mkwe wako unamleta kwako akutunzie mkeo mjamzito au mgonjwa, bila kujua kuwa aliyemchukua kuna wanao mtegemea huko akiondoka yeye kuna majukumu yanalala.
Mchukue mama ako au ndugu kutoka upande wa familia yako waje wakutunzie mkeo na siyo kumchukua mama mkwe au ndugu wa upande wa mke.